Absa Group Reports 3% Increase in Earnings, Bolstered by Improved SA Retail and Business Banking Unit Performance


Absa Group Limited, one of Africa’s largest financial services providers and parent company of Barclays Tanzania reported a 3% increase in earnings for the first half of 2019 as its retail unit in South Africa gained market share, mitigating the negative effects of a difficult economy.

Absa Group, which has a presence in 12 countries in Africa and an office in London, said normalised headline earnings increased to R8.3 billion during the first six months of the year from R8.04 billion during the same period in 2018. Income and costs both grew at 6%. Normalised earnings are considered the best measure of underlying group performance as it strips out the distorting effect of items related to the separation from Barclays PLC.

“Despite the tough operating environment, we have been able to maintain revenue momentum in our key target areas, with total revenue growth improving to 6%,” said Jason Quinn, Absa Group Financial Director.

Absa Group’s largest business unit, Retail and Business Banking South Africa (RBB SA), is showing faster than market growth in key product areas, in line with the group’s commitment to regain its leading position. RBB SA increased its share of home loans new business, with home loan registrations growing 16% - more than double the growth in total home loan registrations in South Africa during the first half. Retail deposits grew 12% while the market increased 9%. New personal loans increased 20%. RBB SA reported a 4% increase in earnings.

Corporate and Investment Banking (CIB) earnings decreased 5% on a pan-African basis, following a difficult trading period in South Africa. However, the client franchise continued to perform well with notable client acquisitions across the countries in which Absa has a presence. The corporate franchise extended its track record of double-digit revenue growth.

Absa’s subsidiaries outside of South Africa, collectively known as Absa Regional Operations (ARO), continued to increase their contribution to group earnings. ARO’s earnings rose 8% during the period, to account for more than a fifth of total Absa Group earnings.

Business Review

“We’ve made significant progress with Absa’s reorganisation following the implementation of our new strategy in March 2018, and we are beginning to see the benefits,” said René van Wyk, Absa Group CEO. “There is still, however, significant work to be done before we can reach our growth, returns and cost targets - a difficult task in a challenging environment,” he said.

RBB SA, which accounts for more than 60% of Absa group income, has largely completed its reorganisation and expects to reap further benefits from its integration with Absa’s wealth and investment management and insurance business. The integration, which is underway, will result in a seamless offer for customers between banking and non-banking services.

At CIB, significant work has been undertaken to form an integrated pan-African franchise with a single growth strategy that covers all of the countries where Absa has a presence.

ARO is implementing its new operating model, aligned to the group strategy which devolves accountability and decision-making closer to the customer interface.

“ARO remains a key contributor to the Group’s performance and with our strong focus on entrenching our brand across the African continent, we have built a strong base to drive growth and to attain our pan-African aspirations. Our results reflect a financial institution that has paid attention to market demand and the need to focus on regionally sourced earnings and growth,” said Peter Matlare, Deputy Chief Executive Officer, Absa Group and ARO CEO.

Matlare added: “Our investments in digitalisation and new ways of banking allow us to challenge existing models and positions Absa for growth. Our investment focus is to ensure that our brand delivers sustainable returns in complex markets, which require a deep understanding of local requirements and the need to always put the client at the heart of the business.”

Parallel to the reorganisation work across business units, Absa continues to make good progress in separating its operations from Barclays PLC, and in enhancing its digital capability.

After launching ChatBanking on WhatsApp, Samsung Pay, Timiza and Jumo, earlier, Absa significantly enhanced its Absa app in the first half of the year, resulting in a 20% increase in the number of app users.

Outlook

South Africa’s economic growth outlook appears muted, with gross domestic product (GDP) expected to grow 0.5% in 2019. The prospects for stronger growth are constrained by the slowing global economy, plus weak business sentiment and decelerating household income growth in South Africa. In the group’s ARO markets, GDP is expected to grow 5.5%.

“While Absa’s return on equity (RoE) is likely to be marginally lower in 2019, the group remains committed to its RoE target of 18% to 20% in 2021,” Quinn said.

Absa Group headline earnings (South African Rand million)


Note: Normalised financial results, which strip out the distorting effect of separation-related items, are presented to better reflect the Group’s underlying performance.
Share:

NBC yazidi kuboresha mtandao wa mawakala wake

Na Mwandishi Wetu,
BENKI ya NBC imewahakikishia wateja na wananchi kwa ujumla kuwa mtandao wa mawakala wake unazidi kuongezeka sehemu mbalimbali nchini kote huku wakizidi kuboresha huduma za NBC Wakala ili kuhakikisha wateja wanapata huduma bora na zinazokidhi mahitaji yao.

Akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa Mawakala wake zaidi ya 600 jijini Dar es Salaam hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi alisema pamoja na kuboresha mtandao wa mawakala benki imeendelea pia kuboresha mtandao wake wa kidigitali, ATM na matawi yao yaliyotapakaa sehemu mbalimbali nchini.

Akizungumzia kuhusu semina mawakala Bwana Sabi alisema, semina hiyo pamoja na kwamba ni matakwa ya ya kisheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), bali pia wanapata fursa ya kukutana na wafanyabiashara na kuzungumza jinsi biashara inavyokwenda, maeneo ya kuboresha, changamoto zinazowakabili na kuona jinsi benki inavyoweza kuzitatua.

“Tumezungumza mengi, lakini zaidi ni fursa kwa walaji wa mwisho za huduma za kibenki, tumeweza kuwaeleza mawakala juu ya huduma za benki na jinsi mtandao huu wa mawakala unaokuwa kwa kasi unavyoimarika, na pia ambavyo tunaendelea kuboresha huduma zetu.

“Utaratibu huu utaendelea japo mara mbili kila mwaka ili kuhakikisha tunakuwa karibu sana na wenzetu hawa mawakala  ambao ni muhimu sana kwetu katika kuhakikisha  walaji wa mwisho wa huduma zetu wanapata huduma zilizo bora na zinazokidhi mahitaji yao,” aliongeza mkurugenzi huyo.  

Naye Mkuu wa Huduma za Benki Kidigitali wa NBC, Deogratius Mosha alisema NBC Wakala iliyoanza Mwezi June, 2018 na kufikisha mawakala zaidi ya 1800 ni moja ya mkakati wa benk hiyo katika kuunga mkono azma ya serikali katika kuhakikisha wananchi walio wengi wanafikiwa na huduma za kibenki.

“Tumekutana hapa ili kufahamu kutoka kwao yale yanayojiri katika maeneo wanayofanyia biashara na pia kuwajengea uwezo na elimu ya utoaji wa huduma za kibenki sambamba na kanuni za sheria ya utoaji wa huduma za kibenki inavyotaka tufanye,” alisema.    

Pamoja na hayo alisema NBC ipo mbioni katika kuhakikisha kuwa huduma zao nyingi zinapatikana kupitia mawakala kama kufungua akaunti za papo hapo (fasta akaunti), vituo vya kukusanya taarifa za miamala, huduma za mikopo, bima, taarifa za ubadilishaji wa fedha za kigeni, na pia wateja kuwasilisha malalamiko na maoni kuhusu huduma za NBC tofauti na ilivyo sasa ambapo huduma hizo hupatikana katika matawi pekee.

“NBC inayo malengo kuwa ifikapo Mwaka 2020 sehemu kubwa ya huduma zinazopatikana kwenye matawi ziweze kupatikana kupitia mawakala wao na hiyo itawasaidia pia katika kuwaongezea kipato,” aliongeza Bwana Mosha.

Mmoja wa Mawakala waliohudhuria semina hiyo, Mama Tumaini Bureta wa Mikocheni, Dar es Salaam alitoa pongezi kwa NBC akisema amejifunza mengi hapo ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki hivyo ana matumaini mrejesho waliotoa kwa NBC ukitekelezwa unaweza kuboresha huduma wazitoazo na wao kufaidika kwa sehemu kubwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, akizungumza na baadhi ya mawakala wa benki hiyo wakati wa Semina ya siku moja kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkuu wa huduma za benki kidigitali wa Benki ya NBC, Deogratius Mosha, akizungumza na baadhi ya mawakala wa benki hiyo wakati wa Semina ya siku moja kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Meneja Ukuzaji wa Biashara wa Kitengo cha biashara ndogondogo na za kati wa Benki ya Taifa ya Biashara, Jonathan Bitababaje, akizungumza na baadhi ya mawakala wa benki hiyo wakati wa Semina ya siku moja kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, akizungumza na baadhi ya mawakala wa benki hiyo wakati wa Semina ya siku moja kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Pamoja naye ni baadhi ya maofisa wa ngazi za juu wa benki hiyo.
Mkuu wa huduma za benki kidigitali wa Benki ya NBC, Deogratius Mosha (kushoto), akikabidhi cheti kwa mmoja wa mawakala wao Monica Kikoti baada ya kuhudhuria semina kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya Mawakala wa Benki ya NBC wakihudhuria semina iliyoandaliwa na benki hiyo juu ya utoaji wa huduma za kifedha kupitia NBC Wakala, jijini hivi karibuni.
Mnadhimu Mkuu Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NBC, Joyce Mbago (kushoto), akikabidhi cheti cha wakala wa benki hiyo Dianarose Buddybruno katika semina kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala hao iliyoandaliwa na NBC jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Share:

FAINALI ZA PROPHET SUGUYE CUP ZAFANA

Na Mwandishi Wetu,
Mashindano ya mpira wa miguu yaliyopewa jina la Prophet Suguye Cup ambayo yalikuwa yanatimua vumbi katika viwanja vya Shule ya Msingi Misitu iliyopo Kivule, Ukonga, Dar es Salaam na kudhaminiwa na Muasisi wa Mashindano hayo Nabii Nicolaus Suguye wa Kanisa la WRM lenye Makao yake Makuu Kivule matembele ya Pili, Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa mshindi wa mashindano hayo, muasisi wa mashindano hayo Nabii Nicolaus Suguye amesema lengo la Mashindano hayo ni kuwaweka pamoja na kuwahamasisha vijana kufanya kazi ili kuwasaidia kukwepa maovu yatokanayo na kukaa vijiweni bila shughuli maalumu.

Mashindano hayo yalianza kutimua vumbi tarehe 25 Mei 2019 na kufikia tamati hapo jumamosi ya tarehe 10 Agosti 2019 kwa timu ya FAIRPLAY kuibuka wafalme wa kwanza wa mashindano hayo yaliyoshirikisha timu 24 kutoka maeneo yanayounganisha jimbo la Ukonga wilayani Ilala, Dar es Salaam.

Timu ya FAIRPLAY ya KIVULE jijini DAR ES SALAAM imeibuka kidedea na kuchukua ubingwa wa mashindano hayo baada ya kuichabanga timu ya KIVULE FOREST kwa jumla ya bao mbili kwa moja, katika fainali ya ligi ya mpira wa miguu ya PROPHET SUGUYE CUP.


Wachezaji wa Fairplay FC wakifurahia baada yakukabidhiwa kombe na Nabii Nicolaus Suguye wa Kanisa la WRM na Muanzilishi wa ligi hiyo, wakati wa mchezo wa fainali katika mchezo wa Ligi ya Prophet  Suguye Cup iliyokuwa ikiendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo Fair Play iliibuka kidedea kwa mabao 2-1. Nakufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika Mchezo huo nakukabidhiwa kombe na Mwanzilishi wa ligi hiyo Nabii Nicolaus Suguye.
Mshambuliaji wa timu ya Fair Play FC, akijaribu kuwatoka mabeki wa  Kivule Forest FC, wakati wa mchezo wa Fainali Ligi ya Prophet  Suguye Cup iliyokuwa ikiendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule nje kidogo ya Jiji la DaresSalaam ambapo Fair Play iliibuka kidedea kwa mabao 2-1, nakufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika mchezo huo nakukabidhiwa kombe na Mwanzilishi wa ligi hiyo Nabii Nicolaus Suguye wa kanisa la WRM.
Nahodha wa Fair Play akipokea kombe kutoka kwa Mwanzilishi wa ligi hiyo Nabii Nicolaus Suguye wa kanisa la WRM baada ya kuibuka na ushindi wakati wa mchezo wa Fainali katika mchezo wa Ligi ya Prophet Suguye Cup iliyokuwa ikiendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo ambapo Fair Play iliibuka kidedea kwa mabao 2-1. Nakufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika   Mchezo huo nakukabidhiwa kombe na Mwanzilishi wa ligi hiyo Nabii Nichoraus Suguye wa kanisa la WRM lililopo Kivule Matembele ya pili, Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Nahodha wa Kivule Forest FC, Jolvin Balotel akipokea kombe kutoka kwa Nabii wa Kanisa la UKOMBOZI MINISTRIES FOR ALL NATIONS-BG.MALISA baada ya kushika nafasi ya pili wakati wa mchezo wa Fainali Ligi ya Prophet Suguye Cup iliyokuwa ikiendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo Fair Play iliibuka kidedea kwa mabao 2-1. Nakufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika Mchezo huo.
Nahodha wa Kivule FC akionesha kombe baada yakukabidhiwa.
Wachezaji wa timu hizo wakiwania mpira wakati wa mchezo wa fainali.
Share:

RAIS WA AFRIKA KUSINI KUTUA NCHINI JUMATANO NA KUPOKELEWA NA RAIS DKT. JOHN MAGUFULI


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuwasili Nchini Jumatano ya August 14 kwa Mwaliko wa Ziara ya kitaifa (State Visit) ya siku mbili ambapo atapokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema Rais Ramaphosia atawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere majira ya Saa Tano usiku na baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili ataendelea kubaki Nchini kwaajili ya kushiriki Mkutano Mkubwa wa Viongozi wakuu Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika SADC.

Aidha RC Makonda amesema Maraisi wa Mataifa mengine wataendelea kuingia Nchini kuanzia August 16 ambapo amewataka wananchi kuwa wakarimu kwa wageni na kutumia vizuri fursa ya ujio wa Viongozi hao.
Share:

DCB KUSHIRIKIANA NA MANISPAA KUTEKELEZA MIRADI YA KIMKAKATI

Na Mwandishi wetu, Mwanza.

BENKI ya Biashara ya DCB imesema itaendelea kushirikiana kwa karibu zaidi na manispaa mbalimbali nchini na kwa sasa ikija na mpango maalumu kupitia huduma maalumu (municipal bonds), ili kuziwezesha manispaa hizo kupata pesa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimkakati.

Akizungumza Jijini Mwanza hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa alisema mpango huo utakaosaidia upatikaji wa fedha kuendesha miradi ya kimkakati una masharti wezeshi kwa mkopaji na tayari wameshaanza mazungumzo na manispaa na wadau wengine muhimu katika mchakato huo.

“Mchakato wa uanzishwaji wa huduma hii unaendelea tutakachofanya ni kuongeza manispaa na halmashauri nyingine ambazo pia zina miradi ya kimkakati kuweza kujumuishwa kwenye mpango huu.

“Ombi langu ni kwamba najua vyanzo viko vingi lakini hii yenyewe inaweza ikawa chanzo kizuri cha kutafuta pesa, na vilevile ni chanzo kizuri kwa ajili ya kusaidia umma wa wawekezaji wakubwa na wadogo kupata fursa ya kuwekeza kwenye miradi yetu”, aliongeza.

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa DCB alizungumzia pia udhamini na ushiriki wao katika mikutano mbalimbali na shughuli za kijamii ikiwemo Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirikisho la Serikali za Mitaa (ALAT) uliofanyika mjini Mwanza hivi karibuni akisema hiyo imetokana na azma ya kuanzishwa kwa benki hiyo ikiwa na kuwahudumia wananchi na wajasiriamali wadogowadogo hasa wanawake na vijana na kufanikiwa kwa azma hiyo kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na ushirikiano kutoka katika manispaa na halmashari za Jiji la Dar es Salaam ilikoanzishwa.

“Tumekuwa tukishirikiana kwa karibu sana na manispaa na halmashauri zote za Jiji la Dar es Salaam katika kutoa mikopo ya wanawake na vijana na mafanikio ni makubwa mpaka sasa hivi ukiaangalia hiyo pesa iliyotoka  na wanufaika wamenufaika mara tatu na hii ni kwa sababu ya weledi na uzoefu tulionao”, alisema.

Akizungumza mafanikio ya zoezi la uuzaji hisa lililofanyika hivi karibuni Bwana Ndalahwa alisema zoezi hilo lilifanikiwa kwa asilimia 108  na hiyo imechangiwa sana na   historia yao na mahusiano yao ya karibu na manispaa na halmashauri kwa maana ya kwamba wao ndiyo waanzilishi.

Kuhusu maendeleo ya DCB na mikakati ya kuzidi kujipanua, Mkurugenzi wa DCB alisema wigo wa kufanya biashara umeongezeka kutoka Dar es Salaam pekee na sasa wameruhusiwa kuendesha biashara nchini nzima wakiwa na matawi manane likiwemo la Dodoma pamoja na  mawakala 1000 nchi nzima huku wakipatikana kwenye mtandao hivyo huduma zao kupatikana nchi nzima.

Pamoja na hayo mkurugenzi hiyo alizungumzia huduma yao mpya ya DCB Lamba kwanza inayomwezesha mteja kupata riba ya hadi asilimia 14 siku mteja anapoamua kuwekeza huku akitoa wito kwa watanzania kujiunga na huduma ya DCB Digital kwa njia ya simu za mkononi kwa kubonyeza alama ya nyota 150 nyota 85 reli ili kujiunga na kupata huduma mbalimbali za benki hiyo kwa lugha rahisi wakiita ‘DCB kwanza simu  yako Tawi letu’.

Benki ya DCB ilianzishwa mwaka 2002, ikianzishwa na Maspaa za Dar es Salaam na kujulikana kama Benki ya Wananchi wa Dar es Salaam. Lengo kuu ilikuwa ni kusaidia wajasiriamali wadogowadogo. Baada ya kuanzishwa iliweza kutekeleza lengo hilo na na kuendelea kukua. Mwaka 2008 ilikuwa benki ya kwanza kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), na iliendelea kukua hivyo hivyo na baadae kubadilisha jina kutoka Dar es Salaam Community Bank na  kuwa DCB Commercial Bank kwa sasa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto), akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya  DCB, Godfrey Ndalahwa kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirikisho la Serikali za Mitaa (ALAT), uliofanyika mjini Mwanza hivi karibuni. Katikati ni Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo.  (Picha na DCB).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa baada ya kukabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa (hayupo pichani), kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirikisho la Serikali za Mitaa (ALAT), uliofanyika mjini Mwanza hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo.  (Picha na DCB).
Share:

WAFANYAKAZI WAPYA BODI YA MAPATO ZANZIBAR WAPEWA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO


Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Joseph Abdallah Meza akifungua mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wapya wa ZRB, mafunzo hayo yamefanyika Ofisi za Mtakwimu Mazizini Mjini Zanzibar.
Wafanyakazi wapya wa ZRB wakisikiliza kwa makini hutuba ya ufunguzi iliyotolewa na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Joseph Abdallah Meza (hayupo pichani).
Asma Khamis Hassan, ICT Officer ZRB ni miongoni mwa wafanyakazi wapya akiuliza swali wakati wa mafunzo hayo.
Mgeni rasmi Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Joseph Abdallah Meza (katikati) akipokea maswali kwa wafanyakazi  wake. Kulia ni Afisa Mahusiano wa ZRB Makame Khamis Muh’d na kushoto ni Mkurugenzi Rasilimali Watu na Uendeshaji, Mohamed Amour Mohamed.
Share:

NBC kuendelea kuisaidia serikali kufanikisha miradi ya maendeleo nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Hazina na Masoko ya Fedha  wa Benki ya NBC,Peter Nalitolela akizungumza katika kongamano la siku moja kuhusu mitaji ya fedha na usimamizi wa hatari zinazoweza kutokea katika miamala  ya kifedha kwa wadau kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Benki Kuu ya Tanzania, Tanesco, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kongamano hilo lilifanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), imesema itaendelea kushirikiana kikamilifu na serikali ya awamu ya tano katika azma yake ya kuwaletea wananchi wake uchumi wa kweli na maendeleo imeelezwa jijini Dodoma mwisho mwa wiki.

Akizungumza wakati wa kongamano la wadau  juu ya upatikaji wa fedha  na usimamizi wa hatari zinazoweza kujitokeza katika miamala ya kifedha lililoandaliwa kwa wadau, Mkurugenzi wa Idara ya Hazina na Masoko wa NBC, Peter Nalitolela alisema NBC imejizatiti kushirikiana na serikali na taasisi zake katika kuhakikisha nchi inafaidika na kiasi cha pesa inachotumia katika   miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo inayoendelea kufanyika.

Alisema kongamano hilo lililohudhuriwa na wadau kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tanesco, TPDC na Wizara ya Fedha na Mipango lilikuwa na lengo kubwa ya kuangalia vyanzo mbalimbali vya fedha vinavyopatikana katika miradi mbalimbali mikubwa inayofanywa na serikali pamoja na kuangalia usimamizi wa hatari katika miamala ya kifedha inayoweza kutokea katika miradi hiyo.

“Kama mjuavyo miradi mbalimbali mikubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya tano kama vile mradi wa reli ya kisasa (SGR), mradi wa umeme wa Mto Rufiji wa Stiegler’s Gorge, ujenzi wa barabara na madaraja, baadhi ya miradi hufanywa kwa mikopo kutoka pande tofauti, hivyo tulitaka kuonyesha uwezo wetu kama NBC katika kusaidia upatikanaji wa fedha na pia linapokuja suala la uzimamizi wa hatari za kifedha katika miamala hiyo.

“Kilicho kikubwa ni kwa NBC kuangalia uwezo wetu kwa njia tofauti tofauti ikiwemo katika kukopesha, lakini pia kuona serikali haipati hasara kutokana na masuala ya riba, fedha za kigeni na kushuka kwa thamani ya shilingi, hivyo NBC tumejiandaa kushirikiana na serikali kikamilifu katika kutimiza azma yake, kwa uwezo wetu tunaweza kushirikiana zaidi na zaidi”, aliongeza Bwana Nalitolela.    

Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo alisema kama inavyofahamika kuwa NBC inamilikiwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania, Benki ya Absa ya Afrika Kusini pamoja na Benki ya Dunia,hii huiweka NBC katika nafasi nzuri ya kusaidia juhudi za serikali.




Katika kongamano hilo pia NBC Ilileta wataalam kutoka benki mama ya Absa ili kuweza kuonyesha uzoefu wao walioupata kupitia miamala waliyofanya na serikali za nchi mbalimbali barani Afrika.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (353) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (132) MICHEZO (41) SIASA (3)

Pages