BENKI YA CBA KUWASIDIA WATANZANIA KUMILIKI NYUMBA

Mkurugenzi Mtendaji wa CBA Benki, Gift Shoko, akizungumza na wateja na wadau wa benki hiyo wakati wa Siku ya Wateja wa benki hiyo, Dar es Salaam wikiendi hii.
Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa Benki ya CBA, Hakim Sheikh (kushoto) akizungumza na baadhi ya wateja wakati wa hafla ya Siku ya Wateja wa benki hiyo.

Shoko (kulia) akizungumza na mmoja wa wateja wa benki hiyo, Ernest Kilumbi, wakati wa hafla ya siku ya wateja wa benki hiyo.
BENKI ya CBA Tanzania, imeelezea dhamira yake ya kuwasaidia Watanzania kumiliki nyumba  kupitia mpango mpya utakaotoa mikopo nafuu kwa wenye kutaka kumiliki nyumba.

Akiongea wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kama sehemu ya kukutana na wateja wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii,  Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki hiyo, Gift Shoko, alisema mpango huo utawaleta pamoja wenye ardhi, wajenzi na mkopeshaji.

“Chini ya mpango huu mpya, tutafanya kazi pamoja na wenye ardhi na wajenzi ili kuendeleza ardhi ambayo haijaendelezwa kwa kujenga nyumba ambazo baada ya kwisha tutawapatia wateja wetu mikopo na kuzinunua,” alisema.

Shoko alisema, takwimu zinazotolewa na Serikali zinaonyesha kuwepo kwa mamia na maelfu ya Watanzania wenye uhitaji wa kumiliki nyumba kila mwaka lakini wengi wao wamekuwa wakishindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kushindwa kumudu gharama za kununua nyumba.

“Tunachokifanya sasa ni kutoa mikopo nafuu ambayo itawawezesha Watanzania wenye ndoto za kumiliki nyumba kuweza kufanya hivyo kwa urahisi. Lengo letu ni kuona tunawawezesha Watanzania wengi zaidi kumiliki nyumba zao,” alisema.

Shoko alisema nyumba ni moja kati ya mahitaji ya msingi ya binadamu na benki ya CBA inajisikia furaha kuwa benki ya kwanza kutoa mikopo ya muda mrefu ya nyumba inayofika hadi miaka 20 na kusisitiza kuwa benki hiyo itaendelea kutoa mikopo mingi zaidi ya nyumba.

“Dhamira yetu kwenye kuchangia uchumi wa Tanzania inaonekana kwenye uwekezaji na upanuzi tunaofanya kwenye huduma zetu zikiwemo za kidijitali. Mwaka 2017, wanahisa wetu waliongeza shilingi 16.72bn/- kwenye mjati wa benki,” alisema.

Alisisitiza kwamba benki hiyo itaendelea kuwekeza nchini, Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla kwa kuwa inalenga kuwa benki kubwa barani Afrika.

Chakula hicho cha jioni ni ratiba ya kawaida ya benki hiyo kukutana na wateja wake kwa ajili ya kubadilishana mawazo ya namna ya kuboresha huduma pamoja na kupata mrejesho kutoka kwa wateja wake.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages