Wakazi wa Morogoro wafurika Shika Ndinga ya EFM, wengi wajiunga na akunti ya Fasta ya NBC

Mkuu wa Kitengo cha Uhai wa Wateja wa Benki ya NBC, Gaudence Shawa  akizungumza na wakazi wa Morogoro waliofika katika Viwanja vya Kndege kushuhudia mashindano ya kutafuta washiriki wa fainali za shindano la Shika Ndinga linaloandaliwa na Kituo cha Redio cha EFM chini ya udhamini mkubwa wa NBC.
Mmoja wa washindi wa Kampeni ya Shika Ndinga Mkoa wa Morogoro, Jumanne Mwakapolo akiwasha pikipiki yake aliyojishindia muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhai wa Wateja wa Benki ya NBC, Gaudence Shawa (kushoto kwake), katika hafla iliyofanyika mkoani Morogoro juzi. Kushoto kwa Shawa ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo ambao ni wadhamini wakuu wa kampeni hiyo.
Mmoja wa waratibu wa shindano la Shika Ndinga, Dennis Ssebo (katikati), akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Uhai wa Wateja wa Benki ya NBC, Gaudence Shawa wakati wa shindano hilo mjini Morogoro. Kushoto ni Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo.
Mkazi wa Morogoro akifunguliwa akaunti ya Fasta ya NBC wakati wa shindano la Shika Ndinga mjini Morogoro. Mteja wa akaunti ya Fasta ya NBC hupewa kadi aina ya Visa muda huo huo anaofungua akaunti kwa kiasi cha kuanzia shs 5,000/-
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages