AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA





Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Akiba Bw: Silvest Arumasi, amezindua rasmi wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Kijitonyama. Katika uzinduzi huo, Mkurugenzi amewashukuru wateja kwa kuichagua na kuiamini Benki ya Akiba katika kuwahudumia. Aidha, ameendelea kuwaahidi na kuwahakikishia wateja huduma bora kutoka ACB.

Sherehe za huduma kwa wateja zina adhimishwa katika matawi yote ya ACB na hivyo Bw: Arumasi amewaalika wateja wote kutembelea matawi ya Akiba kwa ajili ya kusherekea wiki hii ya huduma kwa wateja pamoja na kupata taarifa mbali mbali za huduma mpya na maboresho mbali mbali. Mwisho kabisa

Mkurugenzi amewashukuru wateja wote walioshiriki katika zoezi la utafiti wa viwango vya uridhikaji katika utoa huduma yaani (Customer Satisfaction Survey) lililoratibiwa na kampuni huru ya kujitegemea kwa lengo la kuhakikisha uwazi na uhuru wa kutoa maoni kwa wateja.

ACB inao utamaduni wa kufanya utafiti huo kila mwaka na hivyo amewasihi wateja kushiriki tena kikamilifu kwa lengo la kupata maoni na mirejesho itakayosaidioa kuboresha huduma zitolewazo.



 

 

 

Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages