Mkazi wa Jijini Dar es Salaam alalamika kutapeliwa nyumba na Taasisi




Mama mmoja afahamika  kwa jina la Editha Wambura, amejikuta akilala nje jana mara baada ya taasisi inayojishughulisha na udalali hapa nchini, YONO kuifunga nyumba yake yenye namba 58, iliyoko Kata ya Mikocheni mtaa wa Mpungani,  na kumtoa nje yeye pamoja na mtoto huku wakidai agizo hilo limetoka RITA .

Tukio hilo la kutolewa mama huyo nje ya lilitokea jana jioni huku chanzo cha kufungwa kwa nyumba hiyo kikidaiwa ni zuio kutoka kwa ndugu wa marehemu ambao wanashirikiana na  RITA ambao ndio wasimamizi wa Mirathi huku wakiamuru  YONO kufungia Nyumba hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa habari kwenye eneo la Nyumba hiyo, Editha Wambura, ambaye ni mke wa Marehemu ,James  Wambura, amesema  chanzo cha mgogoro huo ilitokea mara baada ya mumewe kufariki na kuacha baadhi ya mali ambazo ndugu zake walijitokeza na kuzidai.

Amesema kuwa, baada ya kufariki mumewe mwaka 2012, kuliibuka mizozo  mbali mbali huku ndugu wa mume wakimletea baadhi ya wanawake  wakidai amezaa nao  watoto 11.

Aidha, amesema kabla ya mumewe kufariki  hajawahi kuwaona hao watoto lakini leo analetewa, miongoni mwa wakina mama waliowaleta watoto hao ni pamoja na wafanyakazi wa Bar na mwalimu ambaye alimfundisha  mtoto wake alivyokuwa chekechea.

"Nashangaa sana ndugu waandishi, mimi na mume wangu tumefunga ndoa 1995, mpaka sasa tumebahatika kupata watoto 3, mmoja yupo darasa la saba na wengine wapo  chuo mwaka wa kwanza, kwani nini leo wanaletwa hawa, kuna namna hapa inafanyika kunidhurumu mali zangu nahangaika sana na hawa watoto nalipia ada, kula na maradhi juu yangu je wakichukua na hii mali iliyobakia  tutaishi vipi?"aliuliza mama huyo akionekana na uchungu mkubwa sana.

Ameongeza kuwa, mpaka sasa wana miaka 18 katika nyumba hiyo wanaishi hapo, amekuwa mtu wa kufuatiliwa sana na Yono pamoja na Rita, amesema Rita ndio wasimamizi wa Mirathi lakini  hawatendi haki wanaangalia upande wa ndugu wa marehemu, Mahakama haijatoa idhini yoyote ya kuondoka kwenye nyumba hiyo, kwanini wao wamechukua majukumu ya kumtoa nje?  hii ni  mara ya pili kuchukua vitu vyake vya ndani na kununua upya, hivyo amesema kuwa watu hao wanafanya unyanyasaji kwani hawafuati sheria wamekuwa watu wa kutumia nguvu pasipo na haki kutendeka.

Pia ametaja baadhi ya mali ambazo amechukuliwa, miongoni mwa mali hizo ni pamoja na fedha, magari 2, vifaa vya Ofisi, Msasani klabu, Trekta 2. 

Mama huyo amesema kuwa, alitegemea RITA wangekuwa msaada kwake lakini cha kushangaza wao ndo wanamnyanyasa wakati kesi hiyo bado ipo Mahakama Kuu na haijatolewa ufumbuzi.

Ameiomba Serikali ya  Rais Magufuli, Waziri husika wa Sheria na Waziri wa Ardhi,  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  pamoja na Mkuu wa Wilaya kuingilia kati suala hilo ili kuhakikisha kwamba anapata haki  zake zote ikiwemo zile walizochukua mwanzo.

Kwa Upande wake  kaimu Meneja wa masuala ya ufilisi na udhamini, RITA, Reinald Makoko, amesema kuwa kuhusiana na suala zima  la usimamizi wa  mirathi ya Marehemu James Wambura, ni kwamba waliteuliwa na Mahakama kuu tarehe 23/5/2014 kusimamia mirathi hiyo mara baada ya mgogoro baina ya warithi kutokuafikiana,hivyo  Mahakama ikaona kwamba kabiziwasi mkuu ndiye mtu pekee ambaye anawea kusimamia mirathi hiyo.

Hivyo baada ya kufuata sheria jana wakafanikiwa kumuondoa mama huyo kwenye hiyo nyumba kuhakikisha inauzwa au kupangishwa  ili warithi wote waweze kupata stahili yao.

"Mamama huyo sio mrithi, ni mtalaka wa muda mrefu wa Marehemu,  lakini ana haki ya kufuatilia sehemu ya mirathi hiyo ambayo ni stahili ya watoto wake watatu aliozaa na Marehemu, hivyo ilikuwa ni sahihi kumuondoa kwenye nyumba hiyo ili haki itendeke kwa warithi wote ikiwemo watoto alionao yeye" amesema  Mkoko.

Aidha ametoa wito na kusema kuwa upo umuhimu wa kuandika wosia kwa sababu itasaidia sana kuepusha migogoro ambayo inaweza kutokea baada ya mtu kufariki, hususani ni pale panapokuwa na warithi wengi au warithi mbali mbali wanaotoka kwenye matumbo tofauti, kwa mfano baba amezaa na wanawake wawili wale watoto kukaa pamoja na kuelewana ni vigumu, hivyo tunawakaribisha wananchi  kuja kwa ajili ya kuandika wosia kwa sababu Ofisi hiyo inaandika wosia kwa manufaa ambayo warithi watapenda mtu anufaike baada ya marehemu kufariki dunia.

 Mama huyo akiwa nje ya nyumba anayodai kutapeliwa.

Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages