Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dr. Bernard Kibesse (katikati), akiinua glasi ili kuitakia mafanikio bora benki ya Absa Tanzania akiwa pamoja na, kutoka kushoto; Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda wa Absa, Saviour Chibiya, Mwenyekiti wa Bodi ya Absa Tanzania, Simon Mponji na Mjumbe wa Bodi ya Absa Tanzania, DK. Suleiman Mohamed. Naibu Gavana Kibesse alikuwa megni rasmi katika hafla iliyoandaliwa na Absa kwa wateja wake jijini Dar es Salaama jana.
Benki Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse (kushoto), akilakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed alipoenda kuwa mgeni rasmi katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam jana ili kuwapa taarifa mbalimbali za utendaji wa benki hiyo ambayo awali iliitwa Barclays Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda wa Absa, Saviour Chibiya na Mwenyekiti wa Bodi ya Absa Tanzania, Simon Mponji.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse (kushoto), akikaribishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Absa Tanzania, Simon Mponji alipoenda kuwa mgeni rasmi katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam jana ili kuwapa taarifa mbalimbali za utendaji wa benki hiyo ambayo awali iliitwa Barclays Tanzania.. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Absa wa Kanda, Saviour Chibiya na Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Abdi Mohamed.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse (wa nne kushoto), akigonganisha glasi na wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam jana ili kuwapa taarifa mbalimbali za benki hiyo ambayo awali iliitwa Barclays Tanzania. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi, Dk. Suleiman Mohamed, Mkurugenzi wa Fedha, Obedi Laiser, Mwenyekiti wa Bodi, Simon Mponji na Mkurugenzi Mtendaji, Abdi Mohamed.
Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Abdi Mohamed (wa pili kulia), akiwa na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla hiyo katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Abdi Mohamed (kulia), Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Absa Tanzana, Aron Luhanga (katikati), pamoja na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa Absa wakigonganisha glasi ili kutakiana afya bora pamoja na mafanikio ya benki hiyo nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Abdi Mohamed, akigonganisha glasi na mmoja wa wakurugenzi wa benki hiyo, Esther Maruma (kushoto), katika hafla hiyo. Kulia ni Naibu Gavana wa BoT, Dk. Bernard Kibesse na Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda wa Absa, Saviour Chibiya.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Benard Kibesse akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya Absa Tanzania kwa ajili ya wateja wake na wadau wengine ili kuwajulisha mikakati mbalimbali ya benki hiyo ambayo awali iliitwa Barclays Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Selcom Tanzania, Sameer Hirji, mmoja wa waalikwa waliohudhuria katika hafla hiyo katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment