Na Patrick Nduwimana | Washington DC | Waziri wa mambo ya nje wa marekani Mike Pompeo amezisihi Armenia na Azerbaijan kufikia suluhisho la kidiplomasiya kuhusu mzozo kati yao wa kudhibiti jimbo lenye ugomvi la Nagorno Karabakh, ambako ghasia zilizoanza miezi miwili iliopita ziliendelea jana jumanne, licha ya mkataba wa kusitisha mapigano uliofikiwa na pande zote mjini Washington.
Akiwa ziarani nchini India, Pompeo alizungumza kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan pamoja na rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev.
Pompeo amewashinikiza viongozi hao wawili kutekeleza ahadi zao za kusitisha mapambano na kutafuta suluhisho la kidiplomasiya, taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya marekani imesema.
Jumanne, nchi mbili kila mmoja imeishtumu nyingine kushambulia ngome zilizoko nje ya Nagorno Karabakh, baada ya mkataba wa sitisho la mapigano uliopatikana kutokana na juhudi za waziri Pompeo.
No comments:
Post a Comment