
Benki ya Absa Tanzania imeipongeza Black Swan kwa kuibuka mshindi wa jumla wa Absa–MEST Africa Challenge 2025, shindano la ubunifu linalojumuisha nchi mbalimbali barani Afrika na linaloendeshwa kwa ushirikiano na Meltwater Entrepreneurial School of Technology (MEST Africa). Black Swan pia ilikuwa miongoni mwa washindi watatu bora wa Absa Wazo Challenge Tanzania 2025.
Ushindi huo wa ngazi ya bara, uliopatikana kupitia kampuni ya Black Swan iliyosajiliwa nchini Mauritius, ni hatua muhimu kwa teknolojia ya fedha (fintech), ambayo safari yake ilianza kutambulika ndani ya nchi kupitia Wazo Challenge Tanzania ya Absa Bank Tanzania. Mafanikio hayo yanaonesha nafasi ya Absa kama kichocheo cha ubunifu, kutoka uthibitisho wa ndani hadi ukuaji wa kiwango cha bara.
Shindano la Absa–MEST Africa Challenge liliwakutanisha kampuni bunifu zinazojihusisha na teknolojia za kifedha zenye uwezo mkubwa kutoka katika nchi mbalimbali ambako Absa inafanya kazi. Black Swan ilijitofautisha kwa suluhisho lake la upimaji mbadala wa uaminifu wa mikopo linalotumia Akili Bandia (AI), linalolenga kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha kwa watu na biashara ndogo na za kati (SMEs) ambazo hazijahudumiwa vya kutosha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi wa Huduma Jumuishi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Kennedy Komba jijini Dar es Salaam hivi karibuni, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa Wazo Challenge Tanzania, unaolenga kuimarisha ubunifu na ujasiriamali katika sekta ya Teknolojia ya Fedha (FinTech) na biashara changa (startup) nchini Tanzania. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja na Huduma za Kidigitali, Bw. Samuel Mkuyu. (Picha; Maktaba)
Akizungumza kuhusu mafanikio hayo, Sam Mkuyu, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja na Huduma za Kidigitali wa Benki ya Absa Tanzania, Samuel Mkuyu, alisema: “Ushindi wa Black Swan ni uthibitisho madhubuti wa sababu za kuwepo kwa majukwaa kama Wazo Challenge Tanzania. Ubunifu haukui ukiwa peke yake, unahitaji upatikanaji wa utaalamu, matumizi halisi, na taasisi zilizo tayari kushirikiana. Kupitia Wazo Challenge Tanzania, tunaunda kwa makusudi mazingira yanayowezesha fintech kujaribu mawazo, kuimarisha mifumo yao ya kiteknolojia, na kujenga suluhisho zinazoweza kukua, salama, na zinazoendana na mustakabali wa sekta ya benki. Kuona ubunifu uliojikita Tanzania ukishinda katika ngazi ya bara ni matokeo hasa tuliyolenga kuyawezesha.”
Wazo Challenge Tanzania, iliyoanzishwa na Benki ya Absa Tanzania kwa ushirikiano na Hindsight Ventures, ilibuniwa kusaidia teknolojia za kifedha na wabunifu wanaoendeleza suluhisho zinazolingana na kaulimbiu ya “Bank of the Future.” Tangu kuanzishwa kwake, mpango huu umejenga imani miongoni mwa wabunifu wa ndani, ukionesha kuwa kampuni zinzojishughulisha na teknolojia za kifedha za Tanzania zinaweza kushindana na kushinda katika majukwaa makubwa barani Afrika.
Zaidi ya Tanzania, Absa Group inaendelea kuchangia kwa kiwango kikubwa ukuaji wa fintech barani Afrika kupitia mipango kama MEST Africa Challenge, inayounganisha kampuni changa na mitaji, ushirikiano wa kibiashara wa kiwango cha taasisi, pamoja na fursa za kuvuka mipaka ya nchi.

Baadhi ya washiriki wa Wazo Challenge Tanzania 2025, wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya zawadi kwa washindi, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. (Picha; Absa Bank Tanzania)
Akizungumza kuhusu dhamira pana ya Absa na umuhimu wa kusimulia hadithi za ubunifu, Aron Luhanga, Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, alisema:
“Safari ya Black Swan inaakisi kikamilifu ahadi ya chapa yetu isemayo ‘Stori yako ina thamani’. Kutoka katika mfumo wa ubunifu wa Tanzania hadi kutambulika katika ngazi ya bara, hii ni stori ya imani, ushirikiano na uwezekano. Katika Absa, dhamira yetu iko wazi, Kuiwezesha Afrika ya Kesho, pamoja, hatua moja baada ya nyingine. Stori za fintech kama Black Swan zinatuhamasisha kuendelea kuunga mkono ubunifu na kusimama bega kwa bega na wajasiriamali wanaounda mustakabali wa Afrika.”
Absa Bank Tanzania pia imetangaza kuwa maandalizi ya toleo lijalo la Wazo Challenge Tanzania yanaendelea, likitarajiwa kufanyika mwaka 2026, likiwa na msisitizo mkubwa zaidi kwenye suluhisho za teknoljia za kifedha zinazoweza kukua, ujumuishi wa kidijitali, na ushirikiano unaozalisha matokeo chanya ya kiuchumi.
“Tunapoangalia mbele kuelekea Wazo Challenge Tanzania 2026, tunataka wabunifu wajue kuwa kuna taasisi katika soko hili zinazowaamini,” aliongeza Mkuyu. “Ubunifu hustawi pale imani inapokutana na fursa, na Absa imejidhatiti kutoa vyote viwili.”
Kupitia mipango ya ngazi ya nchi na ya Kundi, Absa inaendelea kujiweka kama kinara wa fikra katika uwezeshaji wa fteknolojia za kifedha, ushirikiano wa ubunifu, na ujumuishi wa kifedha, ikihakikisha kuwa mawazo yanayozaliwa Tanzania yanaweza kukua na kuwa suluhisho zinazohudumia Afrika nzima.







No comments:
Post a Comment