AGIZO LA RC KUNENGE JUU YA UTOAJI WA KONTENA ZILIZOKUWA ZIMEKWAMA BANDARINI LATEKELEZWA

Kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge kuitaka taasisi ya TICTS kuhakikisha kontena Sita zenye Vifaa vya Ujenzi wa Stand mpya ya Mbezi Louis zilizokuwa zimekwama Bandarin kutoka ndani ya masaa mawili, hatimae Taasisi hiyo imetekeleza mara moja agizo hilo.

Mapema leo RC Kunenge amefika Stand mpya ya Mbezi Louis kujihakikishia Kama kontena hizo zimefika ambapo amethibitisha kujionea kontena zote sita zimefika na kufanya idadi kontena zilizotoka kufikia 14.


Aidha RC Kunenge amebainisha kuwa kontena zilizofika ndani yake Kuna Vifaa mbalimbali ikiwemo Vioo, Fremu za madirisha, Mabati na kueleza kuwa Vifaa hivyo vimeanza kutumika Mara tu vilipofika.

Hata hivyo RC Kunenge ameendelea kumtaka Mkandarasi kufanya kazi usiku na Mchana ili Stendi hiyo ikamilike kabla ya November 30 Kama alivyoagiza Rais Dkt. John Magufuli wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi.


Itakumbukwa siku ya Jana October 23 RC Kunenge alifanya ziara ya kustukiza kwenye Bandari ya Dar es salaam kufuatilia kinachokwamisha kutoka kwa kontena hizo na kubaini kasoro za kiutendaji na kuamua kutoa maagizo ya kutaka kontena hizo zitoke ndani ya masaa mawili.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages