BENKI YA KCB TANZANIA YADHAMINI LIGI KUU YA SOKA TANZANIA BARA 2019/20

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Nd. Cosmas Kimario (kushoto), akikabidhi hundi ya shilingi milioni 500 kwa Rais wa TFF, Nd. Wallace Karia, kwa ajili ya udhamini wa Ligi kuu Tanzania Bara. KCB imeendeleza udhamini wa ligi hiyo kwa msimu wa 2019/20 ikiwa msimu wa tatu mfululizo. Wanaoshuhudia, (watatu kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, Nd. John Ulanga, (Mkuu wa Idara ya Masoko wa Benki hiyo Bi. Christine Manyeye na Mwanasheria Mkuu waBenki ya KCB, Bi. Anthonia Kilama hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Nd. Cosmas Kimario (wa tatu kushoto), Pamoja na Rais wa TFF, Nd. Wallace Karia, wakionyesha hundi ya shilingi milioni 500 iliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya udhamini wa Ligi kuu Tanzania Bara. Benki ya KCB imeendeleza udhamini wa ligi hiyo kwa msimu wa 2019/20 ikiwa msimu wa tatu mfululizo. (watatu kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi Benki ya KCB Tanzania, Nd. John Ulanga,  wengine ni viongozi kutoka TFF na KCB.

Benki ya KCB Tanzania imengia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara  kwa msimu wa 2019/2020. Mkataba huo wenye thamani ya shilingi  za Kitanzania 420,000,000 kabla ya kodi, ulitiwa saini leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Nd. Cosmas Kimario na Rais wa TFF Nd. Wallace Karia katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Benki ya KCB Tanzania ilidhamini ligi hiyo kwa mara ya kwanza msimu wa 2017/18 kwa thamani ya shilingi za Kitanzania 325,000,000 na kuongeza udhamini kwa msimu wa 2018/19 kufikia shilingi za Kitanzania 420,000,000. Mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa udhamini wa misimu iliyopita ndiyo yameivutia Benki ya KCB Tanzania kuendeleza udhamini huo kwa kiasi cha shilingi za Kitanzania 420,000,000 kupelekea jumla ya udhamini ndani misimu mitatu kuwa shilingi za Kitanzania 1.165bn.

Hafla ya kutia saini makubaliano hayo imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, Nd. John Ulanga, Katibu Mkuu TFF, Nd. Kidao Wilfred, Mwenyekiti wa bodi ya Ligi Kuu, Nd. Steven Mnguto na Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Nd. Boniface Wambura, Pamoja na Wakurugenzi wa Bodi na wafanyakazi Benki ya KCB Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Nd. Cosmas Kimario alisema kwamba pamoja na dhamira ya benki hiyo kurudisha kwa jamii, udhamini huo pia ni fursa kubwa kwa Benki ya KCB kuwekeza kwenye sekta yenye kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa kukuza ajira na vipaji vya vijana wa Kitanzania.

Zaidi ya kutengeneza ajira kwenye soka, Benki hiyo imewekeza kwenye programu ya KCB 2jiajiri ambayo hadi sasa imetoa mafunzo ya uweledi wa biashara kwa wanawake 256 na vijana 100 kuanzia mwezi Oktoba. “Matarajio ya benki yetu ni kuona Watanzania wengi zaidi wanapata ajira kupitia sekta mbali mbali tunazozigusa.” Alisema Nd. Kimario.

“Sisi Benki ya KCB, mbali na biashara tunatimiza  wajibu wetu katika jamii inayotuzunguka kwa kuiunga mkono serikali yetu kupinga umasikini nchini. Hivyo pia tunasaidia jamii hitaji kupitia sekta za: elimu, afya, mazingira, wajasiriamali, watoto waishio katika mazingira magumu.” Aliongeza Nd. Kimario.

Rais wa TFF, Nd. Wallace Karia aliishukuru Benki ya KCB Tanzania kwa kuidhamini Ligi kuu Tanzania Bara jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu 2019/20. Pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages