NBC yatoa udhamini wanafunzi vyuo vikuu

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE), Prof. Godliving Mtui (kutoka kushoto), Mkuu wa Chuo cha Uhifadhi Wanyama Pori, Prof. Jaffari Kideghesho, Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emmanuel Mjema na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dr. Imanueli  Mnzava wakisaini mikataba ya ufadhili wa wanafunzi 60 kutoka Benki ya NBC utakaowanufaisha wanafunzi hao katika mwaka wa kwanza wa masomo wa 2018/19 katika hafla iliyofanyika jijini  Dar es Salaam  hivi karibuni. Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (wa tano kushoto waliosimama), Kaimu Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Kassim Hussein (wa sita kushoto) na baadhi ya wakurugenzi wa benki hiyo wakishuhudia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa program ya ufadhili ya NBC ambapo wanafunzi 60 watapata ufadhili katika vyuo vikuu vinne chini. Ufadhili huo wenye thamani ya shs milioni 300 utavihusu  Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Chuo cha Uhifadhi Wanyama Pori Mweka (CAWM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), na  Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Kulia ni wakuu wa vyuo hivyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein (katikati). akishikana mikono na Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Elimu  Dar es Salaam (DUCE), Prof. Godliving Mtui katika hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Chuo cha CBE, Dk. Emanuel Mjema.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dr. Imanueli  Mnzava akzungumza katika hafla hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu ua ufadhili ya benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.  
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Michael Mniko akiishukuru NBC kwa kutoa ufadhili huo akisema utaisaidia serikali katika azma yake ya kuinua kiwango cha elimu nchini.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages