Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa droo ya mwezi Januari ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo ambapo jumla ya washindi watano walijishindia pikipiki mpya kila mmoja. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Masuli Masudi, Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye, Meneja Kampeni ya Malengo, Mtenya Chewa na mmoja wa washindi wa bodaboda wa droo ya Disemba, Rosemary Kibodya.
Meneja wa Kampeni ya Malengo wa Benki ya NBC, Mtenya Cheya ( wa pili kulia), akiziungumza kwa simu na mmoja wa washindi wa droo ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo aliyejishindia bodaboda. Juma ya washindi watano walishinda zawadi hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Masuli Masudi, Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo na Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye na mshindi wa bodaboda wa mwezi Disemba.
Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (kulia), akikabidhi zawadi ya bodaboda kwa Bi. Rosemary Kibodya, mmoja wa washindi wa droo ya mwezi Disemba mwaka jana wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo. Makabidhiano hayo yalifanyika pamoja na droo ya mwezi Januari ambapo jumla ya washindi watano waliojishindia bodaboda walipatikana. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Tawi la Corporate, Mariam Kombo na Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye.
Meneja wa Tawi la NBC Corporate, Mariam Kombo akikabidhi kadi ya pikipiki kwa Rosemary Kibodya, mmoja wa washindi wa droo ya mwezi Disemba mwaka jana wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo. Makabidhiano hayo yalifanyika pamoja na droo ya mwezi Januari ambapo jumla ya washindi watano waliojishindia bodaboda walipatikana.
Dar es Salaam Februari 19, 2020. BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), moja ya benki kongwe nchini imeendelea kuboresha maisha ya wateja wake kwa kuendelea kutoa zawadi mbalimbali kupitia kampeni yake inayoendelea ya akaunti ya Malengo iitwayo 'Ibuka Kidedea na NBC Malengo'.
Akizungumza wakati wa droo ya Mwezi Januari katika droo za kila mwezi za kampeni ya Ibuka Kidedea jijni Dar es Salaam leo, Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo alisema kampeni hiyo imeendelea kufanya vizuri tokea ilipozinduliwa Oktoba mwaka jana, ikishuhudia wateja wa zamani wakiweka amana katika akaunti zao za Malengo huku wateja wapya wakijiunga na NBC Malengo ili kujishindia zawadi na kunufaika na manufaa lukuki yanayopatikana sambamba na akaunti hiyo.
“Tunaposema ‘Ibuka Kidedea' ni kweli tunamaanisha, Kwani mjuavyo hadi sasa jumla ya washindi 10 wamejishindia zawadi za bodaboda huku washindi nane wameshinda safari za mapumziko kwenda sychelles na Serengeti.
“NBC Ibuka Kidedea imekuja kusaidia watanzania kutimiza malengo yao. Watanzania wana malengo mbalimbali kila mmoja ana malengo yake, natoa wito kwa wateja wetu na wasio wateja kujiunga na NBC Malengo ili kutimiza malengo yenu kwa urahisi na uhakika”, alisema Bi. Maria.
Bi Maria aliongeza kuwaNBC inajali maisha ya wateja wake na watanzania kwa ujumla na ndio sababu kila mara imekuwa ikiingiza bidhaa na huduma zinazoendana na kukidhi mahitaji halisi ya watanzania.
“NBC ni benki ya kizalendo, tunajua fika mahitaji halisi ya watanzania, tunajua mahitaji ya wateja wetu, akaunti ya Malengo ya NBC ni moja ya fursa iliyoletwa na NBC ili kumuwezesha mteja wetu kujiwekea akiba kidogo kidogo ili kutimiza malengo yake.
“NBC tunataka wateja wetu na watanzania wawe na utamaduni wa kujiwekea akiba hata Kama ni kidogo kidogo kwani mswahili wanasema 'bandu bandu humaliza gogo”, alisema.
Pamoja na hayo meneja huyo anasema wale wote wanaojiunga na NBC Malengo sio tu kupata nafasi ya kuibuka kidedea lakini pia wanashuhudia akaunti zao zikipata faida nono kila mwezi hivyo kuwasaidia kutimiza malengo yao.
“NBC hatuishii kwenye Malengo tu, tunaposema 'NBC Daima Karibu Nawe' tunamaanisha kuwa NBC ipo karibu na kila mmoja anayehitaji huduma za kibenki, iwe ni akaunti za vikundi, wanawake, mikopo ya aina mbalimbali, huduma za kibenki kwa wajasiriamali, wafanyakazi, katika sekta za kilimo na madini, kila mahali NBC tupo”, aliongeza Bi Maria.
Katika droo ya leo waahindi watano waliibuka kidedea na kujishindia pikipiki mpya aina ya Yamaha kila mmoja huku zawadi kubwa ikipangwa kuwa pikipiki ya miguu mitatu aina ya Toyo itakayotolewa katika droo kubwa inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Mbali na droo hiyo pia mshindi wa droo ya mwezi Disemba mwaka jana Bi. Rosemary Kibodya wa Dar es Salaam alikabidhiwa pikipiki yake katika tukio lililoshuhudiwa pia na wakaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.
No comments:
Post a Comment