Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe akiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika Viwanja Vya Karimjee Dar es Salaam.
Mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng’wilabuzu Ndwata Ludigija (katikati) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo kabla ya kuhutubia hotuba yake ya kuwapongeza wahudumu wa afya kwa kazi nzuri wanayoifanya katika jamii.
Baadhi ya watumishi wa Idara ya Afya na wadau wa Afya wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea katika hafla hiyo.
Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Afya na wadau wa Afya wakiendelea kufuatilia kilichokuwa kikiendelea katika hafla hiyo.
Taswira iliyoonekana katika hafla hiyo.
Hafla ikiendelea ya kuwashukuru watumishi wa idara ya Afya kutokana na utendaji kazi wao wa kila siku wa kuhakikisha wanaokoa maisha ya wananchi.
Watumishi wa Idara ya Afya na wadau mbalimbali wa Afya katika Mkoa wa Dar es Salaam jioni hii wamekutana na kupongezana kwa kazi kubwa wanayoendelea nayo katika kuwatumikiwa wananchi katika sekta ya afya.
Katika hafla hiyo imehudhuriwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng’wilabuzu Ndwata Ludigija.
No comments:
Post a Comment