Vodacom Tanzania Foundation yazindua ripoti ya maendeleo ya jamii na mkakati mpya wa kuchochea ukuaji jumuishi

Na Mwandishi wetu

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation, imezindua ripoti yake ya mchango wa maendeleo ya jamii kwa miaka mitatu iliyopita (2014-2017) pamoja na mkakati mpya wa miaka mitatu 2019-2021 unaolenga kuchochea elimu jumuishi, ukuaji wa sekta ya kilimo, kuboresha mazingiza na ujumuishwaji wa watu kwenye mifumo rasmi ya kifedha.

Uzinduzi huu umefanyika katika tukio lililopewa jina la "Alama za upendo wa Vodacom" na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Afya), Mhe. Josephat Kandege, maafisa kutoka washirika wa maendeleo na wadau wa kitaifa na kimataifa jijini Dar es Salaam.

Taasisi ya Vodacom Foundation imewekeza zaidi ya TZS bilioni 11 katika miradi ya jamii ambayo imeinua na kuboresha maisha ya watu takribani milioni 3 nchini, kupitia miradi mbalimbali hususani afya ya uzazi, elimu na huduma jumuishi za kifedha.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mheshimiwa Kandege alipongeza jitihada za Vodacom Tanzania Foundation katika kusaidia jamii na kusisitiza ushirikiano kati ya wadau mbalimbali. "Nawapongeza sana Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha maisha ya Watanzania na hasa katika sekta ya afya ya uzazi, elimu na uwezeshaji wa kiuchumi. Kuendeleza Tanzania ni jukumu letu sote hivyo basi ni muhimu sana tuungane pamoja kutimiza azma hii ya taifa letu. Natumai kwamba ripoti hii itatuhamasisha sote kuchangia Nguvu katika kuboresha maisha ya watanzania" aliongeza Mheshimiwa Kandege.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Bw. Hisham Hendi akizungumza juu ya mkakati huo mpya wa Taasisi hiyo alisema, "Mkakati wetu wa 2019-2021 umezingatia mipango ya maendeleo ya nchi (Tanzania) na malengo endelevu ya maendeleo (SDGs) huku tukilenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha, ubora wa elimu na kuchochea mabadiliko katika sekta ya kilimo. Kama mtandao wa simu unaoongoza nchini, tuna nafasi ya pekee kuchangia maendeleo ya jamii na ya kiuchumi nchini kwa kupitia matumizi ya teknolojia ya simu."

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kampuni za simu zina fursa kubwa na wajibu wa kutumia teknolojia na uvumbuzi wa kidijitali kukuza uchumi wa nchi kwa kuongeza ufanisi wa watu. Kampuni ya Vodacom imekuwa ikifanya hivyo tangu mwaka 2000.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, Bi. Rosalynn Mworia, alisisitiza mashirika kuwekeza katika miradi inayolenga kutatua changamoto mbalimbali za kijamii. "Tumeshirikisha wadau mbalimbali katika uzinduzi wa ripoti hii ili kuwahamasisha kuwekeza katika miradi ya kuboresha jamii na kuchochea ushirikiano zaidi baina yetu na wao ili kufikia lengo la kuwa taifa lenye maendeleo jumuishi.” aliongeza Rosalynn.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006, Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imekuwa ikishirikiana na taasisi mbalimbali, imechangia vilivyo katika kuboresha maisha ya Watanzania kupunguza umasikini, kuboresha elimu, kuwezesha Wanawake na Wasichana, pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Afya Mh. Josephat Kandege, (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Hashim Hende, wakati wa Uzinduzi wa ripoti ya Maendeleo ya jamiI na mkakati mpya wa kuchochea ukuaji jumuishi uliopewa jina la Alama za upendo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi TCRA, Dk John Killimbe.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Afya Mh. Josephat kandege (watatu kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Hashim Hende (kulia), wakati wa Uzinduzi wa ripoti ya Maendeleo ya jamiI na mkakati mpya wa kuchochea ukuaji jumuishi uliopewa jina la Alama za upendo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wengine (kushoto), ni Mwenyekiti wa Bodi TCRA, Dk John Killimbe pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Afya Mh. Josephat kandege (watatu kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia wakati akimuonesha picha maalum zilizoandaliwa na Vodacom wakati wa Uzinduzi wa ripoti ya Maendeleo ya jamiI na mkakati mpya wa kuchochea ukuaji jumuishi uliopewa jina la Alama za upendo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Hashim Hende pamoja na Mwenyekiti wa Bodi TCRA, Dk John Killimbe.

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Hashim Hende akipiga picha ya pamoja na wageni waalikwa.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages