TANZANIA COMMERCIAL BANK YAWAPUNGUZIA MWENDO WAKAZI WA BUTIAMA

  Meneja wa Tanzania commercial Bank (TCB), Tawi la Musoma Hagai Gilbert (kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa mabati 135 yaliyotolewa na Benki hiyo kwa Diwani wa kata ya Kyanyari kijiji cha Nyamikoma wilaya ya Butiama  Mkoa wa Mara, Mkingi Itagata, kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nyamikoma wilayani humo.


Maofisa wa Tanzania Commercial Bank wakiongozwa na Meneja Benki hiyo tawi la Musoma Hagai Gilbert pamoja na uongozi wa kijiji cha Nyamikoma wakikagua ujenzi wa kituo cha Afya kinachojengwa kwa nguvu za wananchi ambapo TCB imeguswana kuchangia kwa kutoa msaada wa mabati 135 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huo


Wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Butiama wakisaidia kushusha mabati 135 yaliyotolewa na Tanzania Commercial Bank (TCB) kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa zahanati.



Tanzania commercial bank imekabidhi mabati 135 katika kijiji cha Nyamkoma kilichopo wilaya ya Butiama mkoani Mara kwa dhamira ya kuunga mkono juhudi za serikali katika juhudi zake za kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma ya afya.

Msaada huo ulitolewa leo katika kijiji cha Nyamkoma kilichopo wilaya ya Butihama mkoani mara na kupokelewa na Diwani wa kata ya kinyare Mh. Mkingi Itagata. 



Pamoja ya kuishukuru Benki ya TCB wakati akipokea msaada huo, Diwani wa kata ya Kinyare Mh Mkingi Itagata amesema kuwa bado kuna uhitaji ili ujamilisha ujenzi wa kituo cha afya kwani gharama ya ujenzi ni milioni 150 lakini hadi sasa kiasi walichokusanya ni milioni 47.



“Serikali pamoja na wazazi tutaongeza nguvu kwenye ujenzi  huu maana wananchi wamekuwa wakifuata huduma ya afya mbali kidogo na kijijini hapo.” Amesema Mingi


Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa Benki ya TCB Tawi la Musoma Gilbert Hagai   aliwasihi wananchi wa kijiji hicho kuwa TCB itaendelea kuunga mkono juhudi za wananchi wapenda maendeleo na kuhakikisha kuwa benki hiyo inasogea huduma zake karibu.


Aidha  pia amewapongeza wazazi na uongozi wa kijiji kwa jitihada zao za kuchangia na kuanza ujenzi wa zahanati hiyo toka mwaka 2017 hii inaonesha kuwa ni kwa namna gani kumekuwa na uhitaji.


“Benki yetu ya Tanzania Commercial Bank ni mdau mkubwa wa  Maendeleo, kwa kawaida kila mwaka tunatenga fungu kutoka katika faida yetu kwa ajili ya kurudisha katika jamii na tunaipa kipaumbele kwani Kuwekeza kwenye Elimu, Afya  na maeneo mbalimbali tukiwa kama benki tunaamini vitu hivi vyote vinatusiaida kupata wateja na wafanyakazi wa benki yetu wa baadaye.


 Tutaendelea kuchangia na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassani katika kuboresha sekta ya afya kwa kadri tunavyoweza na tunaahidi kwamba huu si mwisho.” Ameongeza gilbert.

Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages