Mkuu wa Kitengo cha
Fedha Taslim na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati wa Benki ya Taifa
ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize akizungumza na baadhi ya wateja wao wa makampuni
wa jijini Mwanza, walipokutana na kufanya mazungumzo nao wakiwafahamisha huduma
mbalimbali zitolewazo na NBC na pia kupata mrejesho kutoka kwao juu ya huduma
hizo na jinsi wanaweza kuwahudumia vizuri zaidi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya mwezi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo jijini humo hivi
karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha
Fedha Taslim na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati wa Benki ya Taifa
ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto), akiwasikiliza wateja wa benki hiyo
Malesh Mathade (kulia), pamoja na Mitesh Metha, walipokutana na wateja wao wa
makampuni mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma
kwa wateja wa NBC jijini humo hivi karibuni. NBC katika kipindi cha mwezi
wa huduma kwa wateja imefanya mikutano kama hiyo kwa wateja wake sehemu
mbalimbali nchini.
Mkuu wa Kitengo cha
Fedha Taslim na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati wa Benki ya Taifa ya
Biashara (NBC), Jimmy Myalize (katikati),akishikana mikono na Mteja wa NBC
kutoka kampuni ya Marine Services, Erick Hamissi, walipokutana na wateja
wao wa makampuni mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa
huduma kwa wateja wa NBC jijini humo hivi karibuni.. Kulia ni Nelson
Julius naye kutoka Marine Services.
Meneja wa Huduma kwa
Wateja Wakubwa wa Benki ya NBC, Mary Opiyo (wa tatu kushoto), akishikana mikono
na mteja wa benki hiyo, Mkurugenzi wa Bugando Medical Centre, Padre Engelbert
Nyandwi, katika hafla waliyoiandaa kwa wateja wao wa makampuni ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja jijini humo hivi
karibuni. Wengine kutoka kushoto ni maofisa uhusiano wateja wa benki
hiyo, Abdallah Aruga na Fainess Jeremiah.
Mkuu wa Kitengo cha
wafanya biashara wa kati wa Benki ya NBC Moses Minja (kushoto), akishikana
mikono na mteja wa NBC kutoka kampuni ya Marine Services, Erick Hamissi,
walipokutana na wateja wao wa makampuni mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wateja jijini humo
hivi karibuni. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslimu na Miamala
kwa Wateja Wakubwa na wa Kati wa NBC, Jimmy Myalize.
BENKI
ya Taifa ya Biashara (NBC), imeendelea kuongeza na kuimarisha huduma zake za
kibenki kwa njia za kidigitali ili kuwawezesha wafanyabiashara na wateja
wengine kufanya miamala mingi ya kibenki
mahali walipo imeelezwa jijini Mwanza hivi karibuni.
Akizungumza
na wateja wa benki hiyo jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi
wa huduma kwa wateja wa NBC, Meneja
Huduma katika Kitengo cha Wateja
wa Makampuni wa benki hiyo, Mary Opiyo alisema benki hiyo imerahisisha huduma
zake nyingi kwenda kidigitali ili
kuwafanya wateja wao kupata muda zaidi wa kufanya biashara zao kuliko kupata
huduma hizo katika matawi yao.
“Sasa
mteja wetu anaweza kufanya malipo akiwa ofisini kwake kwa njia ya mtandao wa intaneti
akatuma pesa kwa wateja wake ambao pengine ingebidi awapelekee au waje pale,
NBC itaendelea kuboresha na pia imo mbioni kuongeza huduma nyingine bora zaidi hususan
malipo kwa njia ya mtandao ili kutengeneza fursa mbalimbali za kibiashara kwa
wateja wetu”, aliongeza meneja huyo.
Akizungumza
katika hafla hiyo Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslimu na Miamala kwa wateja
Wakubwa na wa Kati wa beni hiyo, Jimmy Myalize alisema mkutano huo una lengo la
kuwashukuru wateja wao kwa biashara
wanayowapa na kuweza kuwaamini wakawa benki
waitumiayo kwa ajili ya mambo yao
ya kifedha.
Alisema
pia katika kukutana kwao wameweza kuwafahamisha bidhaa zao mpya, benki ipo wapi na maendeleo ya benki kwa
ujumla na pia kupata mrejesho kutoka kwao juu ya huduma za NBC na kama kuna
maeneo wangependa yaboreshwe ili kuweza kuwahudumia vizuri zaidi.
“Pia
tunawakutanisha wateja wetu ili kuweza kuongea biashara na kutengeneza fursa za kibiashara kati yao jambo
litakalosaidia wateja wetu kukua kibiashara kwani mteja anapokua na sisi kama
benki tunakua”
Benki
ya NBC huadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja mwezi wa Oktoba kila mwaka kwa
kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kutoa misaada mbalimbali na
kutoa elimu ya kifedha na ujasiriamali kwa makundi tofauti, kutembelea wateja
wao mahali walipo na kufanya mikutano na wateja hao.
No comments:
Post a Comment