Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akikabidhi cheti cha shukrani kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benjamin Nkaka (kushoto), kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1, Jumbe Menye.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya (kulia), akizungumza na Meneja Mahusiano Wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Chiku Chambuso (kushoto), pamoja na mwenzake, Lena Mwakisale katika banda la benki hiyo wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Meneja Mahusiano Wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Lena Mwakisale pamoja mwenzake Isdory Maumba (kushoto), alipokutana nao wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akihutubia wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo Benki ya NBC ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benjamin Nkaka (kulia), akishikana mikono na Kaimu Mwenyekiti Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1, Jumbe Menye.
Baadhi ya wanawake waliohudhuria wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
NA Mwandishi Wetu, Dar
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imewataka wafanyabiashara na wajasiriamali wanawake nchini kuondoa hofu ya kutembelea na kuzungumza na wataalamu wa masuala ya fedha na biashara katika matawi ya benki hiyo ili kufahamu huduma zao na jinsi wanavyoweza kupata huduma za kifedha zitakazoweza kuinua biashara na maisha yao.
Akizungumza wakati wa Kongamano la Kwanza la Wafanyabiashara Wanawake wakubwa na wa kati jijini Dar es Salaam jana ambao benki hiyo ililidhamini, Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Benjamin Nkaka, alisema ni vyema kwa wafanyabishara hao wanawake kuzoea kufanya kazi na benki kwani ni njia rahisi na pekee itakayoweza kustawisha biashara zao.
“Kuna hofu imejengeka kwa wengi kuja benki. Hofu hiyo iondoke. Njooni benki muweze kufahamu ni nini tunakitoa katika kusapoti wajasiriamali hasa wanawake,” alisema Nkaka.
Alisema miongoni mwa majukumu ya benki hiyo ni kusaidia katika kukuza uchumi hasa wa wanawake wajasiriamali, na kuongeza:
“Kwa zaidi ya miaka 50 ya huduma za benki hii nchini, tunafahamu kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili wajasiriamali wanawake ni elimu ya mikopo. Sisi tunatoa elimu hiyo pamoja na ushauri kwa wateja wetu wafanyabiashara kadri biashara yao inavyoendelea na kuwaunganisha na mnyororo wa thamani.
“NBC pia huwakutanisha wateja na wadau mbalimbali kama vile Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Wakala wa Usajili wa Leseni za Biashara (BRELA) na taasisi nyingine. Katika harakati zetu za kuwasapoti wanawake, tumeanzisha Vikundi Akaunti ambazo hazina makato yoyote, huku pia tukishirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) kutoa mikopo yenye garantii ya hadi asilimia 80 kuwawezesha wanawake kuingia kwenye kilimo kwa nguvu.”
Mkutano huo ulihudhuriwa na takriban wanawake wajasiriamali na wafanyabiashara 1,000 kutoka mikoa yote ya Tanzania huku mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda.
Wanawake hao walikutanishwa kupitia mwavuli unaofahamika kama ‘Madirisha’ huku wadau mbalimbali wa maendeleo wakipata nafasi ya kuwaonyesha wanawake hao fursa mbalimbali zilizopo nchini katika kuboresha uchumi wao kama vikundi.
Kampuni ya GS1 iliandaa kongamano hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) pamoja na taasisi ya PASS.
No comments:
Post a Comment