BANDARI YA DAR ES SALAAM KIUNGO MUHIMU KATIKA KUIMARIKA KWA NAFASI YA AFRIKA MASHARIKI KATIKA BIASHARA YA KIMATAIFA – ABSA

DAR ES SALAAM, TANZANIA — Afrika Mashariki inazidi kujitokeza kuwa daraja la kimkakati linalounganisha Afrika na masoko ya dunia, huku mvutano wa kisiasa na kiusalama duniani, mabadiliko katika minyororo ya ugavi na jitihada za kutafuta njia imara zaidi za biashara vikiendelea kubadilisha mwenendo wa uchumi wa dunia.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mashirika Makubwa wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Nellyana Mmanyi, ambaye amesema mazingira yanayobadilika ya biashara duniani yanaipa Afrika fursa kubwa ya kuimarisha nafasi yake si tu kama chanzo cha malighafi na soko linalokua la watumiaji, bali pia kama kitovu cha uzalishaji na kiunganishi cha kimkakati kati ya masoko makubwa duniani.

Bi. Nellyana alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa GTR East Africa 2026, uliofanyika hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya, ukiwakutanisha watunga sera, taasisi za fedha, makampuni, wawekezaji na wadau wengine kutoka sekta za biashara, bidhaa, minyororo ya ugavi, miundombinu na ufadhili wa mauzo ya nje.

Uwasilishaji wake ulifanyika wakati ambapo kampuni duniani zinazidi kutafakari upya namna na maeneo wanakopata bidhaa, wanakotengeneza bidhaa na jinsi bidhaa hizo zinavyosafirishwa kuvuka mipaka.

Kwa mujibu wa Bi. Nellyana, mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi duniani yanazisukuma kampuni kutafuta njia mbadala za minyororo ya ugavi na kupunguza utegemezi kwa nchi moja, hali inayofungua fursa mpya kwa maeneo yenye uwezo wa kutoa uzalishaji wa kuaminika, miundombinu imara na fursa ya kufikia masoko.

Kwa Afrika, hili si jambo la kuvuruga tu mifumo iliyopo; ni fursa ya kimkakati,” alisema Bi. Nellyana.

Alisema Afrika Mashariki iko katika nafasi nzuri zaidi ya kunufaika na mabadiliko hayo kutokana na eneo lake la kijiografia, kuongezeka kwa ukubwa wa masoko, kuimarika kwa ushirikiano wa kikanda pamoja na uhusiano wake na Mashariki ya Kati na Asia.

Kwa Tanzania, fursa hiyo inahusishwa kwa karibu na nafasi ya nchi kama lango la kufikia baadhi ya masoko yanayokua kwa kasi na yenye umuhimu mkubwa kimkakati barani Afrika.

Bi. Nellyana aliitaja Bandari ya Dar es Salaam kuwa lango muhimu la kuingiza na kusafirisha bidhaa katika ukanda huo, likihudumia biashara ya Tanzania pamoja na nchi zisizo na bandari, zikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia, Uganda na Rwanda.

Umuhimu wa Bandari ya Dar es Salaam unaongezwa na uwekezaji unaoendelea katika njia za usafirishaji zinazoiunganisha bandari hiyo na masoko ya ndani ya ukanda.

Kwa mfano, Bandari ya Dar es Salaam ni lango muhimu linalohudumia masoko yasiyo na bandari kama DRC, Zambia, Uganda na Rwanda,” alisema.

Katika muktadha huo, Ukanda wa Kati, inayounganisha miundombinu ya bandari za Tanzania na masoko ya ndani ya Afrika Mashariki na Kati, una uwezo wa kuwa njia kuu na muhimu zaidi ya biashara ya kikanda.

Ukanda wa Kaskazini ya Kenya inatekeleza jukumu linalokamilishana na Ukanda wa Kati, na hivyo kuimarisha nafasi ya Afrika Mashariki kama mtandao wa njia za biashara zilizounganishwa badala ya kuwa mkusanyiko wa masoko ya kitaifa yaliyotengana.

Uchambuzi wa Absa kuhusu GTR East Africa 2026 umeonyesha umuhimu wa kuwa na minyororo ya ugavi inayoweza kustahimili misukosuko, upatikanaji wa fedha kwa ajili ya minyororo ya ugavi ya kikanda na uwekezaji katika miundombinu ili kuimarisha nafasi ya ukanda katika biashara.

Hata hivyo, Bi. Nellyana alionya kuwa Afrika haitanufaika moja kwa moja na mabadiliko yanayoendelea katika biashara ya kimataifa bila kuchukua hatua madhubuti.

Alisema wafanyabiashara barani Afrika bado wanakabiliwa na changamoto kubwa katika kusafirisha bidhaa kuvuka mipaka, zikiwemo mifumo isiyokuwa na ufanisi ya usafirishaji na ugavi, ucheleweshaji wa forodha, tofauti za kanuni kati ya nchi, vikwazo visivyo vya ushuru, sera zisizokuwa na ulinganifu na gharama kubwa za usafirishaji wa bidhaa kutoka maeneo ya ndani hadi masokoni.

Vikwazo vya miundombinu pia vinaendelea kuwa changamoto, hususan pale msongamano bandarini, mifumo isiyokuwa na ufanisi ya reli, barabara zisizo katika hali nzuri na ukosefu wa miunganisho bora vinapoongeza gharama na muda wa kusafirisha bidhaa.

Kwa biashara ndogo, changamoto hizo zinaweza kuwa kubwa zaidi kutokana na upatikanaji mdogo wa mtaji wa uendeshaji na fedha za biashara, hali inayoweza kuzifanya zishindwe kutumia fursa zilizopo katika masoko ya nchi jirani.

Kuna mahitaji ya bidhaa zao, lakini wanakabiliwa na changamoto katika utekelezaji wa biashara kuvuka mipaka,” alisema Bi. Nellyana.

Alisisitiza pia umuhimu wa kuifanya AfCFTA (Eneo Huru la Biashara Barani Afrika) kutoka kwenye ahadi za kisera na kuwa utekelezaji wa vitendo, ikiwemo kupunguza vikwazo visivyo vya ushuru na kurahisisha biashara kati ya nchi za Afrika.

Kadri njia za biashara zinavyozidi kuwa changamano, Bi. Nellyana alisema benki zina jukumu muhimu la kusaidia wafanyabiashara kudhibiti hatari na mahitaji ya kifedha yanayohusiana na biashara ya kuvuka mipaka.

Alisema bidhaa za kawaida za kibenki pekee hazitatosheleza mahitaji ya wafanyabiashara katika mazingira ambapo wanahitaji huduma jumuishi zinazohusisha ufadhili wa biashara, huduma za fedha za kigeni, mtaji wa uendeshaji na utaalamu kuhusu masoko.

Absa tunaona ongezeko la mahitaji kutoka kwa kampuni ya huduma jumuishi za kibenki zinazosaidia biashara kuvuka mipaka, zikichanganya ufadhili wa biashara, huduma za fedha za kigeni na utaalamu wa masoko ya kikanda,” alisema.

Kwa mujibu wake, wafanyabiashara wanazidi kutafuta washirika wa kifedha wanaoweza kuwasaidia katika safari nzima ya biashara, kuanzia upatikanaji wa malighafi na uzalishaji hadi usafirishaji, malipo na kuingia katika masoko mapya.

Hii ina maana kwamba benki zinahitaji kwenda zaidi ya bidhaa za kawaida kama hati za malipo za biashara na mikopo ya overdraft, na badala yake kubuni suluhisho za ufadhili wa biashara zilizo rahisi kubadilika na zenye kuendana na mahitaji ya mteja.

Kasi ya huduma ni jambo muhimu la kutofautisha. Mwisho wa siku, benki inayochukua hatua kwa kasi zaidi ndiyo inayompata mteja,” alisema Bi. Nellyana.

Bi. Nellyana alitaja maeneo matano muhimu yatakayoamua iwapo Afrika inaweza kubadili mazingira mapya ya biashara duniani kuwa fursa ya ukuaji endelevu wa uchumi.

Kwanza ni utekelezaji madhubuti wa AfCFTA na kuondoa vikwazo vinavyofanya biashara kati ya nchi za Afrika kuwa ghali na changamani.

Pili ni maendeleo ya miundombinu, hususan bandari, reli na nishati. Alisema uwekezaji huo unapaswa kuleta kasi na ufanisi zaidi katika usafirishaji wa bidhaa, badala ya kuongeza tu uwezo wa miundombinu.

Tatu ni kuziba pengo la ufadhili wa biashara na kuboresha upatikanaji wa mtaji kwa biashara ndogo na za kati pamoja na kampuni za ukubwa wa kati zinazotaka kupanua shughuli zao kuvuka mipaka.

Nne ni kuharakisha ukuaji wa viwanda kwa kuondoka katika utegemezi mkubwa wa kusafirisha malighafi ghafi na badala yake kuongeza uzalishaji wenye thamani zaidi pamoja na kuimarisha minyororo ya ugavi ya kikanda.

Jambo la tano ni kuongeza uratibu kati ya serikali, benki na sekta binafsi ili kuweka sera zinazolingana, kuimarisha imani ya wawekezaji na kuchochea uwekezaji wa muda mrefu.

Kwa Tanzania, mazingira hayo mapya ya biashara yanatoa fursa kubwa ya kuimarisha nafasi ya nchi kama kitovu cha uzalishaji, usafirishaji na usambazaji bidhaa katika ukanda.

Mchanganyiko wa Bandari ya Dar es Salaam, Ukanda wa Kati, upatikanaji wa nchi jirani zisizo na bandari na nafasi ya Tanzania katika mwambao wa Bahari ya Hindi unaipa nchi jukwaa muhimu la kimkakati ambalo linaweza kusaidia biashara kufikia masoko mapana zaidi barani Afrika na kimataifa.

Hata hivyo, Bi. Nellyana alisisitiza kuwa miundombinu pekee haitoshi.

Alisema Afrika inahitaji kuunganisha miundombinu ya kimwili na mifumo yenye ufanisi ya forodha, kanuni zinazotabirika, upatikanaji wa fedha na minyororo imara ya ugavi ya kikanda ili iweze kushindana kikamilifu katika uchumi wa dunia unaobadilika.

Afrika, na hasa Afrika Mashariki, ina fursa kubwa ya kujijenga katika biashara ya kimataifa, si kwa sababu tu ya masoko yake mazuri yaliyopo, bali pia kama kiunganishi na kitovu cha uzalishaji,” alisema.

Alionya kuwa fursa inayotokana na mabadiliko ya mfumo wa biashara duniani haitadumu milele.

Mafanikio hayatakuja yenyewe. Yatategemea kasi ya utekelezaji, upatikanaji wa mtaji na uwezo wa taasisi za benki kuwawezesha kikamilifu wateja katika mnyororo mzima wa thamani wa biashara. Fursa ipo, lakini haitasubiri.”

Akiwa Mdhamini wa Dhahabu (Gold Sponsor) wa GTR East Africa 2026, Absa ilisisitiza tena dhamira yake ya kusaidia biashara, uwekezaji na ukuaji wa uchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Mkutano huo ulilenga kuwa jukwaa muhimu la kujadili uwezo wa biashara kustahimili misukosuko, ufadhili wa minyororo ya ugavi, ufadhili wa miundombinu na fursa mpya zinazotokana na nafasi inayobadilika ya Afrika katika biashara ya kimataifa.
Share:

OTR STAFF RECEIVE TRAINING ON QUALITY MANAGEMENT SYSTEM

By the OTR Reporter, Dar es Salaam │ The Office of the Treasury Registrar (OTR) has stepped up efforts to strengthen its operational systems by equipping staff with knowledge and skills on the Quality Management System (QMS), as part of its drive to align the institution with internationally recognised quality standards.

The training, conducted by Amaxon Company Limited and held on Friday, September 4, 2026, in Dar es Salaam, is part of OTR’s preparations to obtain ISO 9001:2015 certification, an internationally recognised standard for quality management systems.

Opening the training on behalf of the Treasury Registrar, Ms Lightness Mauki, the Director of Performance Management of Commercial entities, said the implementation of QMS would enable OTR to strengthen its work systems, improve efficiency and ensure that its services respond effectively to the needs of stakeholders.

We want to be recognised internationally for delivering quality services, operating efficiently and meeting the expectations of our stakeholders,” Ms Mauki said.

She said achieving this objective would require the participation of all staff, supported by clear procedures that define how work is carried out, monitored and assessed.
The staff training was preceded by a one-week capacity-building programme for QMS Champions drawn from all OTR departments and units.

The programme equipped them with practical skills in applying quality management principles to their day-to-day work, as well as conducting internal audits of work systems.

The QMS Champions are expected to play an important role in promoting and supporting the implementation of the system across different areas of the institution, helping to ensure that its requirements are well understood and consistently applied.
Share:

VODACOM TANZANIA YAPUNGUZA UZALISHAJI WA HEWA CHAFUZI (CARBON EMISSIONS) KWA 24%

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mtandao wa Vodacom Tanzania Plc, Andrew Lupembe (kushoto), na Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Zuweina Farah, wakizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Mazingira, Jamii na Utawala (ESG) ya kampuni hiyo kwa mwaka wa fedha ulioishia Machi 2026. Ripoti hiyo imeonesha kupungua kwa uzalishaji wa hewa chafuzi (carbon emissions) kwa asilimia 24, pamoja na uwekezaji mkubwa katika uboreshaji wa mtandao.
Mkurugenzi wa Miundombinu wa Vodacom Tanzania Plc, Andrew Lupembe, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Mazingira, Jamii na Utawala (ESG) ya kampuni hiyo kwa mwaka 2026.

DAR ES SALAAM | Septemba 3, 2026

VODACOM Tanzania Plc imepunguza uzalishaji wa hewa chafuzi kwa asilimia 24, huku maboresho makubwa ya mtandao yakifikia wateja milioni 27.7, ikiwa ni sehemu ya mafanikio yaliyoainishwa katika Ripoti ya Mazingira, Jamii na Utawala (ESG) ya kampuni kwa mwaka ulioishia Machi 31, 2026.

Vodacom Tanzania ilizindua ripoti hiyo Septemba 1, 2026, ikionesha hatua mbalimbali zilizopigwa katika kupunguza athari za kimazingira, kuboresha ufanisi wa nishati, kupanua huduma za kidijitali na kuimarisha ujumuishwaji wa kifedha nchini.

UZALISHAJI WA HEWA CHAFUZI WAPUNGUA KWA 24%

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, uzalishaji wa hewa chafuzi ulipungua hadi tani 18,445.5, kutoka tani 24,285.6 katika kipindi kilichotangulia.

Wakati huo huo, matumizi ya mafuta ya dizeli yalipungua kwa asilimia 24, kutoka lita milioni 8.6 hadi lita milioni 6.6.
Kupungua huko kulitokana na kubadilisha vifaa vya zamani vya mawasiliano ya redio katika maeneo 1,808 ndani ya kipindi cha miezi saba, pamoja na kuimarisha upatikanaji wa umeme wa gridi ya taifa.

Hatua hizo zimepunguza muda ambao jenereta hutumika katika vituo vya kampuni na hivyo kupunguza matumizi ya mafuta pamoja na uzalishaji wa hewa chafuzi.

SHILINGI BILIONI 3.5 ZATUMIKA KATIKA UFANISI WA NISHATI

Katika mwaka huo, Vodacom Tanzania iliwekeza Shilingi bilioni 3.5 katika ufanisi wa nishati, na kufikisha uokoaji wa nishati hadi megawati 18,340, zaidi ya mara sita ya megawati 2,861 zilizookolewa mwaka 2025.

Mtandao wa Vodacom Tanzania unatumia takriban GWh 169.5 kwa mwaka katika maeneo zaidi ya 3,800 nchini, ambapo 2,190 kati yake yapo vijijini.
Vituo vya msingi vya mawasiliano vinachukua asilimia 78.9 ya matumizi yote ya nishati ya kampuni.

Katika mwaka huo, maeneo 169 yaliyokuwa nje ya gridi ya taifa yaliunganishwa kwenye gridi, hatua iliyosaidia kupunguza utegemezi wa jenereta.

MATUMIZI YA DIZELI KWENYE KITUO CHA KWALE YAPUNGUA KWA 88%

Katika kituo cha data cha Kwale, uwezo wa umeme wa gridi ya taifa uliongezeka kutoka 11kVA hadi 33kVA, hatua iliyopunguza matumizi ya jenereta kutoka saa 18 kwa siku hadi saa mbili.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mabadiliko hayo yamesababisha kupungua kwa asilimia 88 kwa matumizi ya dizeli katika kituo hicho.

Kwa ujumla, asilimia 57 ya nishati yote iliyotumiwa na Vodacom Tanzania ilitokana na vyanzo vya nishati jadidifu.

Kampuni pia iliendelea kuhakikisha kuwa umeme wote wa gridi iliyonunua unaendana na nishati inayotokana na vyanzo jadidifu, hatua iliyosaidia kufikia uzalishaji sifuri wa hewa chafuzi katika eneo hilo.

Aidha, Vodacom Tanzania imehuisha tena cheti chake cha ISO 50001, kinachohusiana na mifumo ya usimamizi wa nishati.

Uzalishaji wa hewa chafuzi unaotokana na shughuli za biashara za kampuni na mnyororo wake wa thamani pia ulipungua hadi tani 94,944, kutoka tani 100,455.

MABORESHO YA MTANDAO YAWAFIKIA WATEJA MILIONI 27.7

Mbali na mafanikio ya kimazingira, Vodacom Tanzania imeendelea kuwekeza katika upanuzi na uboreshaji wa mtandao wake.

Wigo wa mtandao wa 4G umefikia asilimia 76.3 ya wakazi, huku wateja milioni 27.7 wakiwa kwenye mtandao wa kampuni hiyo baada ya uzinduzi wa huduma ya kwanza ya 5G nchini Tanzania.

Umiliki wa simu janja umefikia asilimia 46.7, huku wateja 325,415 wakipata vifaa kupitia ubia wa mikopo ya rejareja.

Kwa wateja ambao bado hawatumii simu janja, Vodacom Tanzania imeanzisha huduma mpya ya kidijitali inayotumia akili unde, inayowezesha upatikanaji wa intaneti kupitia SMS na simu za sauti.

Huduma hiyo inalenga kusogeza fursa za kidijitali kwa wateja ambao hawana simu janja, hususan katika maeneo ya vijijini.

M-PESA YAHUDUMIA WATEJA MILIONI 14.1

Katika eneo la huduma za kifedha, M-Pesa imeendelea kuwa sehemu muhimu ya juhudi za ujumuishwaji wa kifedha nchini, ikiwa imehudumia wateja milioni 14.1.

Wakati huo huo, M-Koba, jukwaa la kidijitali la vikundi vya akiba ambalo wanachama wake wengi ni wanawake, lilifikia vikundi hai 299,420.

Akiba ya jumla kupitia M-Koba iliongezeka kwa asilimia 81, ikionesha kuendelea kukua kwa matumizi ya huduma za kidijitali katika kuwezesha vikundi vya akiba.

VODACOM FOUNDATION YAWAFIKIA WANUFAIKA MILIONI 2.9

Kupitia Vodacom Tanzania Foundation, kampuni ilifikisha programu mbalimbali kwa wanufaika milioni 2.9.

Kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania, kampuni iliondoa gharama za data kwenye jukwaa la kitaifa la maendeleo ya walimu.

Hatua hiyo iliwawezesha walimu 121,832 kupata nyenzo za maendeleo ya kitaaluma bila gharama ya data.

Katika uhifadhi wa mazingira, miti 80,000 ya asili iliongezwa katika Msitu wa Kahe 2 katika eneo la Mlima Kilimanjaro.

VODACOM YADUMISHA REKODI YA USALAMA KAZINI

Vodacom Tanzania pia imerekodi mwaka wa 14 mfululizo bila kutokea kifo cha mfanyakazi mahali pa kazi.

Mpango wa maboresho ya mtandao ulihusisha wafanyakazi 411, waliosafiri zaidi ya kilomita milioni 1.7.

Awamu ya kwanza ya mpango huo ilikamilika bila kutokea kifo au tukio kubwa.

Kampuni pia ina uthibitisho wa ISO 27001 kwa usalama wa data na haikurekodi faini yoyote inayohusiana na ushindani usio halali au utakatishaji fedha.

MAFANIKIO HAYA YAMETOKANA NA UHANDISI WA MSINGI

Akizungumzia mafanikio hayo, Mkurugenzi wa Miundombinu ya Mtandao wa Vodacom Tanzania, Andrew Lupembe, alisema hatua zilizochukuliwa katika kuboresha miundombinu zimeleta manufaa kwa wateja na mazingira.

Mafanikio haya ya kimazingira yametokana na kufanya uhandisi wa msingi kwa usahihi, siyo kutoka mradi tofauti wa uendelevu.”

Alisema kubadilisha vifaa vya zamani katika maeneo 1,808 kumewapa wateja muunganisho wa haraka zaidi, huku taifa likinufaika na kupunguzwa kwa athari za kimazingira zinazotokana na matumizi ya mafuta.

Kwa mujibu wa Lupembe, hatua hiyo imewezesha kupunguza matumizi ya takriban lita milioni mbili za dizeli. NYUMA YA KILA MUUNGANISHO KUNA MAISHA YANAYOBADILIKA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire, alisema mafanikio hayo yanaonesha namna teknolojia na muunganisho vinavyoweza kuleta mabadiliko katika maisha ya Watanzania.

Nyuma ya kila muunganisho kuna maisha yanayobadilika, mwalimu anayefikia nyenzo za kujifunzia bila gharama ya data, kikundi cha akiba ambacho hakihifadhi tena fedha taslimu katika bati.”

Besiimire alisema Vodacom Tanzania itaendelea kuwajibika kwa wananchi wa Tanzania wanaoiamini kampuni hiyo kila siku.

Kwa ujumla, matokeo yaliyoainishwa katika Ripoti ya ESG ya Vodacom Tanzania ya mwaka 2026 yanaonesha jitihada za kampuni hiyo katika kuunganisha ukuaji wa biashara, upanuzi wa huduma za kidijitali, ujumuishwaji wa kifedha na uendelevu wa mazingira.

Share:

OTR, ANGLOGOLD ASHANTI SEEK STRONGER LONG-TERM PARTNERSHIP

Dar es Salaam. Treasury Registrar Nehemiah Mchechu has held discussions with representatives of AngloGold Ashanti, a leading global mining company, on strengthening the company’s long-term relationship with the government and advancing cooperation in Tanzania.

The discussions took place on Tuesday, September 1, 2026, when a delegation from AngloGold Ashanti, through its Tanzanian subsidiary, Geita Gold Mining Limited (GGML), paid a courtesy visit to the Office of the Treasury Registrar (OTR) to brief Mr Mchechu on the company’s business developments and interests in the country.

The delegation was led by Ms Lizelle Marwick, Chief Legal Officer of AngloGold Ashanti, and included Ambassador Baso Sangqu, Senior Vice President for Sustainability at AngloGold Ashanti, and Mr Simon Shayo, Vice President for Sustainability and Stakeholder Engagement at Geita Gold Mining Limited (GGML).
Mr Mchechu said OTR, as the government’s shareholder representative, approaches its relationship with companies from the perspective of being a fellow shareholder rather than an opposing party.

Whatever keeps you away also keeps us away, and whatever brings results brings results for both of us,” he said, underscoring the importance of working together to achieve sustainable business outcomes.

He said OTR works closely with relevant authorities, with the institutions reading from the same page on key issues to ensure consistency and stability for investors.

Mr Mchechu said OTR was committed to building a long-term relationship with AngloGold Ashanti based on mutual understanding, effective corporate governance and a shared interest in ensuring the success of the business.
He also stressed the importance of strengthening corporate governance and ensuring that boards have capable members with a strong understanding of business, enterprise and strategic direction, particularly in companies that contribute taxes and dividends to the Government.

For her part, Ms Marwick said AngloGold Ashanti values its relationships with host governments and appreciates its long-standing engagement with the Tanzanian Government.

She said the company was committed to building a genuine partnership in which both sides contribute their strengths and perspectives for mutual benefit and the wider interests of the country.

Ms Marwick said AngloGold Ashanti was ready to support capacity building for government-appointed directors through governance and induction programmes covering fiduciary responsibilities, board processes and financial literacy.
She also proposed technical exposure visits to Geita Gold Mine to help government directors better understand mining operations, including the technical aspects of resources and reserves.

Ms Marwick described Geita Gold Mine as a flagship asset and said AngloGold Ashanti had remained committed to Tanzania despite legislative changes and challenges associated with COVID-19.

She said the company’s relationship with the government would provide an important stepping stone for its other exploration titles in Tanzania, noting that AngloGold Ashanti could expand more easily where it already had operations, infrastructure and a strong working relationship with the Government.
Share:

DKT. YONAZI AWAKUMBUSHA VIJANA KULINDA AFYA ZAO KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

Na. Mwandishi Wetu - Kazuramimba Kigoma

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi, Amewaasa vijana kulinda afya zao na kuepuka tabia hatarishi ili kupunguza maambukizi mapya ya VVU, kwa kuzingatia kuwa ni kundi linaloongoza kuwa hatarini zaidi nchini Tanzania.

Dkt. Yonazi ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Afua za UKIMWI Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma alipoambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Dkt. Adam Mrisho, timu ya wataalam kutoka Ofisi yake, Wizara ya Afya, TAMISEMI na Ofisi ya Mkoa huo.

Aidha amepata wasaa kutembelea Kituo cha Maarifa Kata ya Kazuramimba mkoani humo kinachotoa huduma za masuala ya VVU na UKIMWI, na kukutana na vijana wanaotekeleza afua za UKIMWI kupitia vikundi vya uzalishaji mali kwa lengo la kujiinua kiuchumi na kujiletea maendeleo yao.

Akiwa katika kituo hicho, Dkt. Yonazi amepokea taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kikundi, Billy Sekibaha, kuhusu shughuli zinazofanywa na kikundi hicho ikiwemo za biashara ndogondogo za kuuza dagaa pamoja na shunguli za ushonaji wa nguo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kuondokana na dhana ya utegemezi.

Amesisitiza kuwa, kundi la vijana linategemewa na Taifa katika shughuli za uzalishaji mali na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla hivyo ni vyema vijana wakaendelea kujilinda na kulinda wengine kwa kutambua hali zao na endapo wakagundulika kuwa na maambukizi ya VVU inashauriwa kuanza kutumia dawa mapema.

"Mnafanya kazi nzuri sana, endeleeni kuchangamkia uwepo wa mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa zenu ili kuwafikia wateja wengi zaidi na kujitangaza kitaifa na kimataifa," alisisitiza Dkt. Yonazi

Kwa upande wake Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Adam Mrisho amewapongeza vijana hao kwa kazi nzuri wanazofanya na kusisitiza kuwa Tume itaendelea kuwawezesha vijana kiuchumi na kuwajengea uwezo ili kuendeleza mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU na kufikia lengo la kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030.
Share:

ABSA TANZANIA YAONGEZA JUHUDI ZA KUWAWEZESHA WASICHANA KATIKA TEKNOLOJIA KUPITIA GIRLCODE HACKATHON

Zandile Mkwanazi

Benki ya Absa Tanzania, kwa kushirikiana na GirlCode, shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake nchini Afrika Kusini linalolenga kuwawezesha wasichana kutoka mazingira yenye changamoto kwa kuwapatia ujuzi na rasilimali za kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika sekta ya teknolojia, imetangaza kurejea kwa mashindano ya GirlCode Tanzania Hackathon kwa mwaka wa pili mfululizo.

Hatua hiyo inafuatia mafanikio makubwa yaliyopatikana mwaka 2025, ambapo timu ya Tanzania iliibuka na tuzo kuu ya Pan-African Grand Prize yenye thamani ya Dola za Marekani 5,000.

GirlCode Hackathon ni sehemu ya mpango mpana wa GirlCode unaolenga kuwawezesha wanawake vijana barani Afrika kwa kuwapatia ujuzi wa vitendo katika teknolojia, kuwaunganisha na walezi na wataalamu kupitia programu za ushauri, pamoja na kuwapa fursa ya kubuni suluhisho zinazolenga kukabiliana na changamoto halisi katika jamii zao.

Kurudi kwa mashindano hayo nchini Tanzania kunatajwa kuwa hatua muhimu katika kuimarisha kizazi cha wataalamu wanawake katika teknolojia na kujenga juu ya mafanikio yaliyopatikana na washiriki wa Tanzania mwaka jana.

Ushindi wa Tanzania mwaka 2025 ulidhihirisha umuhimu wa kuwekeza kwa wanawake vijana kama wabunifu, wajenzi wa suluhisho na watatuzi wa changamoto. Mafanikio hayo hayakuweka tu Tanzania katika ramani ya GirlCode Hackathon barani Afrika, bali pia yalitoa hamasa kwa wanawake vijana zaidi nchini kujiona kuwa sehemu ya uchumi wa kidijitali unaokua barani Afrika.

Akizungumzia kurejea kwa mpango huo nchini Tanzania, Ofisa Mtendaji Mkuu wa GirlCode, Zandile Mkwanazi, alisema shirika hilo linajivunia mafanikio yaliyopatikana na timu ya Tanzania mwaka jana.

GirlCode inajivunia sana kile ambacho timu ya Tanzania ilifanikiwa kukipata mwaka jana. Kushinda tuzo kuu ya Pan-African Grand Prize kumeonyesha kiwango cha vipaji, ubunifu na uwezo uliopo miongoni mwa wanawake vijana nchini Tanzania,” alisema.

Aliongeza kuwa kurejea kwa mashindano hayo kwa mwaka wa pili kunalenga kujenga juu ya mafanikio yaliyopatikana na kuwapa wanawake vijana zaidi fursa ya kuendeleza ujuzi wao, kufanya kazi kwa pamoja na kubuni suluhisho zinazotumia teknolojia na ambazo zinaweza kuwa na matokeo chanya katika jamii.

Hackathon ya mwaka huu itawakutanisha wanafunzi wa kike, wahitimu, wanaotarajia kuwa watengenezaji wa programu pamoja na wabunifu vijana, ambao watashirikiana katika timu, kupata ushauri kutoka kwa wataalamu na kuwasilisha suluhisho zao mbele ya jopo la majaji.

Washiriki watatakiwa kutumia fikra tunduizi, kutumia ujuzi wao wa kiteknolojia na kubuni mawazo mapya yanayoweza kuchangia katika mustakabali wa ajira, ujasiriamali na mageuzi ya kidijitali.

Mbali na mashindano, mpango huo utatoa jukwaa muhimu kwa wanawake vijana kupata uzoefu na uelewa zaidi kuhusu sekta ya teknolojia, kuunganishwa na wenzao pamoja na washauri, na kujenga kujiamini katika kutafuta ajira na fursa mbalimbali katika sekta hiyo.

Kwa washiriki wengi, uzoefu huo unaweza kuwa hatua ya kuingia katika programu za mafunzo kwa vitendo, ajira, ujasiriamali na kuendelea kujifunza katika teknolojia.
Oscar Mwamfwagasi

Akizungumzia umuhimu wa mpango huo, Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi, alisema ushiriki wa waanzilishi wa biashara ndogo na za kati (SMEs) ni moja ya mambo yanayoongeza thamani katika Hackathon ya mwaka huu.

Kinachofanya Hackathon ya mwaka huu kuwa na thamani zaidi ni ushiriki wa moja kwa moja wa waanzilishi wa biashara ndogo na za kati, ambao wanaleta uzoefu wa vitendo katika biashara pamoja na changamoto halisi zinazokabili biashara kwenye programu hii.”

Alisema ushiriki wao unasaidia kuboresha safari ya kujifunza kwa washiriki, huku ukifungua fursa kwa kampuni changa kuonyesha mawazo yao, kupata mwongozo kutoka kwa wataalamu wa sekta mbalimbali na kujenga mahusiano yanayoweza kusaidia kuharakisha ukuaji wa biashara zao.

Programu kama hii ni muhimu katika kukuza ubunifu, kuwawezesha wajasiriamali na kujenga mfumo jumuishi zaidi wa kidijitali unaosaidia maendeleo endelevu ya Afrika,” alisema Mwamfwagasi.

Kadiri GirlCode Hackathon inavyoendelea kukua katika mataifa mbalimbali ya Afrika, Tanzania imeendelea kuwa mfano wa kile kinachoweza kufikiwa pale wanawake vijana wanapopewa majukwaa, rasilimali na mitandao sahihi ya kuwawezesha.

Ushindi wa Tanzania katika mashindano ya Pan-African mwaka 2025 umeweka msingi imara, huku toleo la mwaka huu likilenga kutoa hamasa kwa kizazi kijacho cha wanawake wa Tanzania wanaotaka kujikita katika teknolojia kufikia mafanikio makubwa zaidi.

GirlCode imewahimiza wanawake vijana nchini Tanzania, wadau, walezi na washiriki wa mfumo wa teknolojia kuunga mkono Hackathon ya mwaka huu na kushirikiana katika kujenga mustakabali wa kidijitali unaojumuisha watu wengi zaidi barani Afrika.

GirlCode Tanzania Hackathon 2026 itafanyika tarehe 26–27 Septemba 2026.

Share:

PROF. KABUDI AWATAKA WANANCHI KUZINGATIA TAHADHARI ZA MAAFA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu–Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Prof. Palamagamba Kabudi, amewataka wananchi kuzingatia tahadhari na maelekezo yanayotolewa na wataalamu na mamlaka husika ili kupunguza madhara yanayotokana na majanga na maafa.

Prof. Kabudi ametoa wito huo tarehe 19 Agosti, 2026 wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Watoa Huduma za Misaada ya Kibinadamu Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Ushiriki wa wananchi ni muhimu katika kuimarisha ustahimilivu wa jamii dhidi ya majanga, huku akiwataka kuendelea kufuata taarifa na maelekezo rasmi kutoka kwa wataalamu na mamlaka zinazohusika na masuala ya maafa.

Katika hatua nyingine, alisema Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema na kujenga ustahimilivu wa jamii ili kuongeza uwezo wa wananchi kukabiliana na majanga na kupunguza madhara yanayotokana na matukio hayo.

Alisema uwezo wa nchi katika kukabiliana na majanga kwa ufanisi unategemea uwepo wa mifumo madhubuti, uratibu na ushirikiano wa karibu na wenye tija kati ya Serikali na wadau wa huduma za kibinadamu.

Prof. Kabudi pia alimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake katika kusimamia masuala ya kibinadamu na ustawi wa wananchi.

Kupitia uongozi wa Rais Dkt. Samia, Serikali imeendelea kuhakikisha wananchi wanaokumbwa na changamoto za majanga wanapata msaada na faraja wakati wa dharura.

Prof. Kabudi aliwataka watoa huduma za kibinadamu kuwekeza zaidi katika kuwawezesha wananchi kwa elimu na taarifa sahihi kuhusu vihatarishi vinavyowazunguka, pamoja na hatua za kuchukua kabla, wakati na baada ya janga.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. James Kilabuko, amesema maadhimisho ya siku hiyo yanatoa fursa ya kutambua na kuthamini mchango wa watoa huduma za kibinadamu ambao hujitolea kwa moyo wa huruma, ujasiri na mshikamano katika kuokoa maisha na kupunguza madhara.

Alisema ni muhimu kuendelea kuimarisha ushirikiano na mshikamano miongoni mwa Serikali, wadau wa huduma za kibinadamu na jamii katika kuhakikisha kuwa msaada unapatikana kwa wakati na unawafikia wale wanaouhitaji.

Ni muhimu kuhakikisha kuwa katika kila hatua ya utoaji wa huduma za kibinadamu, maisha, usalama na utu wa mwanadamu vinaendelea kuwa kiini cha hatua tunazochukua.
Share:

BENKI YA ABSA YAZINDUA “ABSA LIPA SASA” KUKUZA MALIPO YA KIDIJITALI NA UJUMUISHAJI WA HUDUMA ZA KIFEDHA

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa, Bw. Victor Nchimbi (wa tano kushoto), Meneja Masoko, Mawasiliano na Chapa, Bw. Beda Biswalo (wa nne kushoto) na Meneja Bidhaa Kitengo cha Biashara, Bi. Devroda Kagusa (wa tatu kulia), pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, wakizindua mfumo wa malipo wa Absa Lipa Sasa, wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kupitia Absa Lipa Sasa, wateja wanaweza kulipa kutoka benki au mtandao wowote kwa kutumia QR code au lipa namba hivyo kurahisisha malipo kwa kutumia njia za kidigitali.

Benki ya Absa Tanzania imezindua rasmi Absa Lipa Sasa, huduma mpya ya malipo ya kidijitali inayotumia mfumo wa TanQR, ikiwa na lengo la kuwawezesha wafanyabiashara na watumiaji kufanya malipo kwa haraka, usalama na urahisi kupitia mfumo mmoja unaokubalika na benki mbalimbali pamoja na mitandao ya simu nchini.

Huduma hiyo imejengwa kwa kuzingatia kiwango cha kitaifa cha TanQR chini ya usimamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), na inawawezesha wafanyabiashara kupokea malipo kutoka benki mbalimbali na mitandao ya simu kwa kutumia QR Code moja, hivyo kurahisisha miamala na kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Victor Nchimbi, alisema huduma hiyo imeundwa kurahisisha malipo kwa wafanyabiashara na wateja wao.

Kupitia Absa Lipa Sasa, mfanyabiashara anahitaji QR Code moja tu kupokea malipo kutoka kwa wateja wanaotumia benki tofauti au mitandao mbalimbali ya simu. Hii inaondoa ulazima wa kutumia vifaa au mifumo mingi ya malipo, hivyo kupunguza gharama za biashara, kuongeza kasi ya miamala, kuboresha utunzaji wa kumbukumbu na kuimarisha usalama wa malipo. Kwa wateja, huduma hii inaleta uzoefu rahisi, salama na unaotegemewa wa kufanya malipo ya kidijitali,” alisema Nchimbi.

Alieleza kuwa uzinduzi wa huduma hiyo unaunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania za kuongeza ujumuishaji wa huduma za kifedha na kuharakisha matumizi ya teknolojia katika shughuli za kiuchumi kupitia mifumo ya malipo ya kidijitali.

Kwa kutumia uwezo wa mfumo wa TanQR, Absa Lipa Sasa inawawezesha wafanyabiashara kupokea malipo yote kupitia mfumo mmoja bila kuwa na ulazima wa kutumia mifumo au vifaa tofauti vya malipo.

Akizungumza zaidi kuhusu faida za huduma hiyo Nchimbi alisema QR Code hiyo moja inakubali malipo kutoka benki mbalimbali na mitandao ya simu huku uthibitisho wa miamala ukipatikana papo hapo.

Aliongeza kuwa mfumo huo unapunguza utegemezi wa fedha taslimu, kuongeza uwazi katika miamala ya malipo na kupunguza gharama za kupokea malipo, hususan kwa biashara ndogo, za kati na za kati zinazokua (MSMEs).

"Huduma hiyo inalenga kuwahudumia wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa, pamoja na wafanyabiashara wa sekta isiyo rasmi wanaohitaji njia salama, rahisi na yenye ufanisi ya kupokea malipo", aliongeza.

Kwa upande wake, Meneja Masoko, Mawasiliano na Chapa wa Benki ya Absa Tanzania, Beda Biswalo, alisema uzinduzi wa Absa Lipa Sasa unaakisi dhamira ya benki hiyo ya kuwasaidia wateja kufikia malengo yao kupitia suluhisho bunifu za malipo.

Katika Absa tunaamini kuwa ‘Stori Yako Ina Thamani’ kwa sababu kila mteja, mjasiriamali na biashara ina ndoto zinazostahili kuungwa mkono. Absa Lipa Sasa inaonesha dhamira yetu ya kuwasaidia wateja wetu kukua kupitia huduma rahisi, salama na zinazopatikana kirahisi ambazo zinakidhi mahitaji yao ya kila siku. Hivi ndivyo tunavyotekeleza lengo letu la ‘Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja… Hatua Moja Baada ya Nyingine,’ huku tukichochea ujumuishaji wa huduma za kifedha na mageuzi ya kidijitali nchini Tanzania,” alisema Biswalo.

Kupitia Absa Lipa Sasa, wafanyabiashara watapanua wigo wa wateja wao, kupunguza hatari zinazotokana na matumizi ya fedha taslimu, pamoja na kujenga historia ya miamala ya kidijitali ambayo inaweza kusaidia kupata huduma nyingine za kifedha siku zijazo.

Huduma hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa Benki ya Absa Tanzania wa kuendeleza mageuzi ya kidijitali na kuimarisha nafasi yake kama mshirika wa kuaminika wa kifedha na taasisi inayochangia maendeleo chanya ya jamii.

Absa Lipa Sasa imeanza kupatikana kwa wafanyabiashara kote nchini, ambapo usajili unaweza kufanyika katika matawi yote ya Benki ya Absa Tanzania au kupitia wasimamizi wa mahusiano ya wateja wa benki hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa, Bw. Victor Nchimbi (katikati), Meneja Masoko, Mawasiliano na Chapa, Bw. Beda Biswalo (kushoto) na Meneja Bidhaa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Devroda Kagusa wakifanya malipo kwa simu kwa kutumia mfumo wa malipo wa Absa Lipa Sasa, wakati wa uzinduzi wa mfumo huo jijini Dar es Salaam leo. Kupitia Absa Lipa Sasa, wateja wanaweza kulipa kutoka benki au mtandao wowote kwa kutumia QR code au lipa namba hivyo kurahisisha malipo kwa kutumia njia za kidigitali.
Share:

TANZANIA YAZINDUA UWANJA WA KISASA WA KRIKETI, ICC YAIONA TAYARI KWA MASHINDANO YA KIMATAIFA


Mwenyekiti wa Shirikisho la Kimataifa la Kriketi (ICC), Jay Shah (katikati), akiongoza uzinduzi wa Uwanja wa Kisasa wa Chama cha Kriketi Tanzania (TCA Cricket Arena) uliojengwa katika Viwanja vya Michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Uwanja huo utatumika kama kituo cha taifa cha kukuza vipaji na kuandaa timu za taifa za wanaume, wanawake na vijana wenye umri wa chini ya miaka 19. Wengine pichani ni wadau wa mchezo wa kriketi.

DAR ES SALAAM – Shirikisho la Kimataifa la Kriketi (International Cricket Council - ICC) limesema Tanzania ina nafasi ya kuwa miongoni mwa mataifa yatakayoweza kuandaa mashindano makubwa ya kriketi duniani siku zijazo, kufuatia uwekezaji unaoendelea katika miundombinu ya kisasa ya mchezo huo na maendeleo ya vijana.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa uzinduzi wa Uwanja wa Kisasa wa Chama cha Kriketi Tanzania (TCA Cricket Arena), uliojengwa katika viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Uwanja huo utatumika kama kituo cha taifa cha kukuza vipaji na kuandaa timu za taifa za wanaume, wanawake na vijana wenye umri wa chini ya miaka 19.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Mwenyekiti wa ICC, Jay Shah, alisema Tanzania imeonyesha dhamira kubwa ya kuendeleza mchezo wa kriketi kupitia uwekezaji katika miundombinu na programu za maendeleo ya vijana, hatua ambayo imeifanya kuwa miongoni mwa mataifa yanayokua kwa kasi katika mchezo huo barani Afrika.

Alisema iwapo kasi hiyo ya maendeleo itaendelea, Tanzania inaweza kuwa miongoni mwa nchi zitakazopewa fursa ya kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa, ikiwemo Kombe la Dunia la Kriketi, katika miaka ijayo.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Chama cha Kriketi Tanzania (Tanzania Cricket Association - TCA), Hamisi Hassan Abdallah, alisema uwanja huo mpya utaongeza uwezo wa Tanzania kuandaa mashindano ya kimataifa huku ukiwapatia wachezaji mazingira bora ya mazoezi yanayokidhi viwango vya kimataifa.

Alibainisha kuwa kwa muda mrefu TCA ilikuwa na uwanja mmoja pekee, hali iliyokuwa ikizuia juhudi za kuandaa mashindano makubwa kutokana na uhaba wa miundombinu inayokidhi matakwa ya mashirikisho ya kimataifa.

Naye Afisa Mwandamizi wa Michezo kutoka Baraza la Michezo la Taifa (NSC), Apansia Lema, alisema Serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya michezo ili kuibua na kukuza vipaji vya vijana nchini.

Alisema maendeleo ya mchezo wa kriketi yanaendelea kuimarika, huku zaidi ya shule 400 nchini zikishiriki mchezo huo. Aidha, alitaja kufuzu kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 19 kushiriki Kombe la Dunia la Kriketi 2026 kuwa mafanikio makubwa yanayoonyesha mwelekeo mzuri wa maendeleo ya mchezo huo nchini.

Uzinduzi wa TCA Cricket Arena unatarajiwa kuifanya Tanzania kuwa kitovu muhimu cha kriketi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuongeza uwezo wa nchi kuvutia mashindano ya kimataifa, kuendeleza vipaji vya vijana na kukuza utalii wa michezo.


Share:

BENKI YA ABSA NA KNAUF GYPSUM TANZANIA WAUNGANISHA NGUVU KUWEZESHA WASAMBAZAJI KUPATA MITAJI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw Obedi Laiser (kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania, Bw. Christoforos Stamoulakatos, wakisaini Hati za Makubaliano (MoU) yenye lengo la kuanzisha Mpango wa Ufadhili kwa Wasambazaj, hatua inayolenga kuwawezesha wasambazaji wa Knauf kupata mitaji ya biashara kwa urahisi zaidi, kuimarisha mnyororo wa ugavi na kuchochea ukuaji wa sekta ya ujenzi nchini. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja wa Sheria na Mahusiano ya Nje na Serikali wa Knauf, Bi. Flora Erasto na kulia ni Katibu wa Kampuni kutoka Benki ya Absa Tanzania, Bw. Desmond Malyi.

BENKI ya AbsaTanzania na Kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya kuanzisha Mpango wa Ufadhili kwa Wasambazaji (Distributor Financing Programme), hatua inayolenga kuwawezesha wasambazaji wa Knauf kupata mitaji ya biashara kwa urahisi zaidi, kuimarisha mnyororo wa ugavi na kuchochea ukuaji wa sekta ya ujenzi nchini.

Kupitia makubaliano hayo, Benki ya AbsaTanzania itatoa huduma maalum za kifedha kwa wasambazaji watakaokidhi vigezo vya benki, ikiwa ni pamoja na mikopo ya mtaji wa biashara na ufadhili wa ununuzi wa bidhaa. Awamu ya kwanza ya mpango huo inatarajiwa kuwahusisha wasambazaji kati ya 30 na 40 kutoka mtandao wa Knauf nchini Tanzania.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika katika makao makuu ya Knauf Gypsum Tanzania jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki AbsaTanzania, Bw. Obedi Laiser alisema, ushirikiano huo unaakisi dhamira ya benki hiyo ya kutumia huduma za kifedha kuimarisha biashara na kuongeza thamani katika mnyororo mzima wa biashara.

"Ushirikiano huu unaonesha nguvu ya mfumo shirikishi wa huduma za kibenki katika kusaidia ukuaji wa biashara na kuleta manufaa kwa wadau wote. Kwa kuwapatia wasambazaji wa Knauf suluhisho za kifedha, tunawawezesha kuongeza uwezo wao wa biashara, kuboresha ufanisi na kutumia kikamilifu fursa za ukuaji. Absa tunaendelea kutekeleza dhamira yetu ya kuiwezesha Afrika ya kesho, pamoja, hatua moja baada ya nyingine," alisema Bw. Laiser.

Alisema mpango huo utawapa wasambazaji uwezo wa kupata mitaji ya kuendesha biashara, kuongeza akiba ya bidhaa na kupanua shughuli zao, jambo litakaloimarisha upatikanaji wa bidhaa za Knauf katika soko la Tanzania.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Knauf Gypsum Tanzania, Bw. Christoforos Stamoulakatos, alisema ushirikiano huo utawajengea uwezo wasambazaji wa kampuni hiyo na kuongeza ufanisi wa huduma kwa wateja.

"Wasambazaji wetu ni sehemu muhimu ya mafanikio ya kampuni yetu na uwezo wetu wa kuwahudumia wateja kote nchini. Kupitia ushirikiano huu na Absa Bank Tanzania, tunawapa fursa ya kupata huduma za kifedha zitakazowasaidia kukuza biashara zao na kukidhi mahitaji yanayoendelea kuongezeka sokoni," alisema.

Mpango huo unaendana na mkakati wa Benki ya Absa Tanzania wa mfumo shirikishi wa huduma za kibenki unaolenga kutoa huduma jumuishi za kifedha zinazosaidia mnyororo mzima wa thamani kwa kuwaunganisha wazalishaji, wasambazaji na wadau wengine wa biashara kupitia suluhisho bunifu za kifedha.

Knauf Gypsum Tanzania ni mmoja wa wateja wakubwa wa Benki ya Absa Tanzania katika kitengo cha Wateja wa Makampuni (CIB), na kampuni hiyo imeendelea kuwa mdau muhimu katika sekta ya ujenzi nchini. Kupitia mpango huo mpya, taasisi hizo zinatarajia kuimarisha zaidi ushirikiano wao na kufungua fursa mpya za ukuaji wa biashara kwa wadau wote.

Hafla ya utiaji saini ilihudhuriwa na viongozi wakuu wa Benki ya Absa Tanzania na Knauf Gypsum Tanzania, wasambazaji, washirika wa biashara pamoja na wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya habari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw Obedi Laiser (kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania, Bw. Christoforos Stamoulakatos, wakibadilishana Hati za Makubaliano (MoU), katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo, yenye lengo la kuanzisha Mpango wa Ufadhili kwa Wasambazaji, hatua inayolenga kuwawezesha wasambazaji wa Knauf kupata mitaji ya biashara kwa urahisi zaidi, kuimarisha mnyororo wa ugavi na kuchochea ukuaji wa sekta ya ujenzi nchini. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja wa Sheria na Mahusiano ya Nje na Serikali wa Knauf, Bi. Flora Erasto na kulia ni Katibu wa Kampuni kutoka Benki ya Absa Tanzania, Bw. Desmond Malyi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw Obedi Laiser, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania, Bw. Christoforos Stamoulakatos, wakipiga picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi kutoka pande zote mbili katika hafla ya utiaji saini hati za makubaliano (MoU), yenye lengo la kuanzisha Mpango wa Ufadhili kwa Wasambazaji, hatua inayolenga kuwawezesha wasambazaji wa Knauf kupata mitaji ya biashara kwa urahisi zaidi, kuimarisha mnyororo wa ugavi na kuchochea ukuaji wa sekta ya ujenzi nchini. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw Obedi Laiser (kulia), akimsikiliza moja wa wateja wa Kampuni ya Knauf ambaye ni Mkurugenzi wa Kichomo General Traders, Bw. Hamad Msellem Hassan (wa pili kushoto), mara baada ya utiaji saini hati za makubaliano (MoU), na Knauf yenye lengo la kuanzisha Mpango wa Ufadhili kwa Wasambazaji, hatua inayolenga kuwawezesha wasambazaji wa Knauf kupata mitaji ya biashara kwa urahisi zaidi, kuimarisha mnyororo wa ugavi na kuchochea ukuaji wa sekta ya ujenzi nchini. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Share:

BENKI ZA ABSA NA TCB KUIMARISHA MAHUSIANO YA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB, Bw. Adam Mihayo, mara baada ya Bw. Laiser pamoja na ujumbe wake kumtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam jana, kwa mazungumzo yenye lengo la kuimarisha mahusiano ya ushirikiano wa kimkakati kati ya taasisi hizo mbili katika kuangalia fursa za kibiashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB, Bw. Adam Mihayo, mara baada ya Bw. Laiser pamoja na ujumbe wake kumtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, kwa mazungumzo yenye lengo la kuimarisha mahusiano ya ushirikiano wa kimkakati kati ya taasisi hizo mbili katika kuangalia fursa za kibiashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa pili kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB, Bw. Adam Mihayo (kushoto), pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo, mara baada ya Bw. Laiser pamoja na ujumbe wake kumtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, kwa mazungumzo yenye lengo la kuimarisha mahusiano ya ushirikiano wa kimkakati kati ya taasisi hizo mbili katika kuangalia fursa za kibiashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa nne kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB, Bw. Adam Mihayo (wa tano kushoto), pamoja na baadhi ya maofisa kutoka benki zote mbili, wakipiga picha ya kumbukumbu mara baada ya Bw. Laiser pamoja na ujumbe wake kutembelea ofisini za TCB, jijini Dar es Salaam jana, kwa mazungumzo yenye lengo la kuimarisha mahusiano ya ushirikiano wa kimkakati kati ya taasisi hizo mbili katika kuangalia fursa za kibiashara.
Share:

BENKI ABSA TANZANIA YAENDELEA KUJIZATITI KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA

Mtendaji Mkuu wa Kitengo Cha Wateja wa Makampuni (CIB), wa Absa Group kutoka Afrika Kusini, Bw. Zaid Moola (wa pili kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wa makampuni (CIB), katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya Absa Tanzania jijini Dar es Salaam leo, kama sehemu ya kudumisha ushikiriano wa kibiashara baina yao. kikao hicho pia kiliwakutanisha wateja hao na watendaji wakuu wa kitengo cha CIB kutoka Absa Group, waliopo nchini kwa ziara ya kikazi.

Katika kuendeleza ushirikiano na kutambua mchango mkubwa wa wateja wake wa Kitengo cha Corporate and Investment Banking (CIB), Benki ya Absa Tanzania leo imeandaa kikao cha kifungua kinywa cha kukutanisha wadau wa biashara jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimetoa fursa kwa viongozi wa benki na wateja kufanya majadiliano ya wazi kuhusu fursa za ukuaji wa biashara, mwenendo wa masoko, pamoja na mustakabali wa sekta ya biashara nchini Tanzania.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, amesema benki hiyo inaendelea kutoa huduma mbalimbali za kifedha zinazolenga kukidhi mahitaji ya wateja wake, hususan makampuni na taasisi zinazofanya biashara kubwa.

Aidha, hafla hiyo ilitumika kuwatambulisha viongozi waandamizi kutoka Kitengo cha Corporate and Investment Banking cha Absa Group, wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wake, Bw. Zaid Moola, ambao walipata nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na wateja wakati wa ziara yao ya kikazi nchini Tanzania.

Ziara ya viongozi hao wa Absa Group inaonesha dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kuimarisha mahusiano na wateja wake pamoja na kutoa suluhisho bunifu za kifedha zitakazosaidia biashara kukua na kustawi.

Hatua hiyo pia inaakisi dira ya Absa ya "Kuwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja... Hadithi Moja Baada ya Nyingine."
Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Makampuni (CIB), wa Absa Group Kutoka Afrika Kusini, Bw. Zaid Moola (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Wateja wa Makampuni wa Kanda ya Afrika, Bw. Sola Adegbesan, wakifurahi katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya Absa jijini Dar es Salaam leo kwa wateja wa makampuni, kama sehemu ya kudumisha ushikiriano wa kibiashara baina yao. kikao hicho pia kiliwakutanisha wateja hao na watendaji hao kutoka absa group, waliopo nchini kwa ziara ya kikazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kulia), akimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance, Bw. Muhammad Shah Newaj, katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake wa makampuni (CIB), jijini Dar es Salaam leo, kama sehemu ya kudumisha ushirikiano wa kibiashara baina yao. Kikao hicho pia kiliwakutanisha wateja hao na watendaji wakuu wa CIB kutoka Absa Group, waliopo nchini kwa ziara ya kikazi. Katikati ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Masoko ya Fedha za Kigeni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Rwegalulira.
Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga akizungumza katika hafla waliyowaandaliwa wateja wa makampuni (CIB), jijini Dar es Salaam leo, kama sehemu ya kudumisha ushikiriano wa kibiashara baina yao. kikao hicho pia kiliwakutanisha wateja hao na watendaji wakuu wa kitengo cha CIB kutoka Absa Group, waliopo nchini kwa ziara ya kikazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa pili kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Masoko ya Fedha za Kigeni wa benki hiyo, Bi. Irene Rwegalulira, wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake wa makampuni (CIB), jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja wa Makampuni wa Absa Tanzania, Bi. Nellyana Mmanyi, Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano, Bw. Aron Luhanga na Mkuu wa Kitengo cha Shughuli za kibenki wa benki hiy, Bw. Alred Urasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Wateja wa Absa Group, Bw. Clive Potter (kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja wa makampuni (CIB), katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya Absa Tanzania jijini Dar es Salaam leo, kama sehemu ya kudumisha ushikiriano wa kibiashara baina yao. Katikati ni Mkurugenzi wa Fedha wa Amref Health Africa, Bw. Damas Nugashe na Mkurugenzi Mtendaji wa Savanna Fibre Tanzania, Bw. Thomas Wenanga.
Mtendaji Mkuu wa Wateja wa Makampuni (CIB) wa Absa Group, Bw. Zaid Moola, baadhi ya watendaji wakuu kutoka Absa Group, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, baadhi ya wafanyakazi na wateja wa CIB, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho jijini Dar es Salaam leo.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (338) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (131) MICHEZO (41) SIASA (3)

Pages