NBC yasaidia waathirika wa mafuriko Lindi

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (wa pili kushoto), akipokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Mkoa wa Lindi, Iovin Mapunda vililivyotolewa na benki hiyo kusaidia waathirika wa maafa ya mafuriko yaliyosababishwa na mfua kubwa iliyonyesha mkoani humo hivi karibuni. Msaada huo ulijumuisha mashuka 1,000, katoni 1,000 za sabuni, kilo 500 za mchele, kilo 1,500za unga wa mahindi, kilo 750 za maharage na mikate 500. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (wa pili kushoto), akizungumza kabla ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Mkoa wa Lindi, Iovin Mapunda (wa tatu kushoto), vililivyotolewa na benki hiyo kusaidia waathirika wa maafa ya mafuriko yaliyosababishwa na mfua kubwa iliyonyesha mkoani humo hivi karibuni. Msaada huo ulijumuisha mashuka 1,000, katoni 1,000 za sabuni, kilo 500 za mchele, kilo 1,500 za unga wa mahindi, kilo 750 za maharage na mikate 500. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge.
 
NA MWANDISHI WETU

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa misaada mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko ya yaliyotokea mkoani Lindi Januari 27 mwaka huu na kusababisha vifo, uharibifu wa mali, makazi na miundombinu.

Akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, misaada hiyo hivi karibuni, Meneja wa NBC Mkoa wa Lindi,Iovin Mapunda alisema benki hiyo ya kizalendo imeguswa sana na tukio hilo na kuona umuhimu wa kusaidia.

“Tukiwa kama benki ya Kitanzania, tunaamini kuwa ni muhimu kwa watu waliokumbwa na majanga asilia kama haya kusaidiwa ili waweze kurejea katika maisha ya kawaida,” alisema.

Katika hafla hiyo NBC ilitoa msaada wa mashuka 1,000, katoni 1,000 za sabuni, kolo 500 za mchele, kilo 1,500 za unga wa mahindi, kilo 750 za maharage na mikate 500.

“Wafanyakazi wa NBC ma uongozi wake tupo pamoja nanyi katika kipindi hiki cha majonzi yaliyoletwa na tukio lisilotarajiwa linalotokana na hali ya hewa na sasa limechukua maisha ya Watanzania wenzetu.

“Tunaamini kuwa tunawajibika kuchangia chochote na hivyo kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwasaidia wenye mahitaji,” alisema Bw.  Mapunda.

Alisema kama ilivyotangazwa, mafuriko haya yaliharibu miundombinu, shule na madaraja, nyumba hivyo kuwaacha wakazi wa maeneo hayo bila makazi jambo linaloweza pia kusababisha kuenea kwa magonjwa ya mlipuko.

“Tunaahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuwasaidia waathirika wa majanga mbalimbali kwani ni wajibu wetu kutoa sehemu ya faida kwa jamii,” alisema.

Pamoja na hayo, Bw. Mapunda aliongeza kusema: “Kama benki kongwe nchini tukiwa na uzoefu katika kutoa huduma bora za kibenki kwa zaidi ya miaka 53 sasa, NBC tunaweka msisizitizo mkubwa katika kuhudumia jamii, hapa Lindi tumeunga mkono pia juhudi za serikali kwa kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa majengo ya vituo vya polisi na shule.”
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages