NBC yazidi kuboresha mtandao wa mawakala wake

Na Mwandishi Wetu,
BENKI ya NBC imewahakikishia wateja na wananchi kwa ujumla kuwa mtandao wa mawakala wake unazidi kuongezeka sehemu mbalimbali nchini kote huku wakizidi kuboresha huduma za NBC Wakala ili kuhakikisha wateja wanapata huduma bora na zinazokidhi mahitaji yao.

Akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa Mawakala wake zaidi ya 600 jijini Dar es Salaam hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi alisema pamoja na kuboresha mtandao wa mawakala benki imeendelea pia kuboresha mtandao wake wa kidigitali, ATM na matawi yao yaliyotapakaa sehemu mbalimbali nchini.

Akizungumzia kuhusu semina mawakala Bwana Sabi alisema, semina hiyo pamoja na kwamba ni matakwa ya ya kisheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), bali pia wanapata fursa ya kukutana na wafanyabiashara na kuzungumza jinsi biashara inavyokwenda, maeneo ya kuboresha, changamoto zinazowakabili na kuona jinsi benki inavyoweza kuzitatua.

“Tumezungumza mengi, lakini zaidi ni fursa kwa walaji wa mwisho za huduma za kibenki, tumeweza kuwaeleza mawakala juu ya huduma za benki na jinsi mtandao huu wa mawakala unaokuwa kwa kasi unavyoimarika, na pia ambavyo tunaendelea kuboresha huduma zetu.

“Utaratibu huu utaendelea japo mara mbili kila mwaka ili kuhakikisha tunakuwa karibu sana na wenzetu hawa mawakala  ambao ni muhimu sana kwetu katika kuhakikisha  walaji wa mwisho wa huduma zetu wanapata huduma zilizo bora na zinazokidhi mahitaji yao,” aliongeza mkurugenzi huyo.  

Naye Mkuu wa Huduma za Benki Kidigitali wa NBC, Deogratius Mosha alisema NBC Wakala iliyoanza Mwezi June, 2018 na kufikisha mawakala zaidi ya 1800 ni moja ya mkakati wa benk hiyo katika kuunga mkono azma ya serikali katika kuhakikisha wananchi walio wengi wanafikiwa na huduma za kibenki.

“Tumekutana hapa ili kufahamu kutoka kwao yale yanayojiri katika maeneo wanayofanyia biashara na pia kuwajengea uwezo na elimu ya utoaji wa huduma za kibenki sambamba na kanuni za sheria ya utoaji wa huduma za kibenki inavyotaka tufanye,” alisema.    

Pamoja na hayo alisema NBC ipo mbioni katika kuhakikisha kuwa huduma zao nyingi zinapatikana kupitia mawakala kama kufungua akaunti za papo hapo (fasta akaunti), vituo vya kukusanya taarifa za miamala, huduma za mikopo, bima, taarifa za ubadilishaji wa fedha za kigeni, na pia wateja kuwasilisha malalamiko na maoni kuhusu huduma za NBC tofauti na ilivyo sasa ambapo huduma hizo hupatikana katika matawi pekee.

“NBC inayo malengo kuwa ifikapo Mwaka 2020 sehemu kubwa ya huduma zinazopatikana kwenye matawi ziweze kupatikana kupitia mawakala wao na hiyo itawasaidia pia katika kuwaongezea kipato,” aliongeza Bwana Mosha.

Mmoja wa Mawakala waliohudhuria semina hiyo, Mama Tumaini Bureta wa Mikocheni, Dar es Salaam alitoa pongezi kwa NBC akisema amejifunza mengi hapo ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki hivyo ana matumaini mrejesho waliotoa kwa NBC ukitekelezwa unaweza kuboresha huduma wazitoazo na wao kufaidika kwa sehemu kubwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, akizungumza na baadhi ya mawakala wa benki hiyo wakati wa Semina ya siku moja kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkuu wa huduma za benki kidigitali wa Benki ya NBC, Deogratius Mosha, akizungumza na baadhi ya mawakala wa benki hiyo wakati wa Semina ya siku moja kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Meneja Ukuzaji wa Biashara wa Kitengo cha biashara ndogondogo na za kati wa Benki ya Taifa ya Biashara, Jonathan Bitababaje, akizungumza na baadhi ya mawakala wa benki hiyo wakati wa Semina ya siku moja kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, akizungumza na baadhi ya mawakala wa benki hiyo wakati wa Semina ya siku moja kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Pamoja naye ni baadhi ya maofisa wa ngazi za juu wa benki hiyo.
Mkuu wa huduma za benki kidigitali wa Benki ya NBC, Deogratius Mosha (kushoto), akikabidhi cheti kwa mmoja wa mawakala wao Monica Kikoti baada ya kuhudhuria semina kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya Mawakala wa Benki ya NBC wakihudhuria semina iliyoandaliwa na benki hiyo juu ya utoaji wa huduma za kifedha kupitia NBC Wakala, jijini hivi karibuni.
Mnadhimu Mkuu Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NBC, Joyce Mbago (kushoto), akikabidhi cheti cha wakala wa benki hiyo Dianarose Buddybruno katika semina kuhusu elimu ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala hao iliyoandaliwa na NBC jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages