Showing posts with label BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts

Wakazi wa Buza Kanisani walalamikia Uchafuzi wa Mazingira wa Sauti

  


Wakazi wa Buza Kanisani, Mtaa wa Amani, wamelamikia mfanyanya biashara kwa kujenga ukumbi wa sherehe katika eneo la makazi (residentional) , jambo linalosabisha uchafuzi mkubwa wa mazingira kwa njia ya sauti kutokana kelele zinatoka katika ukumbi huo.

 

Wanamshutumu mfanyabiashara huyo Bw. Shayo kwa kuvunja sheria za matumizi ya ardhi kwa  ukumbi wa sherehe na bar kubwa  kwenye la eneo ambalo limepimwa na mamlaka za Serikali kwa ajili ya makazi, na sio biashara.

 

"Tunashindwa kulala usiku, watoto wetu wanashindwa kujisomea usiku kwa kelele na ghasia zinasababishwa na ukumbi huu," amesema bw.Mika Moza, mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

 

"Serikali imetumia fedha nyingi za walipa kodi kupima maeneo haya ya makazi, iweje leo mtu anabadilisha matumizi ya ardhi kiholela kwa kufanya biashara kama hii yenye athari kubwa kwa mazingira kwa njia ya sauti/ kelele, alafu serikali ya mtaa iko kimya," amesema mkazi mwingine, Kulwa Muga

 

Wakazi wamedai kuwa wamewasilisha malalamiko yao (kwa maandishi) kwa Afisa mipango miji- Manispaa ya Temeke tangu Mwaka 2013, lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

 

"Mfanyabiashara huyu Bw. Shayo, ni mbabe na kwa sababu ana pesa kiongozi wa serikali ya mtaa, maafisa wa mipango miji -Temeke Manispaa, wote wametiwa mfukoni, hawawezi kuthibiti jambo hili, hali inayosababisha hadha kubwa kwa wakaxi wa eneo hili," Bi. Moza Mrope, amadai mkazi mwingine.

 

Kuthibisha mahusiana wenye mashaka kati mfanyabiashara huyo, wakazi wanasema baada ya kuvunja sheria kwa miaka za ya tisa, hivi karibuni maafisa mipango miji -Temeke manispaa wamemshauri Bw. Shayo, kubadilisha matumizi ya kiwanja hicho No. 686, Kitalu E, kutoka makazi kwenda biashara, jambo ambalo ni "uvunjifu wa sheria za mazingira."

 

"Kumruhudu abadilishe matumizi ya kiwanja -kutoka makazi kwenda biashara, ni kosa kwa sababu maeneo haya yamepimwa kwa ajili makazi, na si biashara...Manispaa wakiruhusu jambo hili watakuwa wamebariki rasmi uchafuzi wa mazingira na uvunjaji wa sheri za mazingira, bila kujali athari za kelele na uchafu huu mkubwa wananchi walio wengi.

 

Alipohojiwa, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amani, Bw. Omary Katoto amesema "Sio wakazi wote wanalalamika kuhusu jambo hili, ninachofahamu mimi ni kwamba kulikuwa ugomvi kati ya mfanyabiashara huyo na mtu mmoja katika eneo hilo."

 

"Miaka kama mitatu iliyopita walipelekana polisi, walitishiana maisha sijui, lakini niitwa kama Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa, nikawasihi polisi watuachie jambo lile tukalisuhishe kirafiki kama wa mtaa mmoja, walikubali ...tulikaa chini tuongea na pande zote mbili, tukamaliza. Leo hii nashangaa kuone jambo hili nimeibuka tena.".

 

Alipotafutwa, Afisa Ardhi-Temeke Manispaa, Salumu Ali, amesema “Njia rahisi kwa wakazi hao ni kupeleka malalamiko yao kwa maandishi kwa Mkurugenzi wa Manispaa, ili kuweka pingamizi la kuzuia mabadiliko ya matumizi ya Ardhi ambayo Bw. Shayo, amepanga kuyafanya—kutoka Makazi kwenda biashara.”

 

“Kama mamlaka, tutapokea maoni na mapingamizi ya wananchi hao, na kuyafanyia kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za maswala ya Ardhi. Hilo ndo naona kama suluhisho kwa wakazi hao wanaolalamika.”

Share:

Tanzia : MSANII SAM WA UKWELI AFARIKI DUNIA


Usiku wa June 6, 2018 Muimbaji Sam wa Ukweli aliyevuma kwa wimbo wa 'Hata kwetu wapo' amefariki dunia baada ya kuzidiwa ghafla akiwa studio, na kupelekwa katika hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam huku Producer wake Steve aliyekuwa akifanya kazi na Msanii huyo na amesema Sam alikuwa akiumwa na walipomuuliza alisema ni UKIMWI wa kulogwa.

Walichoandika Wolper, Snura na Prof.Jay kuhusu kifo caha Sam wa Ukweli 

..>>> “Sam alianza kuzidiwa toka J’mosi, tulipomuuliza anaumwa nini alisema UKIMWI lakini sio UKIMWI wa kawaida bali wa kulogwa” – Steve

Sasa baadhi ya mastaa mbalimbali wameguswa na tukio hilo na kupost kwenye ukura zao za Instagram…>>>“Dah!!!😢😢😢😢nitasema nini sasa mimi 😢😢tangulia tu mdogo wangu harakati ndio zimeishia hapa kweli????😢😢😢😢😢” – SNURA


.…>>>”Poleni Ndugu wafiwa wote na Mashabiki kwa ujumla jamani🙌 R.i.p Sam Tangulia mwaya 🙏” – WOLPER


……>>>Whaaaat? R.I.P SAM WA UKWELI🙏” Prof. Jay

Share:

Mahakama Kuu yamtoa gerezani Lulu

Mcheza Filamu, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu amebadilishiwa kifungo na sasa atatumikia adhabu hiyo akiwa nje yaani ‘kifungo cha nje’.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Akizungumza na DolKidoti Media Jumatatu Mei 14, 2018, Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu  na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.


“Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi. Hii si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, kitaalamu tunaita ‘community service’” amesema Mboje
Share:

Lulu Diva: Siwezi Kupata Mtoto Sasa Hivi Labda Miaka 5au 6 Inayokuja


Mwanadada Lulu Diva amefunguka na kusema kuwa hatokaa kubadilisha msimamao wake wa kupata mtoto sasa hivi kwa sababu hana  mpango wa kupata mtoto kwa sasa kama ambavyo alishasema tangu hapo awali,

Kuna kipindi cha hapo awali kulikuwa na tetesi kuwa Lulu Diva alishapata mtoto huku awali lakini mtoto huyo amemuacha kwa mama yake na kwamba hataki watu wajue kama anamtoto, kitu ambacho Lulu Diva mwenyewe alikanusha na kusema kuwa amekuwa akikaa na watoto wa ndugu zake wengi kwahiyo hana mtoto wala hategemei kupata mtoto kwa sasa.

"Kama mtoto nilishasemaga kuwa siwezi kupata mtoto sasa hivi labda miaka 5 au 6 inayokuja not now, maana sio kitu cha kukimbilia."

Akiongea na waandishi wa habari alipokuwa katika ufunguzi wa car wash ya Perfect Chrispin, Lulu Diva anasema kuwa kwa sasa amejikita kuwekeza zaidi katika kilimo kwa sababu kuna mashambe mengi ya mama yake ambayo ameachiwa na marehemu baba yake kwaio akiwa kama mtoto mkubwa kwenye familia yao ameona ni bora kuyafanyia kazi mashamba hayo.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (275) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (119) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages