Mchezaji
wa timu ya Magole Fc, Abdallah Ally (kushoto) akijaribu kumtoka mchezaji wa
timu ya Stonefire Fc, Abdallah Sultan katika mchezo wa fainali ya Ligi ya
Waitara Mbuzi Cup iliyochezwa katika Uwanja wa Magole kwa Mama Anna Mkapa
jijini Dar es Salaam. Stonefire Fc ilishinda Magole Fc kwenye matuta kwa bao
4-2.
Mchezaji
wa Timu ya Stonefire Fc, Sudy Manyama (kulia) akichuana Vikali na Mchezaji wa timu ya Magole Fc,Msafiri Oscar
katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Waitara Mbuzi Cup iliyochezwa katika Uwanja
wa Magole kwa Mama Anna Mkapa jijini Dar es Salaam.
Diwani
wa Kata ya Kivule,Wilson Molel (kushoto) akizungumza jambo na Vijana wa kata
hiyo jijini Dar es Salaam katika mchezo wa fainali ya ligi ya Waitara Mbuzi
Cup iliyochezwa katika Uwanja wa Magole kwa Mama Anna Mkapa jijini Dar es Salaam
leo.Ligi hiyo inayodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga,M wita Waitara.Wapili
kushoto ni Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Singo Benson,Katibu Mwenezi wa Chadema kata ya Kivule,Bihimba
Nassoro na Mwenyekiti Chadema kata ya Kivule, Kisiri Anthony.
Mwakilishi
wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Singo Benson (wapili kushoto)
akizungumza na wakazi wa kata ya Kivule jijini Dar es Salaam leo katika hafla
ya kukabidhi mbuzi kwa mshindi wa kwanza wa ligi ya Waitara Mbuzi Cup
iliyofanyika katika uwanja wa Magole kwa Mama Anna Mkapa jijini Dar es Salaam.
Diwani
wa Kata ya Kivule,Wilson Molel (wapili kushoto), pamoja na Mwakilishi wa Mbunge
wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Singo Benson wakikabidhi mbuzi kwa Kapteni wa timu ya
Stonefire Fc baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika fainali ya ligi ya
Waitara Mbuzi Cup kwa kuipiga bao 4-2 Timu ya Magole Fc katika Uwanja wa Magole
kwa Mama Anna Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Singo Benson (kulia) akikabidhi mpira
kwa Kapteni wa Timu ya Magole Fc, Isack Mairi baada ya kuibuka mshindi wa pili
katika fainali fainali ya ligi ya Waitara Mbuzi Cup iliyodhaminiwa na Mbunge wa
Jimbo la Ukonga Mwita Waitara.Katikati ni Diwani wa Kata ya Kivule,Wilson Molel.
Mwenyekiti
Chadema kata ya Kivule,Kisiri Anthony akizungumza katika hafla hiyo.
Katibu
Mwenezi wa Chadema kata ya Kivule,Bihimba Nassoro akitoa shukrani za dhati kwa
timu zilizoshiriki katika ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment