PUMA ENERGY, SELCOM NA MASTERCARD WAUNGANA KUHAMASISHA MALIPO YA KIELEKTRONIKI


Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa kampuni ya Selcom Baguma Ambarei (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari akitoa mfano wa kulipia mafuta kwa kutunia Mastercard kwa wamiliki magari wanaotumia vituo vya mafuta ya Puma kwa ushirikiano Makampuni hayo ambapo mteja atarudishiwa asilimia 5 ya fedha kwa kutumia kadi hiyo, kutoka (kulia) ni mfanya kazi wa Puma, Khamis Ali, Mkurugenzi wa Puma, Dominic Dhanah, na Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Sameer Hirj.
Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Sameer Hirj (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya kulipia mafuta kwa kutunia Mastercard kwa wamiliki magari wanaotumia vituo vya mafuta ya Puma kwa ushirikiano Makampuni hayo ambapo mteja atarudishiwa asilimia 5 ya fedha kwa kutumia kadi hiyo (kulia), ni Mkurugenzi Mtendaji wa Puma, Dominic Dhanah.
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma, Dominic Dhanah (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya kulipia mafuta kwa kutunia Mastercard kwa wamiliki magari wanaotumia vituo vya mafuta ya Puma kwa ushirikiano Makampuni hayo ambapo mteja atarudishiwa asilimia 5 ya fedha kwa kutumia kadi hiyo kulia kwa Dominic ni Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Sameer Hirj.

PUMA ENERGY, SELCOM NA MASTERCARD WAUNGANA KUHAMASISHA MALIPO YA KIELEKTRONIKI.

Dar es salaam, Tanzania; Puma Energy, Selcom Paytech LTD na Mastercard kwa wamezindua kampeni ya pamoja iitwayo #BombaWeekend ambayo inaangalia kurejeshea wateja hadi 5% ya pesa watakayotumia watakapojaza mafuta katika vituo vya Puma Energy endapo watalipia kupitia Mastercard QR.

Kampeni hiyo itaendeshwa kwa wiki 11, kila Ijumaa hadi Jumapili kuanzia saa 10 hadi 12 jioni kupitia mtandao wa Puma wenye vituo 52 nchi nzima. Pamoja na dhumuni la kuzawadia watumiaji wa huduma hiyo, Bomba Weekends ina dhamira ya kuchangia katika juhudi za serikali za kurasimisha malipo na kuhamasisha uchumi wa malipo ya kieletroniki ili kufikia malengo ujumuishaji wa kifedha wa nchini Tanzania.

Mchakato mzima wa kurudishia pesa wakati wa Bomba Weekends unaendeshwa kupitia huduma ya zawadi kwa wateja ya Qwikrewards iliyoundwa na Selcom Paytech LTD mahususi kwa watumiaji wa Mastercard QR. Qwikrewards inamuwezesha mtu yeyote kukusanya pointi au kupata pesa taslim kupitia akaunti iliyounganishwa na namba yake ya simu kila afanyapo malipo kutumia Mastercard QR. Watumiaji Qwikrewards wanaweza kukomboa pointi walizokusanya kwa kupiga *150*15* na kuzitumia katika maeneo zaidi ya 30,000 nchini ambapo Mastercard QR inakubalika kama njia ya malipo. Aidha Mastercard QR imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake nchini mwaka 2018 hadi sasa kupelekea kukubalika na watoa huduma mbali mbali zaidi ya 30,000 kuwa na uwezo wa kupokea malipo kutoka mitandao yote 7 ya simu na benki 15 nchini.

Akiongea na wanahabari katika hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Nd. Dominic Dhanah alisema, "Bomba Weekends inahamasisha wateja we kulipia  mafuta katika vituo yetu kutumia njia rahisi, haraka na salama zaidi na kunufaika papo hapo kupitia Qwikrewards kutoka Puma. Ushirikiano huu unadhahiri kwamba Puma ni kiongozi wa katika sekta ya mafuta inapofikia kujiunga na suluhisho bunifu za malipo ambazo hurahisisha malipo kwa wateja wetu na kutuwezesha kutoa huduma bora zaidi katika vitu vyetu."

Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Paytech LTD, Nd. Sameer Hirji, alionyesha matumaini makubwa kuelekea uchumi wa malipo ya kielektroniki akisisitiza kuwa ni lazima taasisi ambazo zinaongoza mchakato huo kuongeza thamani kwa wateja ili kuwapa hamasa zaidi kutumia malipo ya elektroniki."Kupitia Bomba Weekends tukishirikaina Puma Energy pamoja na Mastercard QR tumedhamiria kuwazawadia wateja watakaolipa kielektroniki katika matumizi yao ya kila siku, mafuta yakiwa sehemu kubwa ya matumizi hayo. Tunaamini kwamba tunavyozidi kurahisisha na kuimarisha upatikanaji na upokeaji wa malipo ya kieletroniki ndivyo tutazidi kuwajengea Watanzania imani ya kutoka nyumbani bila pesa taslim. Tukiwa na Qwikreward na maeneo zaidi ya 30,000 ambapo Mastercard QR inakubali kitaifa tunaamini tunaongoza mabadiliko kuelekea malipo ya kielektroniki na malengo ujumuishaji wa kifedha nchini Tanzania.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Biashara wa Mastercard Ukanda wa Afrika Mashariki, Nd. Adam Jones alisema,”Mastercard itaendelea kutoa huduma shirikishi za malipo ambazo zitasaidia kusukuma jamii kuelekea malipo ya kieletroniki. Njia sahihi ya kufikia malengo haya ni kuendelea kuvumbua mifumo thabiti ya kidijitali kwa kushirikiana na mashirika kama Selcom na  Puma Energy. Tuna uhakika kampeni hii itawahakikishia wateja malipo rahisi, salama na ya uhakika katika kila kituo cha Puma, lakini pia kuchangia juhudi ya nchi kuelekea malipo ya kidijitali.”
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages