





























Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa (wa tatu kulia), akikabidhi baadhi ya misaada kwa Msimamizi wa Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Child in the Sun, Padri Paul Raj kinachoendeshwa chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kujitolea kusaidia jamii yenye mahitaji. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Sullivan Provost, Fanuel Nashon, Meneja wa shule hiyo, Richard Samwel Mkami pamoja na baadhi ya watoto wanaolelewa kituoni hapo.
Mkuu wa Shule ya Wavulana ya Sullivan Provost, Fanuel Nashon, akikabidhi baadhi ya misaada kwa mmoja ya watoto wanaoelelewa katika Kituo cha Kulelea Watoto wenye Mahitaji cha Child in the Sun kinachoendeshwa na kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kusaidia jamii yenye mahitajii. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu. Wengine kutoka kulia ni msimamizi wa kituo hicho, Padri Paul Raj, Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa pamoja na vijana wanaolelewa kituoni hapo.
Meneja wa shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost , Richard Samwel Mkami (kulia), akikabidhi baadhi ya misaada kwa Msimamizi wa Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Child in the Sun, Padri Paul Raj kinachoendeshwa chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kujitolea kusaidia jamii yenye mahitaji. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu. Wengine pichani ni vijana wanaolelewa katika kituo hicho. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi, (kushoto), akizungumza na wanahabari wakati wa mkutano wa mwaka wa wanahisa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya TPB, Dkt. Edmund B. Mndolwa.

Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya TPB, Dkt. Edmund B. Mndolwa (kulia), akizungumza na wanahabari wakati wa mkutano wa mwaka wa wanahisa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi,

Picha ya pamoja.
BENKI ya TPB imepata faida ya Shilingi bilioni 21 kabla ya kodi kwa mwaka 2020. Kiasi hicho ambacho kimepatikani kabla ya kodi, kinatajwa na uongozi wa benki kuwa ni kikubwa ukizingatia changamoto mbalimbali zilizojitokeza mwaka jana, hasa janga la Corona lililoathiri dunia nzima.
Akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa wanahisa jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo, Dkt. Edmund B. Mndolwa alisema benki hiyo inaendelea kufanya vizuri kwa kupata faida hiyo kabla ya kodi.
Utendaji kazi uliotukuka, ufanisi na umakini wa menejimeti ya benki huku wakisimamiwa kwa karibu na Bodi tumeweza kupata faida kubwa ambalo ni jambo la kujivunia sana kwa kufanya kazi kubwa kwa tija,’’ alisema Dkt. Mndolwa.
Alisema kwamba pamoja na kwamba benki hiyo ina mtaji mdogo, ikilinganishwa na benki nyingine, imeendelea kufanya vizuri katika nyanja zote kwa miaka takriban kumi.
Dkt. Mndolwa alisema kwamba benki hiyo itaendelea kujipanga na kupanua shughuli zake za kibenki nchini na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto za kiuchumi kwa sasa katika sekta ya fedha nchini.
Benki ya TPB ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 11 ya mwaka 1991, kama ilivyofanyiwa mabadiliko mwaka 1992. Mwaka 2016 jina la Benki lilibadilishwa na kuwa Benki ya TPB badala ya Benki ya Posta Tanzania.
Katika kuendelea kuelezea matukio makubwa Kwa mwaka 2020, Dkt. Mndolwa alisema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
iliziunganisha Benki ya TPB na Benki ya Biashara ya TIB.
Lengo likiwa kuunda benki kubwa ya serikali itakayo boresha huduma, kupanua wigo wa mtandao na kutengeneza faida kubwa.
Benki ya TPB itaendelea kuboresha huduma zake na kubuni huduma mpya zinazokidhi matarajio ya wateja na kuwafikia wateja wengi zaidi wa kipato cha chini. Miongoni mwa huduma kama hizo ni SONGESHA na M-KOBA ambazo zinatolewa na Benki ya TPB kwa kushirikiana na Kampuni ya simu ya Vodacom.
Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Edmund Mndolwa akimalizia taarifa yake amesema Benki ya TPB inafanya vizuri katika soko la mabenki na hivyo kutoa wito kwa wateja kuendelea kuiunga mkono Benki yao. Mwelekeo ni mzuri na ndiyo maana benki imeendelea kukua na hadi kufikisha thamani ya Mali za Shilingi trioni moja mwisho mwa mwaka 2020 ikishika nafasi ya Saba kati ya benki zaidi ya 50 kote nchini.
Wafanyakazi wa Benki ya Akiba wakiwa kwenye maandalizi kabla ya kuanza zoezi la kuchangia damu lilofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi kuelekea maadhimisho yake June 14, 2021.
Meneja Masoko wa Benki ya Akiba Commercial Bank PLC (ACB), Innocent Ishengoma akipima damu kabla ya kuanza zoezi la kuchangia damu lilofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi kuelekea maadhimisho yake June 14, 2021.Benki ya Taifa ya Biashara leo imezindua kampeni yake ya Twende Sawa na NBC yenye lengo la kuwafuata na kuwapa elimu wafanyabiashara wanaochipukia katika maeneo yao ya kazi na biashara. Kampeni hiyo imezinduliwa leo katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wakiwemo wafanyakazi na baadhi ya wateja wa benki hiyo.

Rais wa Jumuiya ya Urafiki wa Tanzania na Urusi Yuri Korobov (kushoto), akiteta jambo na Rais wa Jumuiya ya Wanadiaspora wa Kiafrika nchini Urusi Dk. Prof Zunebe Kinfu Tafesse wakati walipokutana kujadili namna watakavyoungana na Tanzania kuunda miradi ya pamoja ya mazingira mazungumzo hayo yalifanyika nchini Urusi hivi karibuni.




