RC MAKONDA AMTAKA MKANDARASI WA KAMPUNI YA MISTECO KUKABIDHI JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITAL YA MWANANYAMALA KABLA YA DISEMBA 30



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 16 ametembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la Gorofa tano la Mama na Mtoto Hospital ya Rufaa ya Mwananyamala na kumtaka Mkandarasi wa jengo hilo Kutoka Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kuongeza kasi na masaa ya kazi ili akabidhi jengo hilo kabla ya Disemba 30 mwaka huu.


RC Makonda amesema ujenzi wa Jengo hilo ulisimama tangu mwaka 2014 lakini kupitia uongozi thabiti wa Rais Dkt. John Magufuli aliona hilo changamoto hiyo na kuamua kutoa zaidi ya Shilingi Billion 2.1 kwaajili ya kukamilisha ujenzi huo ili kupunguza kero kwa wananchi.

Aidha RC Makonda amesema Jengo hilo litaanza kutumika mwezi January mwakani ambapo ndani yake litakuwa na uwezo wa kuchukuwa Vitanda 100 vya Mama na Mtoto na fedha ya kununua Vifaa tiba ipo tayari.


Pamoja na hayo RC Makonda amesema mbali na ujenzi wa Jengo hilo Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospital ya Wilaya Mabwepande na tayari yupo kwenye hatua za kujenga Kituo cha Afya Kawe na Bunju ambapo miradi yote ikikamilika itasaidia kumaliza Changamoto za Afya Wilaya ya Kinondoni.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages