Benki ya Absa Tanzania Yashinda Tuzo 11 za Heshima Mwaka 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kushoto), akizungumza na waandishi wakati akitangaza mafanikio ya benki kwa Mwaka 2024 kupitia Tuzo mbalimbali 11 ilizopata. Pamoja naye ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga.

• Kutambuliwa kwake kunadhihirisha, Ufanisi katika Ubunifu wa Kifedha, Uongozi na kujali Wateja.

Benki ya Absa Tanzania inajivunia kutangaza mafanikio yake makubwa ya kushinda tuzo 11 za heshima mwaka 2024. Tuzo hizi zinatambua mchango mkubwa wa benki katika uwezeshaji wa kifedha, uvumbuzi, utawala bora, na huduma kwa wateja.

Tuzo muhimu ambazo benki imeshinda mwaka huu ni pamoja na:

• Chapa ya Benki Inayokua Haraka Zaidi 2024, iliyotolewa na World Brand Magazine.

• Benki ya Wateja rejareja na Wateja Wadogo na wa Kati inayokua haraka zaidi Tanzania 2024 zilizotolewa na World Economic Magazine Awards.

• Benki inayofanya vizuri zaidi katika kuwawezesha wanawake kupata huduma za kifedha Tanzania, iliyotolewa na Tanzania Women Industrial Awards.

• MD/CEO Bora wa Mwaka, iliyotolewa na Top 100 Executive List Awards.

• Hatifungani Bora ya Mwaka, iliyotolewa na Soko la Hisa la Dar es Salaam.

• Muwasilishaji Bora wa Ripoti ya Taarifa za Fedha 2023, iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)

• Mwajiri Bora anayeinukia na Mwajiri Bora katika Usimamizi na Maendeleo ya Vipaji, zilizotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

• Benki inayotoa Huduma Rafiki na Utulivu za Mikopo Tanzania, iliyotolewa na Consumer Choice Awards Afrika 2024.

• Benki inayopendwa zaidi na kufikika zaidi Kusini mwa Afrika, iliyotolewa na Consumer Choice Awards Afrika 2024.

Utendaji bora wa Benki ya Absa Tanzania mwaka 2024 umeoneshwa kupitia matokeo yake mazuri ya kifedha kwa nusu ya kwanza ya mwaka. Mapato ya jumla yaliongezeka kwa 25% kufikia TZS bilioni 105, huku faida kabla ya kodi ikipanda kwa 65% kufikia TZS bilioni 54. Amana za wateja ziliongezeka kwa 21%, zikionesha uimara wa benki hiyo na uwezo wake wa kutoa ukuaji endelevu.

Tuzo ya Chapa ya Benki Inayokua haraka zaidi inaadhimisha maendeleo makubwa ya Benki ya Absa Tanzania tangu ilipoanzishwa mwaka 2020. Ndani ya miaka minne tu, Absa imepata kiwango sawa cha imani na kutambuliwa kama benki za ndani na kimataifa zenye karibu karne moja ya historia nchini Tanzania. Tuzo hii inaonyesha ahadi ya chapa ya Absa: 'Stori yako ina Thamani', inadhihirisha kujitolea kwa benki hiyo katika kuthamini Stori za kipekee za wateja wake, kuunda suluhisho za kibunifu, na kuiwezesha jamii.

Tuzo ya Benki inayofanya vizuri zaidi katika kuwawezesha wanawake kupata huduma za kifedha inaonyesha dhamira ya Absa katika kukuza ujumuishi wa kifedha. Kupitia bidhaa kama Akaunti ya Absa She Business, benki hiyo imewawezesha wanawake wajasiriamali kupata huduma za kibenki bila gharama, msaada wa ushauri, na programu za kujenga uwezo.

Katika sekta ya SME, suluhisho maalum za Absa na ushirikiano wa kimkakati zimesaidia benki kushinda tuzo ya Benki inayotoa huduma Kwa wateja wadogo na wa Kati (SME) inayokua haraka zaidi Tanzania 2024.

Tuzo ya Benki ya Wateja Rejareja inayokua haraka zaidi Tanzania 2024 inaonyesha msisitizo wa benki hiyo katika mabadiliko ya kidijitali na urahisi wa wateja, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa huduma za uwakala na suluhisho za kibunifu kama jukwaa la malipo la Mobi Tap.

Kutambuliwa kwa Mkurugenzi Mtendaji kama MD/CEO wa Mwaka na tuzo ya Ripoti Bora za Kifedha 2023 kunathibitisha kujitolea kwa Absa kwa utawala bora, uwazi, na uongozi wa mfano wa kuigwa.

Tuzo kutoka Consumer Choice Awards, kama Benki Inayotoa Huduma Rafiki na Utulivu wa Mikopo Tanzania, zinaonyesha dhamira ya Absa ya kuwapa wateja nafasi ya kwanza katika shughuli zake.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Obedi Laiser, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, alisema: "Tuzo hizi ni ushahidi wa nguvu ya ushirikiano wetu na wateja na wadau wetu. Tunaheshimika kutambuliwa katika nyanja nyingi, na tutaendelea kujitolea kuimarisha Afrika ya Kesho kupitia suluhisho za kibenki zenye ubunifu, ujumuishi, na athari chanya.”

Benki ya Absa Tanzania inapoendelea na safari yake ya ukuaji na mabadiliko, inabaki imara katika dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwawezesha jamii. Tuzo hizi ni kielelezo cha kujitolea kwa benki hiyo kwa uvumbuzi, uwazi, na kuridhisha wateja wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kushoto), akionesha Moja ya tuzo waliyoshinda wakati akizungumza na waandishi wa habari kutangaza mafanikio ya benki kwa Mwaka 2024 kupitia tuzo mbalimbali 11 walizipata. Pamoja naye ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa tatu kushoto), pamoja na baadhi ya maofisa wa ngazi za juu wa benki hiyo, wakionesha kwa waandishi wa habari, tuzo mbalimbali 11 ambazo benki hiyo imeshinda kwa mwaka 2024, alipokutana nao, jijini Dar es Salaam jana.
Share:

Benki ya Absa Tanzania yang'ara tuzo za Chaguo la Walaji

       

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) akikabidhi tuzo ya Benki Bora kwa kutoa Huduma Bora rafiki za Mikopo nchini Tanzania kwa Mkurugenzi wa Sheria na Udhibiti wa Sera na Kanuni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Sengati Giattas, wakati wa hafla ya kila mwaka ya utoaji wa Tuzo za Chaguo la Walaji, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) akikabidhi tuzo ya Benki Bora inayopendwa Zaidi na inayofikika zaidi Kusini mwa Afrika kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser wakati wa hafla ya kila mwaka ya utoaji wa Tuzo za Chaguo la Walaji, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa pili kushoto) akionesha tuzo ya Benki Bora inayopendwa zaidi na inayofikika zaidi Kusini mwa Afrika wakati wa hafla ya kila mwaka ya utoaji wa Tuzo za Chaguo la Walaji, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser na Mkurugenzi wa Sheria na Udhibiti wa Sera na Kanuni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Sengati Giattas (katikati), wakionesha tuzo za Benki Bora kwa kutoa Huduma Bora rafiki za Mikopo nchini Tanzania na Benki Bora inayopendwa zaidi na inayofikika zaidi Kusini mwa Afrika, mara baada ya kukabidhiwa, wakati wa hafla ya kila mwaka ya Tuzo za Chaguo la Walaji, jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Share:

Benki ya Absa Tanzania yashinda tuzo ya uandaaji bora wa taarifa za fedha

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Fedha, CPA. Benjamin Mashauri (wa pili kulia), akikabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza wa Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati kwa Mwaka 2023 zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Muhsin Kaye katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA Prof. Sylvia Temu na Mkurugenzi Mtendaji NBAA, CPA. Pius Maneno.

BENKI ya Absa Tanzania imeibuka kidedea kwa kuibuka na ushindi wa kwanza wa Uandaaji Bora wa Taarifa za Fedha kwa Mwaka 2023 katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati wa tuzo za kila mwaka zinazoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Tuzo za mwaka 2023 zilishuhudia mchuano mkali ukihusisha washiriki 86 kutoka katika vitengo tofauti waliokidhi vigezo vilivyowekwa na NBAA ambapo washindi wake walikabidhiwa tuzo za na mgeni rasmi, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Fedha, CPA. Benjamin Mashauri.

Akizungumza muda mfupi baada ya kupokea tuzo hiyo, Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Muhsin Kaye alisema ushindi huo unaonesha ni kwa jinsi gani benki yao imebobea na kuwa na uzoefu, pamoja na watu wenye ujuzi wa kutosha katika uandaaji wa taarifa hizo.

“Ushindi huu ni ishara ya uwajibikaji sisi kama benki lakini pia uadilifu na uwazi katika uwasilishaji wa taarifa zetu, natoa ahadi kwa wateja wetu na kwa watanzania kuwa tutaendelea kujitahidi kuandaa taarifa sambamba na vigezo na kanuzi zinazohitajika na ni fahari kwetu sisi benki lakini ni fahari pia kwa wateja wetu wote.

“Ningependa kuishukuru Bodi ya NBAA kwa kuweka chachu ya uandaaji wa taarifa za kifedha kwa kuzingatia vigezo vilivyo sahihi kabisa, sisi kama benki tumefarijika kupata tuzo hii ikiwa ni muendelezo kwani tumeshapata tuzo hii miaka kadhaa iliyopita”, alisema Bw. Kaye.

Pamoja na hayo alisema, ushindi huo unaenda sambamba na lengo kuu la benki hiyo ambalo ni Kuiwezesha Afrika na Tanzania ya Kesho Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, huku ikitiwa nguvu na ahadi ya chapa isemayo, ‘Story yako Ina Thamani.

“Sisi kama Absa Tanzania tunaamini ushindi huu utaendelea kuongeza ari na hamasa zaidi kwa benki yetu kufanya vizuri zaidi katika kuziwesha Story za mafanikio ya wateja wetu na watanzania kwa ujumla”, alisema Bw. Kaye
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA. Pius Maneno (wa pili kushoto) akimpongeza Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Muhsin Kaye, mara baada ya benki hiyo kutangazwa mshindi wa kwanza kwanza wa Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati kwa Mwaka 2023 zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA Prof. Sylvia Temu na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Fedha, CPA. Benjamin Mashauri.
Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Muhsin Kaye (kulia), akipozi kwa picha ya kumbukumbu na pamoja na wawakilishi wa taasisi zilizoibuka na ushindi wa kwanza katika vitengo mbalimbali wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa tuzo a Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha zinazoandaiwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), jijini Dar es Salaam jana. Wengine katika picha ni mgei rasmi, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Fedha, CPA. Benjamin Mashauri, Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA Prof. Sylvia Temu na Mkurugenzi Mtendaji NBAA, CPA. Pius Maneno.
Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Bernard Tesha (wa pili kushoto ), Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi, Bw. Heristraton Genesis (kushoto), Mdhibiti wa Masuala ya Fedha, Muhsini Kaye na Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi, wakionesha tuzo ya Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati kwa Mwaka 2023 zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), muda mfupi baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam jana.
Share:

Absa Bank Tanzania yakabidhi Subaru Forester ya kwanza, huku ikichezesha droo ya mshindi wa pili ya Kampeni ya 'Spend & Win'

Mshindi wa kwanza wa kampeni ya Tumia na Ushinde 'Spend & Win' ya Benki ya Absa Tanzania, Bw. Rashidi Saidi (kulia) akionesha ufunguo wa gari jipya aina ya Subaru Forester 2024, muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Obedi Laiser (katikati), katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kampeni hii inalenga kuwahamasisha watanzania wengi zaidi kutumia suluhisho za kibenki za kidijitali, kama vile kadi za ATM, na kadi za mkopo, zinazotoa usalama, urahisi, ili kupata huduma mbalimbali za kibenki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa tatu kushoto), akizungumza, wakati wa hafla ya droo ya pili na kukabidhi gari jipya aina ya Subaru Forester 2024 kwa mshindi wa kwanza wa kampeni inayoendelea ya Tumia na Ushinde 'Spend & Win' Bw. Rashidi Saidi (wa tatu kutoka kulia), katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Kampeni hii inalenga kuwahamasisha Watanzania kufanya miamala ya kibenki kwa njia za kidijitali, kama vile kadi za ATM na kadi za mkopo, zinazotoa usalama, urahisi, na upatikanaji wa huduma mbalimbali za kibenki.
Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Heristraton Genesis (wa pili kushoto), akizungumza, wakati wa hafla ya kukabidhi gari jipya kabisa aina ya Subaru Forester 2024 kwa mshindi wa kwanza wa kampeni inayoendelea ya Tumia na Ushinde 'Spend & Win' Bw. Rashidi Saidi (wa tatu kutoka kulia), katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Kampeni hii inalenga kuwahamasisha Watanzania kufanya miamala ya kibenki kwa njia za kidijitali, kama vile kadi za ATM na kadi za mkopo, zinazotoa usalama, urahisi, na upatikanaji wa huduma mbalimbali za kibenki.
Mshindi wa kwanza wa kampeni ya Tumia na Ushinde ya Benki ya Absa Absa Bank Tanzania, Bw. Rashidi Saidi (kulia) akichezesha droo ya pili ya kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Mteja wa benki hiyo, Bi. Alyshah Aminmohamed Bharwani aliibuka mshindi.
Mshindi wa Droo ya Kwanza ya Kampeni ya Tumia na Ushinde 'Spend & Win', ya Benki ya Absa Tanzania, Bw. Rashid Nassoro, akipozi kwa picha ndani ya gari lake aina ya Subaru Forester 2024 lenye thamani ya zaidi ya shs milioni 40 jijini Dar es Salaam leo baada ya kukabidhiwa rasmi.
Share:

Absa Bank Tanzania CEO Wins Top 100 Executive List Award

Zanzibar’s Minister of State in the President’s Office for Labour, Economic Affairs, and Investment, Hon. Shariff Ali Shariff, presents the 1st runner-up award in the MD/CEO of the Year category to Absa Bank Tanzania Managing Director, Mr. Obedi Laiser (second left), during a ceremony in Dar es Salaam yesterday. The event, organized by the Eastern Star Consulting Group, celebrates the outstanding achievements of Tanzania’s corporate leaders. Also pictured (from left) are Mr. Deogratius Kilawe, Project Director for the Top 100 Executive List, and Eng. Rogatus Mativila, Deputy Permanent Secretary in the President’s Office, Regional Administration and Local Government (PO-RALG).

The Managing Director of Absa Bank Tanzania, Mr. Obedi Laiser, has been named the 1st runner-up in the MD/CEO of the Year category at the prestigious Top 100 Executive List Awards. The award ceremony, held in Dar es Salaam over the weekend, was a vibrant celebration of corporate excellence.

The Top 100 Executive List Awards aim to spotlight exceptional executives from both profit and non-profit organizations, encouraging them to share their success stories and inspire others.

Organized by the Eastern Star Consulting Group, the awards recognize and celebrate individual and corporate achievements by trailblazing leaders across Tanzania’s corporate landscape.
Absa Bank Tanzania Managing Director, Mr. Obedi Laiser (center), celebrates his recognition as 1st runner-up in the MD/CEO of the Year category at the Top 100 Executive List Awards. He poses for a commemorative photo with senior officials from the bank shortly after the ceremony in Dar es Salaam.
Share:

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto) , Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian Thomas na Mkuu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Sezaria Kiwango wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kisima kilichojengwa na wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Ni mwendelezo wa wafanyakazi wa benki hiyo kufanya huduma za kijamii katika shule hiyo Kwa takriban miaka mitatu sasa. Kutoka Kushoto ni Mameneja Rasilimali Watu wa benki hiyo, Bw. Hance Mapunda na Bi. Anna Chacha.
Meneja Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Hance Mapunda (kushoto), Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto) , Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian Thomas, Mkuu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Bi. Sezaria Kiwango na Meneja Rasilimali Watu mwingine wa benki hiyo, Bi. Anna Chacha wakishangilia baada ya kuzindua kisima kilichojengwa na wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (kushoto) akikabidhi kisima kilichojengwa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Nabili Tuli jijini Dar ea Salaam jana.
Mkuu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Bi. Sezaria Kiwango (kulia), akikabidhi cheti cha shukurani kwa maofisa wa Benki ya Absa Tanzania, mara baada ya kupokea msaada wa kisima Cha maji kilichojengwa na wafanyakazi hao, katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Dar es Salaam jana.
Share:

BENKI YA DCB KUONGEZA MTAJI WA SH BILIONI 10.7

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Masoko na Uchunguzi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw. Exaut Julius (katikati), akikata utepe, kuashiria uzinduzi rasmi wa zoezi la uuzaji wa Hisa za Upendeleo za Benki ya Biashara ya DCB, jijini Dar es Salaam leo. Wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro na wa tatu kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi pamoja na wawakilishi wa taasisi nyingine waliohudhuria.

*Ni kwa kupitia uuzaji wa Hisa za Upendeleo

BENKI ya Biashara ya DCB, imezindua zoezi ya uuzaji wa Hisa za Upendeleo, ikitarajia kupata zaidi ya sh bilioni 10.7 ili kuongeza kiasi cha mtaji wake unaofikia sh bilioni 15 kwa sasa, ili pamoja na mambo mengine kukidhi vigezo vilivyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), pamoja na kuwaletea wanahisa wake na watanzania kwa ujumla tija za kiuchumi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa uuzaji wa hisa hizo jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro alisema uamuzi huo unaenda sambamba na mikakati yao ya maendeleo ya miaka mitano katika kuongeza mtaji wake kutoka ulipo sasa hadi kufikia sh bilioni 61.

“Bodi ya Wakurugenzi ya DCB iliidhinisha mpango mkakati wa miaka mitano ukijikita kwenye mambo makuu Matano; Kwanza kukuza mtaji wa benki kutoka shs bilioni 15 (2024) hadi kufikia shs bilioni 61 ifikapo mwaka 2028, pili ukusanyaji wa amana nafuu za benki kupitia wanahisa wakuu na wateja wetu, tatu kuongeza wigo wa mikopo bora itakayotolewa kwa ufanisi na umahiri, nne utaoaji wa mikopo kwa wateja wadogo wadogo na wa kati ili kuendelea kutimiza lengo la kuanzishwa kwa benki yetu na tano, kuboresha njia za utoaji huduma na kuongeza bidhaa zinazotolewa kwa njia za kijiditali."

“Tukio la leo linaenda kuandika historia ya benki na kuanza kutimiza mkakati wa kwanza wa kuongeza mtaji wa benki, hivi sasa, mtaji wa benki uko kwenye kima cha chini kilichowekwa na Benki Kuu ya Tanzania, na ili kuweza kusimama imara kama benki, ongezeko la mtaji ni muhimu sana, benki inadhamiria kufanya biashara kubwa ambapo ili kufanikisha lengo hili, kuna ulazima wa kuongeza mtaji”, alisema Bi. Zawadia.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa ili kuweza kuhakikisha mtaji wa benki unaendelea kukua mwaka hadi mwaka baada ya zoezi hili na pia kutumiza malengo ya benki, Bodi ya Wakurugenzi iliona ni muhimu kufanya mabadiliko machache ya kiutawala katika menejimenti ya benki yetu, na kumteu Ndugu Sabasaba Moshingi kama Mkurugenzi Mtendaji wa benki mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika tansia ya benki, huku mabadiliko mengine yakifanyika katika idara ya biashara, mikopo na uendeshaji na teknolojia, idara zote hizi kwa ujumla ni nguzo muhimu katika biashara ya benki.

Alisema uuzaji wa Hisa za upendelo unatarajia kuwaletea wanahisa na watanzania kwa ujumla tija za kiuchumi, baada ya kuongeza mtaji wa benki ambapo unalenga kukuza biashara na kuwapatia wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati mitaji ya kukuza biashara zao na upande mwingine umiliki wa hisa za benki ya DCB unaunga mkono juhudi zinazoendelea za serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi shupavu wa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwaletea watu wake maendeleo.

“Bodi ya DCB pamoja na Menejimenti ya benki ilipendekeza na kuidhinisha uuzaji wa Hisa za Upendeleo 97,646,913 zenye thamani ya shs 10,741,160,430 kwa bei ya punguzo ya shs 110 kwa kila hisa moja, kinyume na shs 160 iliyopo sokoni, ni matumaini yetu zoezi hii litapata muitikio mkubwa kutoka kwa wanahisa wetu, ambao wana imani na benki hii, bodi na menejimenti yake kwa ujumla."

“Benki imerahisisha ununuzi wa hisa kwa kuruhusu ununuzi kwa njia za kidigitali ili kuongeza wigo wa ushiriki wa wanahisa, natoa rai kwa wanahisa kuchangamkia fursa hii ya kununua hisa kwa njia za kidigitali, au kupitia mawakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam au kwa kufika kwenye matawi yetu ya benki”, aliongeza Bi. Nanyaro.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Masoko na Uchunguzi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw. Exaut Julius aliipongeza Benki ya DCB kwa uamuzi huo uliofanyika kwa weledi na ufanisi mkubwa na kupata idhini kutoka CMSA.

Akimwakilisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa mamlaka hiyo, CPA Nicodemus Mkama, Bwana Julius alisema, serikali kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ina jukumu la kuendeleza na kusimamia masoko ya mitaji hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba shughuli katika masoko ya mitaji zinafanyika kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo ili kuleta uwazi na haki kwa washiriki wote.

“Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana itaendelea kujenga mazingira wezeshi na shirikishi ili kuwezesha taasisi katika sekta ya umma na binafsi kutumia masoko ya mitaji kupata fedha za kutekeleza miradi na shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuuza hisa kwa umma, hatifungani za miundombinu, hatifungani rafiki za mazingira, hatifungani za bluu, hatifungani za jamii na hatifungani za taasisi za serikali”, alisema Bw. Julius.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi alisema, yeye pamoja na menejimenti yote ya DCB wamejipanga kuhakikisha hadi kufikia Mwaka 2028 wanaandika upya historia ya benki hiyo sambamba na mkakati wa miaka mitano wa maendeleo ya benki hiyo wa kuhakikisha benki inaendelea kukua na kupata faida.

Alisema kwa kuthibitisha hayo, benki hiyo imeweza kutengeneza faida katika robo ya pili na ya tatu huku ikiendelea kutoa huduma za kibenki bila kusahau jukumu la kuanzishwa kwake takribani miaka 22 iliyopita ikiweka mkazo mkubwa katika huduma zake za kidigitali ili kuhakikisha watanzania wengi wanafikiwa na huduma za kibenki.

“Tumejipanga kuhakikisha benki yetu inaendeleza maono ya kuanzishwa kwake ambayo ni kusaidia miradi ya kupunguza umasikini kwa kutoa mikopo ya mitaji kwa wajasiriamali wadogo na wa kati waliokosa huduma hizi kutokana na kutokidhi vigezo vya benki ya kibiashara za wakati ule."

“Uuzaji huu wa Hisa za Upendeleo ambao sasa benki yetu inafanya kwa mara ya nne kwa vipindi tofauti utasaidia kuongeza uwezo wa benki yetu katika kuwahudumia wateja wetu na ni imani yetu pia kuanzia mwakani wanahisa wetu wataweza kuanza kupata gawio hivyo tunaomba waendelee kutuunga mkono”, alisema.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Masoko na Uchunguzi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw. Exaut Julius (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa nne kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi (wa tatu kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Bw. Peter Nalitolela, wakionesha kitabu chenye taarifa muhimu kuhusu Hisa wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi la uuzaji wa Hisa za Upendeleo za Benki ya DCB, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa DCB, Bi. Regina Mduma, pamoja na wawakilishi kutoka taasisi nyingine waliohudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, Bw. Ramadhan Mganga, akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Hisa za Upendeleo za benki hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Alisema Bodi na Menejimenti ya benki ilipendekeza na kuidhinisha uuzaji wa Hisa za Upendeleo 97,646,913 zenye thamani ya shs 10,741,160,430 kwa bei ya punguzo ya shs 110 kwa kila hisa moja. Huku bei ya soko ikiwa shs 160.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (353) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (132) MICHEZO (41) SIASA (3)

Pages