Donald Trump amuapisha Amy Coney Barrett kuwa Jaji katika Mahakama Kuu Marekani!


Baraza la seneti la marekani limemuidhinisha jaji Amy Coney Barret kwa kura 52 dhidi ya 48 kuwa jaji kwenye mahakama ya juu ya marekani kuchukua nafasi ilioachwa na marehemu jaji Ruth Bader Ginsburg.

Ma seneta karibu wote wa chama cha republican wamepiga kura kumuidhinisha jaji Barret. Seneta mrepublican wa jimbo la Maine Susan Collins ameungana na ma seneta wa democrats wote kwa kutomuudhinisha jaji Barret.

Jaji Barret ni jaji wa 3 kuteuliwa na rais Donald Trump kwenye mahakama ya juu. Mahakama hiyo sasa itakua na majaji 6 wenye msimamo wa kiconservative na wa tatu wenye msimamo wa kiliberali.

Jaji Barret ameapishwa katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya nchi hiyo White House.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages