Benki ya Biashara
ya DCB imetangaza kumaliza kampeni ya bidhaa yake ya akaunti ya muda maalumu
inayojulikana kama ‘DCB Lamba Kwanza’ kwa mafanikio makubwa huku ikivuka
malengo yake iliyojiwekea ya shilingi Bilion 15 na kuongeza amana kwa shilingi
Bilioni 18.5 ambayo ni zaidi ya asilimia 123.
Kampeni ya DCB
Lamba Kwanza iliyozinduliwa Mei 29 mwaka huu na kudumu kwa muda wa miezi
mitatu huku ikiwa na lengo la kukusanya amana za kiasi cha shilingi Bilioni 15,
iliwawezesha wateja wa benki hiyo kuwekeza na kupata riba ya hadi asilimia 14 ya
amana wanayowekeza ambapo mteja alianza kupokea riba yake ya mwezi
papo hapo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko alisema ‘tunatoa
shukurani zetu za dhati kwa wateja wetu kwa kuweza kuipokea bidhaa hii na
kuweza kunufaika nayo kwani wamenufaika sana, kila mwezi
umekua mwezi wa faida. Mteja anafurahia riba yake inayolipwa mwanzo wa mwezi
kila mwezi, malipo ya riba ni rafiki mteja anaweza kuwekeza kuanzia miezi
mitatu (3) mpaka miaka miwili (2). Ni jambo la fahari kuona Benki ya kitanzania
inatoa fursa kwa Watanzania na kuwawezesha kuboresha maisha na uchumi’.
Alisema DCB Lamba
Kwanza imepokewa kwa mikono miwili na wateja wetu na kufanikiwa kuvuka malengo
kwa kukusanya amana ya zaidi ya shs bilioni 18.5 ambapo awali Benki ilikusudia
kuuza kiasi cha shs bilioni 15.
“Kwa namna ya kipekee ningependa kwanza kabisa
kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kila bidhaa
tunayoiingiza sokoni na kutuwezesha kuvuka malengo hii inaonyesha ni jinsi gani
DCB inavyo aminika kwenye soko.
“Benki ya DCB
tupo imara na tumejidhatiti katika kubuni na kuingiza bidhaa zitakazokidhi kiu
ya mahitaji ya huduma za kifedha kwa wateja wetu,”
Kwa sasa benki imeendelea
kufanya maboresho katika baadhi ya huduma zake ikiwa ni pamoja na kupunguza
riba na kuongeza muda wa marejesho hadi miaka 15 kwa mikopo ya ujenzi na
ununuaji wa nyumba za makazi kwa wateja wetu wote hususan wafanyabiashara na
waajiriwa. Hii imefanya benki yetu kuongoza kutoa mikopo mingi zaidi ya ujenzi
wa nyumba na ununuaji wa nyumba Tanzania. (kwa takwimu za Tanzania Mortage
Refinance-taasisi iliyo chini ya benki kuu). Tunatoa wito kwa wajasiriamali
wote na wafanyakazi wenye lengo la kununua au kujenga nyumba kuwahi fursa hii.
Vilevile benki
inatoa huduma za kidigitali kupitia DCB DIGITAL inayomuwezesha mteja kufungua
akaunti kupitia simu yake ya mkononi, DCB sokoni inayomsaidia mkulima,wenye
viwanda vya kilimo pamoja na wafanya
biashara wa kilimo kwenye mnyororo wa thamani. Vile vile tuna akaunti na huduma
nyingi zinazotoa fursa kwa watanzania kuweka akiba lakini pia kupata faida ya
fedha zao.
Kampeni hii ni muendelezo wa mafanikio
yanayofanywa na Benki ya DCB kwani Benki hii imeendelea kupata faida, na
kufikia kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka
huu imeweza kupata faida ya sh. bilioni 1.2 ikiwakilisha ongezeko la asilimia
118% kutoka faida ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2018. Utendaji wa benki
umeimarika,huku ufanisi katika nyanja zote muhimu ukiongezeka kwa kiwango cha
kuridhisha ukichagizwa na kukua kwa biashara na ukusanyaji wa mikopo chechefu. Vile
vile benki imeendelea kuvunja rekodi
katika malengo kama ilivyotokea hivi karibuni ilipotangaza
kuvuka malengo katika zoezi la uuzwaji wa hisa zake kwa kuuza hisa
milioni 36.6, ikiwa ni zaidi ya malengo ya awali ya kuuza hisa milioni
33.9 na kufanikiwa kukusanya sh. Bilioni 9.7 sawa na asilimia 108.99 ya
matarajio ya awali ya kukusanya shilingi Bilioni 8.9.
“Tunafurahi
kuwaambia kuwa lengo letu limetimia, kampeni imeisha lakini bidhaa ya DCB Lamba
Kwanza itaendelea, hivyo wale wateja ambao bado hawajafungua akaunti hii bado
ipo na wanaweza kuwahi katika matawi yetu kuanza kuwekeza na ‘KULAMBA’ riba.
Ikumbukwe Kuwa
Benki ya Biashara
ya DCB ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa kama Benki ya Jumuiya ya Wananchi
“community bank” na Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kufuatia kilio cha wakazi
wengi wa Jiji kutokuwa na njia rahisi ya kupata mitaji midogo midogo ya
biashara.
Benki ya DCB
imekuwa ni benki ya kwanza kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa mwaka 2008, na
imeweza kukuza mtandao wake wa matawi kufikia matawi nane likiwepo tawi la
Dodoma, na inatarajia kuongeza matawi mengine mikoani katika miaka ya mbeleni.
Uboreshaji huduma
na mahusiano ya wateja umekuwa ndio kigezo kikuu katika kuongeza amana nafuu na
za muda mrefu hasa kutoka kwa wanahisa waanzilishi na mashirika mbalimbali
yaliyoendelea kuwekeza na benki ya DCB.
Idadi ya wateja
imeongezeka kutoka 144,475 mwaka 2017 kufikia 195,611 Agasti 2019 na hivyo
kuchangia ongezeko kubwa la miamala ya kibenki.
Benki ya DCB
imefungua mtandao wa mawakala na huduma za kijiditali hadi kufikia 1000 nchi
nzima.
No comments:
Post a Comment