TIMU HIZI NDIO BALAA PROPHET SUGUYE CUP


Mshambuliaji  wa timu ya Tumaini FC  Azizi Mussa, akijaribu kuwatoka mabeki wa Fair Play FC, wakati wa mchezo wa  Ligi ya Prophet  Suguye Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo timu ya Tumaini imeibuka na ushindi wa 3-0 Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Wachezaji  wa timu ya Magereza FC na Miyosha FC, wakiwania mpiwa  wa  Miyosha wakati wa mchezo wa Ligi ya Prophet  Suguye Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo timu ya Magereza imeibuka na ushindi wa 4-1.  Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Kiungo wa Tumaini FC Chongoro Jolvin akimtoka beki wa Fair Play FC wakati wa mchezo wa Ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo timu ya Tumaini iliilaza  Home Boys kwa mabao 3-0  Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Winga wa kulia wa Mbondole FC Azam Banda, akijaribu kuwatoka Mabeki wa Kigamboni FC wakati wa mchezo wao katika Ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo timu ya Mbondole ilishinda 4-1  Mchezo huo umepigwa jana viwanjani hapo.
Mshambuliaji  wa timu ya Lord Eyes FC John Gisanta, akijaribu kumtoka beki wa Kivule Forest  FC, wakati wa mchezo wa  Ligi ya Prophet  Suguye Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo timu ya Kivule Forest  imeibuka na ushindi wa 1-0  Mchezo huo umepigwa jana viwanjani hapo.
Mlinda mlango wa Lord Eyes Chriss Julius akikamata mpira wakati wa mchezo wa  Ligi ya Prophet  Suguye Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo timu ya Kivule Forest  imeibuka na ushindi wa 1-0  Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Mshambuliaji wa Kivule Forest, akipiga mpira kwa kichwa ambao ulikwenda mpjakwamoja wavuni nakuiandikia timu hiyo bao la ushindi wakati wa mchezo wa  Ligi ya Prophet  Suguye Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo timu ya Kivule Forest  imeibuka na ushindi wa 1-0  Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Share:

Vodacom Tanzania Foundation yazindua ripoti ya maendeleo ya jamii na mkakati mpya wa kuchochea ukuaji jumuishi

Na Mwandishi wetu

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation, imezindua ripoti yake ya mchango wa maendeleo ya jamii kwa miaka mitatu iliyopita (2014-2017) pamoja na mkakati mpya wa miaka mitatu 2019-2021 unaolenga kuchochea elimu jumuishi, ukuaji wa sekta ya kilimo, kuboresha mazingiza na ujumuishwaji wa watu kwenye mifumo rasmi ya kifedha.

Uzinduzi huu umefanyika katika tukio lililopewa jina la "Alama za upendo wa Vodacom" na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Afya), Mhe. Josephat Kandege, maafisa kutoka washirika wa maendeleo na wadau wa kitaifa na kimataifa jijini Dar es Salaam.

Taasisi ya Vodacom Foundation imewekeza zaidi ya TZS bilioni 11 katika miradi ya jamii ambayo imeinua na kuboresha maisha ya watu takribani milioni 3 nchini, kupitia miradi mbalimbali hususani afya ya uzazi, elimu na huduma jumuishi za kifedha.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mheshimiwa Kandege alipongeza jitihada za Vodacom Tanzania Foundation katika kusaidia jamii na kusisitiza ushirikiano kati ya wadau mbalimbali. "Nawapongeza sana Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha maisha ya Watanzania na hasa katika sekta ya afya ya uzazi, elimu na uwezeshaji wa kiuchumi. Kuendeleza Tanzania ni jukumu letu sote hivyo basi ni muhimu sana tuungane pamoja kutimiza azma hii ya taifa letu. Natumai kwamba ripoti hii itatuhamasisha sote kuchangia Nguvu katika kuboresha maisha ya watanzania" aliongeza Mheshimiwa Kandege.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Bw. Hisham Hendi akizungumza juu ya mkakati huo mpya wa Taasisi hiyo alisema, "Mkakati wetu wa 2019-2021 umezingatia mipango ya maendeleo ya nchi (Tanzania) na malengo endelevu ya maendeleo (SDGs) huku tukilenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha, ubora wa elimu na kuchochea mabadiliko katika sekta ya kilimo. Kama mtandao wa simu unaoongoza nchini, tuna nafasi ya pekee kuchangia maendeleo ya jamii na ya kiuchumi nchini kwa kupitia matumizi ya teknolojia ya simu."

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kampuni za simu zina fursa kubwa na wajibu wa kutumia teknolojia na uvumbuzi wa kidijitali kukuza uchumi wa nchi kwa kuongeza ufanisi wa watu. Kampuni ya Vodacom imekuwa ikifanya hivyo tangu mwaka 2000.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, Bi. Rosalynn Mworia, alisisitiza mashirika kuwekeza katika miradi inayolenga kutatua changamoto mbalimbali za kijamii. "Tumeshirikisha wadau mbalimbali katika uzinduzi wa ripoti hii ili kuwahamasisha kuwekeza katika miradi ya kuboresha jamii na kuchochea ushirikiano zaidi baina yetu na wao ili kufikia lengo la kuwa taifa lenye maendeleo jumuishi.” aliongeza Rosalynn.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006, Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imekuwa ikishirikiana na taasisi mbalimbali, imechangia vilivyo katika kuboresha maisha ya Watanzania kupunguza umasikini, kuboresha elimu, kuwezesha Wanawake na Wasichana, pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Afya Mh. Josephat Kandege, (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Hashim Hende, wakati wa Uzinduzi wa ripoti ya Maendeleo ya jamiI na mkakati mpya wa kuchochea ukuaji jumuishi uliopewa jina la Alama za upendo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi TCRA, Dk John Killimbe.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Afya Mh. Josephat kandege (watatu kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Hashim Hende (kulia), wakati wa Uzinduzi wa ripoti ya Maendeleo ya jamiI na mkakati mpya wa kuchochea ukuaji jumuishi uliopewa jina la Alama za upendo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wengine (kushoto), ni Mwenyekiti wa Bodi TCRA, Dk John Killimbe pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Afya Mh. Josephat kandege (watatu kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia wakati akimuonesha picha maalum zilizoandaliwa na Vodacom wakati wa Uzinduzi wa ripoti ya Maendeleo ya jamiI na mkakati mpya wa kuchochea ukuaji jumuishi uliopewa jina la Alama za upendo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Hashim Hende pamoja na Mwenyekiti wa Bodi TCRA, Dk John Killimbe.

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Hashim Hende akipiga picha ya pamoja na wageni waalikwa.
Share:

Unilever yakamilisha kampeni ya Toa Mkono wa Ukaribu kwa kusaidia yatima na wazee wasiojiweza

Meneja Bidhaa ya Omo ya Kampuni ya Unilever, Upendo Mkusa (kushoto) akimkabidhi  msaada wa sabuni, Sukari na Nguo kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto yatima cha Children`s Home Msimbazi, Sista Etienne katika kuhitimisha Kampeni ya Kampuni hiyo ya Toa  Mkono wa Ukarimu iliyofanyika Kipindi cha mwezi wa Ramadhani uliomalizika hivi karibuni. . Makabidhiano hayo yalifanyika kituoni hapo jijini Dar es Salaam  mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Bidhaa ya Omo wa Kampuni ya Unilever, Upendo Mkusa (katikati) akimkabidhi  msaada wa sabuni, sukari na nguo Ofisa Mfawidhi wa Makazi ya wazee wasiojiweza ya Nunge, Jacklina Kanyamwenge katika kuhitimisha kampeni ya kampuni hiyo ya ‘Toa  Mkono wa Ukarimu’ iliyofanyika kipindi cha Mwezi wa Ramadhani. Makabidhiano hayo yalifanyika kituoni Nunge, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam  mwishoni mwa wiki.  Wanaoshuhudia ni  Christabella Msangi na Nurdin Ally walioambata na meneja huyo.
Mmoja wa wazee wanaoishi katika Makazi ya wazee wasiojiweza ya Nunge, Vumilia Chambusho (kulia), akipokea msaada wa baadhi ya vyakula, nguo na sabuni kutoka kwa Meneja Bidhaa ya Omo wa Kampuni ya Unilever, Upendo Mkusa (watatu kushoto) vilivyotolewa na Unilever  katika kuhitimisha kampeni ya kampuni hiyo ya ‘Toa  Mkono wa Ukarimu’ iliyofanyika kipindi cha Mwezi wa Ramadhani. Makabidhiano hayo yalifanyika kituoni hapo, Nunge,  Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni  Christabella Msangi na Nurdin Ally walioambata na meneja huyo.
Meneja wa Bidhaa ya Omo wa Kampuni ya Unilever, Upendo Mkusa (kushoto) akisalimiana na baadhi ya wazee wanaoishi katika Makazi ya wazee wasiojiweza ya Nunge baada ya kukabidhi msaada wa sabuni, sukari na nguo vilivyotolewa na Unilever katika kuhitimisha kampeni ya kampuni hiyo ya ‘Toa  Mkono wa Ukarimu’ iliyofanyika kipindi cha Mwezi wa Ramadhani. Makabidhiano hayo yalifanyika kituoni Nunge, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam  mwishoni mwa wiki. 
Share:

TIMU YA JESHI YAINYUKA MIEMBENI 4-2 LIGI YA PROPHET SUGUYE

Mshambuliaji wa timu ya Air Wing FC Maselo Said (kushoto), akimtoka Beki wa Miembeni FC Tumpale Kasebele, wakati wa mchezo wa ligi ya PROPHET SUGUYE CUP inayoendelea katika viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule nje kidogo ya Dar es Salaam ambapo katika mchezo huo Airwing ilishinda mabao 4-2 mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Wachezaji  wa timu hizo wa kiwania mpira wakati wa mchezo wa ligi ya PROPHET SUGUYE CUP inayoendelea katika viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule nje kidogo ya Dar es Salaam ambapo katika mchezo huo Airwing ilishinda mabao 4-2 mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Mshambuliaji wa timu ya Airwing FC Mushta Thabiti (kulia), akijaribu kumtoka mchezaji wa Miembeni FC, wakati wa mchezo wa ligi ya PROPHET SUGUYE CUP inayoendelea katika viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule nje kidogo ya Dar es Salaam, Airwing ilishinda mabao 4-2 mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Mlinda mlango wa Miembeni FC Idris Abdalaah, akijaribu kuokoa moja ya heka heka wakati wa mchezo wa ligi ya PROPHET SUGUYE CUP inayoendelea katika viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule nje kidogo ya Dar es Salaam ambapo katika mchezo huo Airwing ilishinda mabao 4-2 mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Share:

Watanzania washauriwa kuwekeza katika masoko ya fedha

Mkurugenzi wa Idara ya Hazina na Masoko ya Fedha wa Benki ya NBC, Peter Nalitolela (kulia) akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), wakati wa semina kuhusu ujuzi katika sekta ya benki pamoja na masoko ya fedha na mitaji hapa nchini. Semina hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi.
Wakala wa Mauzo ya Masoko ya Fedha na Mitaji wa Benki ya NBC, Emmanuel Gasirabo akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), wakati wa semina kuhusu ujuzi katika sekta ya benki pamoja na Masoko ya fedha na mitaji hapa nchini. Semina hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi.
Mkuu Kitengo cha Mauzo ya Fedha za Kigeni Wateja Wakubwa na Mashirika wa Benki ya NBC, Juliana Mwapachu akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), wakati wa semina kuhusu ujuzi katika sekta ya benki pamoja na masoko ya fedha na mitaji hapa nchini.Semina hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi.
Mkuu wa Uendeshaji Mizania wa Benki ya NBC Henry Lesika,  akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), wakati wa semina kuhusu ujuzi katika sekta ya benki pamoja na masoko ya fedha na mitaji hapa nchini.Semina hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi.
Meneja Mikopo Midogo midogo wa Benki ya NBC, Mtenya Cheya akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), wakati wa semina kuhusu ujuzi katika sekta ya benki pamoja na masoko ya fedha na mitaji hapa nchini. Semina hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi.
Mmoja wa wanafunzi wa UDBS akiulizwa swali katika semina hiyo iliyoandaliwa na NBC ilikiwa na moja ya majukumu ya shughuli za kijamii za benki hiyo.
Mmoja wa wanafunzi wa UDBS akiulizwa swali katika semina hiyo iliyoandaliwa na NBC ilikiwa na moja ya majukumu ya shughuli za kijamii za benki hiyo kwa lengo la kuongeza ufahamu wa wanafunzi hao katika masuala yab sekta za kibenki na masoko ya fedha na mitaji. 



Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA wameshuariwa kuwekeza katika masoko ya fedha ili kunufaika na fursa zinazopatikana katika masoko hayo ambayo hayahitaji mtaji mkubwa wa kuanzia imeelezwa.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Hazina na Masoko wa Benki ya NBC, Peter Nalitolela katika warsha maalumu iliyoandaliwa na NBC kwa wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), iliyofanyika chuoni hapo, Dar es Salaam hivi karibuni.

Alisema lengo kubwa la warsha hiyo ni kunoa uelewa wa wanafunzi hao kuhusu masoko ya fedha, ili wawe na uwezo wa kuchangamkia fursa lukuki zilizopo sokoni hapo punde wanapomaliza masomo yao.

 “Kuna kasumba iliyojengeka miongoni  mwa watu wenye vipato vya wastani kuwa kuwekeza katika  masoko ya  fedha ni ghali na ni eneo la uwekezaji ambalo limeachiwa matajiri, kitu ambacho hakina ukweli wowote ukiangalia hali halisi”, alisema mkurugenzi huyo.

Bwana Nalitolela aliongeza kuwa kiwango cha chini kabisa kinachohitajika  kuwekeza katika soko la fedha ni shilingi sita, fedha ambayo alisema inaweza kupatikana kwa mtu yeyote aliyejiwekea malengo ya dhati ya kutunza fedha kwa ajili ya kuwekeza kwa manufaa yake ya baadaye.

Nalitolela alisema cha kushangaza, watu wengi ambao wanajichukulia kuwa wenye kipato cha chini wana tabia ya kuwekeza kwenye biashara zilizozoeleka kama kununua daladala au kufungua duka la rejareja, miradi ambayo kiuhalisia inahitaji mtaji mkubwa kupindukia ule unaohitajika kuwekeza katika hati fungati, hisa au dhamana.

 “Tunawashauri watanzania wawekeze kwenye makampuni mengi yaliyobinasishwa na ambayo yanafanya vizuri kibiashara, ili washiriki katika kuendesha uchumi wao na vilevile wajizolee sehemu ya faida inayotengenezwa na makampuni hayo,” alisema Nalitolela.

Aidha kuhusu mafunzo hayo Nalitolela alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa NBC kutumia sehemu ya faida yake kusaidia ustawi wa jamii, na yanalenga kuwapatia wanafunzi wanaosomea  fani za  fedha na benki  katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam stadi za masoko ya fedha ili kuwaanda kuyatumia na kufaidika nayo.




“Haja hii ndiyo inaleta msukumo wetu wa kuelemisha wanafunzi ili watambue ni jinsi gani elimu yao  ya darasani inahusiana na hali halisi kwenye masoko ya fedha. Kama mtoaji mkongwe wa huduma za fedha, NBC itaendelea kuhamasisha umma ili kupanua wigo wa matumizi ya masoko ya fedha.”
Share:

Barclays Bank Tanzania under Absa Group Limited announces Visa Credit Card “Live the Card Life” promotional campaign winner

Barclays Bank Tanzania Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi (right), addresses a media conference in Dar es Salaam at the weekend to announce the winner of the bank’s just ended Visa Credit Card ‘Live the Card Life’ campaign. A Dar es Salaam resident, Yusufu Fadhili Mavura, won a fully paid trip to Johannesburg, South Africa together with his chosen partner for A VIP treatment for three days. Looking on from left are, BBT Head of Cards, Deogratius Moshy and the bank’s Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga.

Barclays Bank Tanzania under Absa Group Limited, one of Africa’s largest financial services providers, today announced their Visa Credit Cards “Live the Card Life” promotional campaign winner. The winner will enjoy a full paid trip to Johannesburg, South Africa (SA) and enjoy a VIP treatment for three days.

The campaign was launched in April 2019 and has run for one month. Speaking at the press today the Head of Marketing and Corporate Relations, Mr Aron Luhanga, commented, ‘our lucky winner will travel to Johannesburg, SA with his or her chosen partner, and get to experience a full VIP treatment from sleeping in luxurious hotel, being driven in private limousine to free shopping at famous malls.

We appeal to all other customers to join Barclays Bank under Absa Group and be part of a great bank. Our focus is to bring possibilities to our customers’ lives and positively impact our communities that we serve.

‘This campaign was opened to all our customers who Bank with Barclays and those who wish to open accounts with us. A customer needed to either open an account and acquire a Barclays Credit Card or make five transactions or more using their Barclays Credit card, and get into the draw to stand a chance to win a fully paid trip to Johannesburg, SA for the VIP treatment for three days’, said Mr Oscar Mwamfwagasi, Head of Retail Banking.

He equally said that Customers who switch to Barclays have multiple reasons to do so including but not limited to a wide range of exciting products and exceptional services from our friendly staff.
 
Barclays Credit Card Campaign ended on May, 31, 2019.
Share:

LIGI YA PROPHET SUGUYE WA WRM YAFIKA PAZURI

Beki wa Bodaboda FC, akipiga mpira kwakichwa kuokoa moja ya shambulizi wakati wakichuana na Kitinye FC, katika mchezo wa Ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shuleya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo timu ya Kitinye iliibuka na ushindi wa 2-1. Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Mshambuliaji wa Bodaboda FC akihamisha mpira katika moja ya heka heka wakati wa mchezo wao na Kitinye FC, katika  Ligi ya Prophet  Suguye Cup inayoendelea katika Viwanjabvya Shule ya Msingi Misitu Kivule nje kidogo ya Jiji la DaresSalaam ambapo timu ya Kitinye iliibuka na ushindi wa 2-1. Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Mlinda mlango  wa Kitinye FC, akikamata mpira dhidi ya mchezo wao na Bodaboda FC, wakati wa mchezo wa  Ligi ya Prophet Suguye  Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo timu ya Kitinye iliibuka na ushindi wa 2-1. Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Wachezaji wa timu hizo wakiwania mpira wakati wa mchezo wa  Ligi ya Prophet  Suguye Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la DaresSalaam ambapo timu ya Kitinye iliibuka na ushindi wa 2-1. Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Share:

Benki ya DCB kuendelea kuwawezesha wananchi kiuchumi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa (kulia), akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa kilichotokewa kwa kutambua udhamini wa benki hiyo katika kufanikisha Kongamano la nne la Kitaifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika mjini Dodoma hivi karibuni. Wa pili kulia ni Waziri Ofisi ya Raia, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng'i Issa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kulia) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rahma Ngassa (kulia kwake), wakionyesha cheti muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa kutambua mchango wao katika kufanikisha Kongamano la nne la Kitaifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi  mjini Dodoma hivi karibuni.
Waziri Mkuu, Kassima Majaliwa (alitekaa kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto aliyekaa), wakipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya wawakilishi wa taasisi zilizowezesha kufanyika kwa Kongamano ls nne la Kitaifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Mkoani Dodoma hivi karibuni. 
Share:

Barclays Tanzania opens another forex bureau in a Dar 5 Star Hotel

Barclays Bank Tanzania Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga (right), shakes hands with Hyatt Regency Dar es Salaam Operations Director, Timothy Mlay during the official opening of BBT second forex bureau in Dar es Salaam yesterday. In the picture from left are BBT City Mall Branch Manager, Winford Mwang’onda, bank’s Head of Global Markets, Esther Maruma and  BBT Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi.

By Our Reporter

The drive to heed Bank of Tanzania call for banks to take the initiative and expand forex services has continued to gain momentum, with Barclays Tanzania Bank opening up a forex shop at Dar’s busy CBD to fill the supply deficit created when tens of bureaus lost licenses over failure to follow laws.

Speaking at the launch at Hyatt Regency hotel yesterday, Barclays Tanzania Head of Global Markets, Esther Maruma said; This strategy direction was taken to support cash trading requirements of the public. We have more than six currencies available for trading immediately.”

Ms Maruma, who said the expansion is part of Barclays foreign exchange retail proposition, added that the bank was evaluating other strategic locations, including ports of entry and other regions outside Dar to ensure the network grows even further and deliver forex services closer to consumers.

The bank’s Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi, said as a business strategy, the bank had to review and improve its forex Board Rate pricing, in order to make services affordable across the clientele base trading in cash, online and through the bank’s footprint.

The forex services, which is an extension of our forex portfolio, gives us opportunity to serve clients beyond the regular working hours, he noted.

However, he said the bank will continue to offer the foreign exchange services in accordance with regulations laid down by The Bank of Tanzania.

The bureau, which will be open seven a week covering weekends and holidays, is the second in the Barclays ambitious forex services provision expansion, having opened up the first one in April.
Share:

MECHI ZA LEO JUNI 19, VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI MISITU KIVULE HAPATOSHI


Mshambuliaji  wa timu ya Magereza FC, Samson Mbangula (wapili kushoto), akijaribu kuwatoka mabeki wa  Professional FC, wakati wa mchezo wa Ligi ya Prophet  Suguye Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo timu ya Magereza imeibuka na ushindi wa 2-0.  Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Beki wa Professional FC, akiwania mpira na Mshambuliaji wa Magereza FC, Samson Mbangula, wakati wakichuana katika mchezo wa Ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shuleya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo timu ya Magereza imeibuka na ushindi wa 2-0. Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Mlinda mlango wa Professional FC, Aloyce Ambrosi akijaribu kuokoa shambulizi dhidi ya mchezo wao na Magereza FC, wakati wa mchezo wa Ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo timu ya Magereza imeibuka na ushindi wa 2-0.  Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.            
Mlinda mlango wa Kitunda FC, Athuman Gasa akijaribu kuokoa shambulizi dhidi ya mchezo wao na Tumaini FC, wakati wa mchezo wa Ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam timu hizo zilitoka kwa sale ya 1-1. Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.


Wachezaji wa timu hizo wakiwania mpira wakati wa mchezo wa  Ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la DaresSalaam ambapo timu hizo zilitoka kwa sale ya 1-1

Mshambuliaji wa Kitunda FC, akiambaa na mpira dhidi ya mchezo wao na Tumaini FC, wakati wa mchezo wa  Ligi ya Prophet Suguye  Cup inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam  timu  hizo zilitoka kwa sale ya 1-1. Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Share:

Maonyesho ya ng'ombe bora wa maziwa yafana Dodoma

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (wa tatu kushoto) akitoa tuzo kwa Mshindi wa kwanza wa Fahali bora kutoka Mbozi, Mkoani Iringa, Abraham Mwalutende wakati wa maonesho ya  Ng`ombe Bora wa Maziwa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane jijini Dodoma juzi.Wapili Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa  ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith na Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (kushoto), akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dk. Eligy Shirima alipokwenda kufungua rasmi Maonesho ya Ng`ombe Bora wa Maziwa Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (IRLI), Dk. Jimmy Smith.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia) akizungumza wakati wa maonesho ya Ng`ombe Bora wa Maziwa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane jijini Dodoma juzi. Wengine kutoka kulia ni, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith; Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dk. Eligy Shirima na Msimamizi wa Mradi wa Utafiti wa Vinasaba vya Ng`ombe wa Maziwa kutoka Taasisi ya Kimataifa  ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk.Okeyo Mwai.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (katikati) akitoa tuzo kwa Mshindi wa kwanza wa ng`ombe bora wa maziwa kutoka Meru, Mkoani Arusha, Emmanuel Nanyaro wakati wa maonesho ya Ng`ombe Bora wa Maziwa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane jijini Dodoma juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (kushoto), akihutubia wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Ng’ombe bora wa maziwa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) pamoja na wadau kutoka maeneo mbalimbali katika Viwanja vya NaneNane Mkoani Dodoma juzi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith (kushoto), akihutubia wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Ng’ombe bora wa maziwa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) pamoja na wadau kutoka maeneo mbalimbali katika Viwanja vya NaneNane Mkoani Dodoma juzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dk. Eligy Shirima akizungumza katika hafla hiyo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (katikati) akipongezana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith wakati wa ufunguzi rasmi Maonesho ya Ng`ombe Bora wa Maziwa Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma jana. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages