NBC kuendeleza udhamini wake kwa wanafunzi wa vyuo vikuu

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) akizungumza na baadhi ya wanafunzi 63 wa vyuo vikuu wanaosoma kwa kupitia Mpango wa Ufadhili wa NBC wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana wa taasisi ya Elevate Education ya Afrika Kusini kuwaandaa kimasomo na katika stadi nyingine za kielimu na kimaisha jijini Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Neema Singo (kushoto) akizungumza na baadhi ya wanafunzi 63 wa vyuo vikuu wanaosoma kwa kupitia Mpango wa Ufadhili wa NBC wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na benki hiyo kwa kusirikiana na taasisi ya Elevate Education ya Afrika Kusini jijini Dar es Salaam leo.

Mtoa Mada kutoka taasisi ya Elevate Education, Yolisa Motha (kulia),  akizungumza na wanafunzi hao jijini Dar es Salaam leo.

Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter (kushoto), akizungumza katika mafunzo hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi, Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe (katikati), wakmisikiliza mkufunzi kutoka taasisi ya Elevate ya Afrika Kusini kabla ya kuanza mafunzo hayo yaliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wanaosoma kwa ufadhili wa NBC.

Baadhi ya wanafunzi wanaosoma kwa ufadhili wa Benki ya NBC wakiwa katika mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na NBC kwa kushirikiana na taasisi ya Elevate Education ya Afrika Kusini katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages