Mchezaji wa timu ya Songas Fc, Frank
Skanyika (kushoto) akichuana vikali na Mchezaji wa Timu ya Wafanyabiashara wa
Kivule Fc, Salum Machaku katika mchezo wa fainali ya ligi ya Waitara Mbuzi Cup
iliyochezwa katika uwanja wa Kivule jijini Dar es Salaam. Timu ya
Wafanyabiashara wa Kivule Fc iliwapiga kwa matuta timu ya Songas Fc bao 3-2.
Mchezaji wa timu ya Songas Fc,Jovin
Joseph (kulia) akijaribu kumtoka mchezaji wa timu ya Timu ya Wafanyabiashara wa
Kivule Fc, Mkwaya Hula katika mchezo wa fainali ya ligi ya Waitara Mbuzi Cup
iliyochezwa katika uwanja wa Kivule jijini Dar es Salaam.
Diwani wa kata ya Kivule,Wilson Molel akizungumza na wakazi wa Kivule jijini Dar es Salaam katika fainali ya ligi ya Waitara Mbuzi Cup kati ya Timu ya Wafanyabiashara wa Kivule Fc na Songas Fc iliyochezwa katika uwanja wa Kivule.Ligi hiyo imedhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Mhe.Freeman Mbowe (wapili kulia) akizungumza na Wakazi pamoja na
wafanyabiashara wa Kivule jijini Dar es Salaam leo baada ya kuwasili katika
kata hiyo kwa ajili ya kushuhudia pamoja na kukabidhi zawadi ya Mbuzi kwa
mshindi wa kwanza wa Ligi ya Waitara Mbuzi Cup iliyochezwa katika uwanja wa
Kivule.Huu ni mwendelezo wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara kutimiza
ahadi alizoahidi kwa vijana katika kuisapoti sekta ya michezo jimboni.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (wapili kushoto) akikabidhi mbuzi kwa Kapteni
wa timu ya Wafanyabiashara wa Kivule jijini Dar es Salaam leo baada ya kuibuka
kidedea kuipiga timu ya Songas Fc kwa matuta bao 3-2 katika fainali ya ligi ya
Waitara Mbuzi Cup iliyochezwa katika uwanja wa Kivule. Wapili kulia ni Diwani wa
kata ya Kivule, Wilson Molel.
Mwenyekiti wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe (katikati) akikabidhi mpira
kwa Kapteni wa timu ya Songas Fc baada ya kushika nafasi ya pili katika fainali
ya ligi ya Waitara Mbuzi Cup iliyochezwa katika uwanja wa Kivule jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema) kata ya Kivule, Bihimba Nassoro (kulia) akizungumza na
wachezaji wa mpira wa miguu pamoja na Viongozi wa Chadema baada ya fainali ya
ligi ya Waitara Mbuzi Cup kumalizika kati ya Wafanyabiashara wa Kivule Fc na
Songas Fc ilyochezwa katika Uwanja wa Kivule jijini Dar es Salaam. Wapili
kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema kata ya Kivule, Kisiri Anthony.
Wachezaji pamoja na mashabiki wa Timu
ya Wafanyabiashara wa Kivule Fc wakishangilia baada ya kukabidhiwa mbuzi na
Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la
Ukonga,Mwita Waitara jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment