Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Luhaga Mpina (wa tatu kushoto) akitoa tuzo kwa Mshindi wa kwanza wa
Fahali bora kutoka Mbozi, Mkoani Iringa, Abraham Mwalutende wakati wa maonesho
ya Ng`ombe Bora wa Maziwa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane
jijini Dodoma juzi.Wapili Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa
ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith na Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa
Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.
Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Luhaga Mpina (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi
ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dk. Eligy Shirima alipokwenda kufungua
rasmi Maonesho ya Ng`ombe Bora wa Maziwa Tanzania yaliyofanyika katika
viwanja vya Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma jana. Katikati ni Mkurugenzi wa
Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (IRLI), Dk. Jimmy Smith.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia) akizungumza
wakati wa maonesho ya Ng`ombe Bora wa Maziwa yaliyofanyika katika
Viwanja vya Nanenane jijini Dodoma juzi. Wengine kutoka kulia ni, Mkurugenzi wa
Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith; Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa
Mifugo Tanzania (TALIRI), Dk. Eligy Shirima na Msimamizi wa Mradi wa Utafiti wa
Vinasaba vya Ng`ombe wa Maziwa kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa
Mifugo (ILRI), Dk.Okeyo Mwai.
Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Luhaga Mpina (katikati) akitoa tuzo kwa Mshindi wa kwanza wa ng`ombe
bora wa maziwa kutoka Meru, Mkoani Arusha, Emmanuel Nanyaro wakati wa maonesho
ya Ng`ombe Bora wa Maziwa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane jijini
Dodoma juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo
(ILRI), Dk. Jimmy Smith.
Naibu Waziri wa Mifugo
na Uvuvi, Abdallah Ulega (kushoto), akihutubia wakati wa uzinduzi wa maonesho
ya Ng’ombe bora wa maziwa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo
Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo
(ILRI) pamoja na wadau kutoka maeneo mbalimbali katika Viwanja vya NaneNane
Mkoani Dodoma juzi.
Mkurugenzi wa Taasisi
ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith (kushoto),
akihutubia wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Ng’ombe bora wa maziwa
yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa
kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) pamoja na
wadau kutoka maeneo mbalimbali katika Viwanja vya NaneNane Mkoani Dodoma juzi.
Mkurugenzi Mkuu wa
Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dk. Eligy Shirima akizungumza
katika hafla hiyo.
Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Luhaga Mpina (katikati) akipongezana na Mkurugenzi wa Taasisi ya
Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith wakati wa ufunguzi rasmi
Maonesho ya Ng`ombe Bora wa Maziwa Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya
Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma jana. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Abdallah Ulega.
No comments:
Post a Comment