TANZANIA COMMERCIA BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI UKUTA WA CHUO CHA TIBA MTWARA
MAENDELEO BANK PLC YAJIVUNIA KUWEKA REKODI MPYA YA MAFANIKIO
Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Biashara wa Maendeleo Bank, Emmanuel Mwaya akizungumza wanahabari pamoja na maofisa wa benki hiyo wakati akitangaza rekodi mpya ya mafanikio kuwa ni benki yenye faida kwa miaka nane mfululizo.hafla yakutangaza faida hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa wakiwa Maendeleo Bank wakifuatilia kwa umakini rekodi mpya ya mafanikio kuwa ni benki yenye faida kwa miaka nane mfululizo.hafla yakutangaza faida hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyi jijini Dar es Salaam.Maendeleo Bank yaweka rekodi mpya ya mafanikio faida ya mwaka 2022 ni shilingi Bilioni 1.984 ambalo ni ongezeko la mara mbili Zaidi.
Akiungumza wakati akitangaza rekodi hiyo mpya Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Biashara wa Maendeleo Bank, Emmanuel Mwaya alieleza kuwa Maendeleo Bank Plc imeendelea kuwa benki yenye faida kwa miaka 8 mfululizo, kwa mujibu wa taarifa za fedha zilizokaguliwa za mwaka 2022, ikiwa na mambo yafuatayo;
Ameeleza kuwa “Faida kabla ya kodi: TZS 1.984 bilioni, ukuaji wa mwaka 181%
Faida baada ya kodi: TZS 1.415 bilioni, ukuaji wa mwaka wa 141%
Jumla ya amapato: TZS 12. bilioni, ukuaji wa mwaka wa 5%
Amana: TZS 72.0 bilioni ukuaji wa 11%
Mikopo: TZS 61.0 bilioni ukuaji wa 5%
Ukuaji mzuri wa faida hizi umechangiwa Zaidi na timu iliyojitolea na ikiwa na lengo la kuifanya benki kuwa moja wapo ya wadau muhimu wa sekta ya kifedha katika uchumi. Ningependa kuangazia baadhi ya vichochezi vya faida ambavyo ni pamoja na; ukuaji wa jumla ya mapato kwa asilimia 26 mwaka hadi mwaka kutoka TZS 14.23 bilioni hadi TZS 17.97 bilioni mwaka 2022.
Benki pia imeendelea kuonyesha ufanisi mkubwa wa utendaji kazi, huku uwiano wa gharama kwa mapato ikiongezeka hadi 58% kutoka 74% katika kipindi kama hicho mwaka jana,ukiwa na nia ya kufikia kiwango elekezi kutoka benki kuu cha 55% ifikapo juni 2023.
Amana za wateja ziliongezeka kwa 11% kutoka TZS 70 bilioni mwaka 2021 hadi TZS 77.8 bilioni mwaka 2022 wakati mikopo ilongezeka kwa asilimia 5 kutoka TZS 57.7 bilioni hadi hadi TZS 60.6 bilioni mwaka 2022.
Mbinu iliyotumika katika uhamasishaji na ukuaji wa amana kwa wateja ulichangiwa kwa kiasi kikubwa uboreshaji wahuduma na bidhaa bunifu ambazo benki imekuwa ikitoa. Kuongezeka kwa bidhaa za kidijitali kama vile huduma za kibenki kwa simu, huduma za uwakala ambapo Zaidi ya benki mawakala 1300 (maendeleo Bank Wakala) Zimechangia ukuaji huu unaoshuhudiwa leo hii.
Akihitimisha wakati akitoa matokeo ya mwaka mzima ya benki hiyo mkuu wakitengo cha biashara Emmanuel Mwaya alisema”ninajivunia sana na ninashukuru kwa mafanikio yetu kama timu, nab ado nina Imani kubwa kwa ya utekelezaji wa mkakati wetu, kuongezeka kwa mahusiano ya wateja wetu, ari ya utendaji wa wafanyakazi, na uongozi thabiti tutadumisha kasi hii ya ukuaji wa biashara yetu kuu.
TANZANIA COMMERCIAL BANK YAFUTURISHA WATEJA WAKE JIJINI DAR ES SALAAM
Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi (watatu kushoto), wakiwaongoza wateja wa pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo kupata mlo wa futari uliyoandaliwa na Tanzania Commercia Bank kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium tower
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi (kushoto), akiongozana pamoja na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar na viongozi mbalimbali wa kidiniwa mkoa wa Dar es Salaam wakati wa hafla yakushiriki mlo wa futari uliyoandaliwa na Tanzania Commercia Bank kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium tower
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa hafla yakushiriki mlo wa futari uliyoandaliwa na TCB kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium tower
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar akitoa neno la shukrani kwa Mkurungenzi Mtendaji waTanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, kwakujali na kuona umuhimu wa mfungo wa Ramadani na kuandaa mlo wa futari kwaajili ya wateja wake wa Dar es Salaam.hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la milenium tower.
Maofisa wa Tanzania Commercial Bank (TCB) pamoja na wateja wa benki hiyo wakishiriki mlo huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank TCB, Bi Chichi Banda (kushoto), akiwa kwenye picha ya pozi na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Benki hiyo Bi Gloria Mutta wakati wa hafla yakupata mlo wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo ambapo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally
TCB YATOA MSAADA WA MADAWATI MKOANI TABORA


TANZANIA COMMERCIAL BANK YAWAPUNGUZIA MWENDO WAKAZI WA BUTIAMA
Meneja wa Tanzania commercial Bank (TCB), Tawi la Musoma Hagai Gilbert (kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa mabati 135 yaliyotolewa na Benki hiyo kwa Diwani wa kata ya Kyanyari kijiji cha Nyamikoma wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara, Mkingi Itagata, kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nyamikoma wilayani humo.
Maofisa wa Tanzania Commercial Bank wakiongozwa na Meneja Benki hiyo tawi la Musoma Hagai Gilbert pamoja na uongozi wa kijiji cha Nyamikoma wakikagua ujenzi wa kituo cha Afya kinachojengwa kwa nguvu za wananchi ambapo TCB imeguswana kuchangia kwa kutoa msaada wa mabati 135 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huo
Wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Butiama wakisaidia kushusha mabati 135 yaliyotolewa na Tanzania Commercial Bank (TCB) kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa zahanati.
Tanzania commercial bank imekabidhi mabati 135 katika kijiji cha Nyamkoma kilichopo wilaya ya Butiama mkoani Mara kwa dhamira ya kuunga mkono juhudi za serikali katika juhudi zake za kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma ya afya.
Msaada huo ulitolewa leo katika kijiji cha Nyamkoma kilichopo wilaya ya Butihama mkoani mara na kupokelewa na Diwani wa kata ya kinyare Mh. Mkingi Itagata.
Pamoja ya kuishukuru Benki ya TCB wakati akipokea msaada huo, Diwani wa kata ya Kinyare Mh Mkingi Itagata amesema kuwa bado kuna uhitaji ili ujamilisha ujenzi wa kituo cha afya kwani gharama ya ujenzi ni milioni 150 lakini hadi sasa kiasi walichokusanya ni milioni 47.
“Serikali pamoja na wazazi tutaongeza nguvu kwenye ujenzi huu maana wananchi wamekuwa wakifuata huduma ya afya mbali kidogo na kijijini hapo.” Amesema Mingi
Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa Benki ya TCB Tawi la Musoma Gilbert Hagai aliwasihi wananchi wa kijiji hicho kuwa TCB itaendelea kuunga mkono juhudi za wananchi wapenda maendeleo na kuhakikisha kuwa benki hiyo inasogea huduma zake karibu.
Aidha pia amewapongeza wazazi na uongozi wa kijiji kwa jitihada zao za kuchangia na kuanza ujenzi wa zahanati hiyo toka mwaka 2017 hii inaonesha kuwa ni kwa namna gani kumekuwa na uhitaji.
“Benki yetu ya Tanzania Commercial Bank ni mdau mkubwa wa Maendeleo, kwa kawaida kila mwaka tunatenga fungu kutoka katika faida yetu kwa ajili ya kurudisha katika jamii na tunaipa kipaumbele kwani Kuwekeza kwenye Elimu, Afya na maeneo mbalimbali tukiwa kama benki tunaamini vitu hivi vyote vinatusiaida kupata wateja na wafanyakazi wa benki yetu wa baadaye.
Tutaendelea kuchangia na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassani katika kuboresha sekta ya afya kwa kadri tunavyoweza na tunaahidi kwamba huu si mwisho.” Ameongeza gilbert.
TANZANIA COMMERCIAL BANK YAWAFIKIA WANAWAKE WENYE UHITAJI HOSPITAL YA OCEAN ROAD WAKISHEREHEKEA SIKUKUU YA WANAWAKE DUNIANI

Meneja Mawasiliano na Uhusiano Tanzanian Commercial bank (TCB), Gloria Mutta (watatu kulia) akikabidhi misaada wa vitu mbalimbali kwa Afisa Ustawi wa jamii wa Hospitali ya Ocean Road Cancer Institute (ORCI) Devotha Kibanga Kwaajili ya kusaidia wagonjwa wanawake wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya Ocean road jijini Dar es Salaam Ukiwa ni kusherehekea siku kuu ya wanawake inayofanyika kila tarehe 8 ya mwezi wa tatu kila mwaka wengine pichani ni wafanyakazi ya hospital hiyo Hafla hiyo imefanyika jana.
Katika kusherehekea sikukuu ya mwanamke duniani, Tanzania Commercial Bank (TCB) imeendelea kuwa karibu na wateja wake katika kuzingatia usawa wa kijinsia kwa maisha endelevu.
Tanzania Commercial Bank (TCB) imetumia sikukuu hiyo kuwakumbuka na kuwatembelea wagonjwa wanawake wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya Ocen Road na kutoa misaada mbalimbali.
Akizungumza wakati alipotembelea wagonjwa hao Meneja mawasiliano na uhusiano wa Benki hiyo Bi. Gloria Mutta ameeleza kuwa "Tanzania Commercial Bank(TCB) imeendelea kuwa karibu na jamii kwa kutoa misaada mbalimbali hususani kwa wenye mahitaji maalum".
Ameeleza kuwa " Tanzania Commercial Bank (TCB) imetambua mchango wa mwanamke katika kuleta maendeleo"
Aliwahamasisha wanawake hao kuendelea kuiamini na kuitumia Benki hiyo kwani tumekuwa tukitoa misaada mbalimbali pale tunapohitajika.
mutta aliongeza kuwa benki ya TCB inatoa huduma nchi nzima ina matawi ambayo yanafanya kazi masaa 24 yote hayo ni kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma muda wowote.
Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii Ocean Road Cancer Institute (ORCI) Devotha Kibanga ameishukuru benki hiyo na kusema kuwa imekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada kwa jamii inayotuzunguka hususani sekta ya afya
MKURUGENZI WA WIKICHA AFUNGUKA KUHUSU UVUNJAJI WA BAA
Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Wikicha Estate Development Agency inayosimamia na kumiliki shughuli zote zinazofanywa kwenye kiwanja namba 48766 kilichopo Ukonga eneo la Banana jiini Dar es Salaam mzee Wilson Kiguha Chacha afunguka kuwa vijana wake hawakuhusika na uvunjaji wa baa ya Big Mountein.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini kwake Banana Ukonga jijini Dar es Salaam Chacha amesema anasikitishwa na kitendo cha mmiliki wa baa hiyo aliyekuwa mpangaji wa sehemu ndani ya kiwanja hicho kukamata vijana wake kwa madai kuwa walihusika kuvunja baa hiyo.
“Mimi nilikuwa Marekani kwa matibabu nikapata taarifa kuwa baa hiyo imevunjwa na aliyevunja ni mmiliki mwenyewe ili asilipe kodi yangu niliyokuwa na mdai kwa kipindi kirefu na tayari mahakama ya Ardhi ilimwamuru aondoke mara moja katika eneo hilo,”amesema Chacha.
Ameongeza kuwa “Hukumu ya Mahakama hiyo iliyotolewa Desemba 19, 2022 ilimtaka mpangaji huyo wa baa ya Big Mountein aondoke na alipe malimbikizo yote ya kodi ya pango aliyokuwa anadaiwa na kampuni yangu ya Wikicha”.
Chacha amesema mpangaji huyo ameleta usumbufu mkubwa kwa vijana wake kwani sasa kazi hazifanyiki wanashinda kituo cha polisi kuripoti kila siku, ndipo alipoamua kurudi Tanzania kutoka Marekani alikokuwa anapatiwa matibabu ingawa bado hajapona vizuri ili kushughurikia suala hilo.
“Nimerudi nchini ingawa hali yangu ya kiafya haijaimalika ili kushungulikia jambo hili la uonevu wanalofanyiwa vijana wangu la kukamatwa hovyo na mpangaji wangu kwa taarifa za uongongo kwa lengu la kukwepa kulipa malimbikizo ya kodi ninayomdai.
“Vijana wangu hawajahusika katika uvunjaji wa baa hiyo kama inavyoelezwa na kwamba mwezi Desemba wafanyakazi wangu wote niliwapa likizo na hata huyo Godfrey Chacha anayedaiwa kutokomea kusiko julikana naye alikuwa likizo, kwa sasa kampuni imempangia majukumu mengine nje ya Dar es Salaam wala hajajificha, Polisi wakimhitaji nitamleta mara moja.”
Amesema mmiliki wa baa ya Big Mountain anaeneza taarifa za uongo ndiyo maana hadi sasa jeshi la polisi limeshindwa kupeleka kesi Mahakamani kwani hakuna ushahidi wa jambo hilo, hivyo vijana wake wanaonewa kuwekwa ndani mara kwa mara.
Mzee Wilson Chacha amewataja vijana wake waliokamatwa na Polisi kuwa ni Joseph Nyagare, Michael Julius Chacha, Amosi Chacha na Elizabeth Kiguha.
Alipotafutwa mmiliki wa baa ya Big Mountain ambaye alielekeza atafutwe wakili wake, na alipotafutwa wakili wake Frenk Chundu amesema wao wanasubili maamuzi ya jeshi la polisi kupeleka kesi Mahakamani kwani mteja wangu hawezi kujihujumu mwenyewe kwakuwa alifanya uwekezaji wa fedha nyingi kwenye biashara hiyo.
“Uwekezaji uliofanywa na mteja wangu ulikuwa ni wazaidi ya shilingi milioni 100, hivyo si kweli kwamba kavunja yeye tusubili vyombo vya sheria vifanye kazi yake,”amesema Wakili Frenk Chundu.


















