Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, James Ngaluko (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa na Mkurugenzi wa Masoko, Rahma Ngassa (kulia), wakati wa uzinduzi wa DCB Skonga jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Na Mwandishi wetu,
KATIKA kuhakikisha wazazi na walezi wanakuwa na uhakika wa elimu ya watoto wao, Benki ya Biashara ya DCB imeongeza fursa zaidi kupitia akaunti yake DCB SKONGA kwa kuongeza DCB MINI SKONGA Ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu nchini.
Akizungumza kuhusu fursa hizo, Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, James Ngaluko alisema tofauti na mpango wa DCB Skonga uliokuwepo awali ambapo mzazi alipaswa kuweka akiba kuanzia mwaka mmoja hadi 17, sasa kwa kupitia DCB mini skonga mzazi anaweza kuweka akiba kidogo kidogo kwa kipindi cha miezi 12 na kupata uhakika wa elimu ya mtoto wake kwa muda wa miaka mitatu.
‘’mpango huu mpya wa DCB MINI SKONGA’’ mzazi au mlezi anakuwa na uhakika wa elimu ya mtoto kupitia akiba yake anayoweka kila mwezi lakini pia pindi anapopata ulemavu wa kudumu au kupoteza maisha, mtoto atasomeshwa kwa kipindi cha miaka mitatu bure.
Mkurugenzi huyo alisema licha ya DCB kuanzisha mpango huu mpya, bado wazazi wanaweza kuendelea kuweka akiba kupitia mpango wa awali wa ‘’DCB SKONGA’’ ambapo mzazi anapata uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi chuo kikuu kutokana na mpango aliouchagua kuanzia mwaka mmoja hadi miaka 17.
Kuhusu bidh aa hizo za DCB Skonga Bwana Ngaluko alisema watanzania wengi hasa wenye kipato cha wastani hukabiliwa na hofu nyingi mara wawazapo hatima ya elimu ya watoto wao kutokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kutokea kiasi cha kupunguza ama kuondoa kabisa uwezo wao wa kulipa gharama za elimu na mahitaji mengineyo.
“Kwa kupitia DCB Skonga au Mini Skonga mteja anapata fursa ya kuamua kiwango cha kuwekeza kila mwezi kwa ajili ya kutimiza ndoto zake lakini pia kupata uhakika wa elimu ya mtoto wake, DCB tunaondoa hofu ya mzazi kwani endapo kutatokea majanga yatakayosababisha ulemavu wa kudumu ama kifo kabla ya muda kukamilika, mtegemezi atarudishiwa kiasi cha pesa kilichowekwa tokea mwanzo na mtoto atalipiwa gharama zote za elimu pamoja na hela ya matumizi ya shule kwa kipindi chote kilichosalia cha mkataba”
“Natoa hamasa kwa wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuzitumia fursa za akaunti hizi kwani ndio suluhisho bora na lenye uhakika kwenye masuala ya elimu ya watoto wetu.
DCB tumeweka kipaumbele katika kutekeleza mipango ya serikali ya awamu ya tano kwa kutoa huduma za kibenki kwa Watanzania nchi nzima katika kutoa fursa na bidhaa zenye tija kwa wateja wetu. Elimu ni kitu muhimu sana kwenye maisha yetu hivyo tunaamini watanzania watakimbilia fursa hii ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao’’, aliongeza bwana Ngaluko
Nae Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Bi Rahma Ngassa aliongeza ‘’kupitia bidhaa hii ya DCB Mini Skongana DCB Skonga mteja anakuwa na uhakika wa usalama wa pesa zake, uhakika wa elimu ya mtoto hadi chuo kikuu, gawio nono la kila mwaka, uhakika wa mkopo wa dharura hadi asilimia 50 ya kiwango cha akiba alichowekeza, bima ya mazishi endapo mwenye akaunti/mume/mke au mtoto atakapofariki.
“Wazazi walindeni watoto wenu, wekeni mazingira bora ya maisha ya baadae, na njia pekee ya kuwezesha hili ni kujiunga na akaunti za DCB Skonga kwani licha ya manufaa ya elimu kwa watoto, endapo ukichangia kwa kipindi chote cha mkataba bila kusitisha kwasababu yoyote, benki itakurudishia amana zako zote ulizowekeza hivyo kukupa fursa ya kujiendeleza zaidi”.
No comments:
Post a Comment