Benki ya Absa Tanzania Yashinda Tuzo 11 za Heshima Mwaka 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kushoto), akizungumza na waandishi wakati akitangaza mafanikio ya benki kwa Mwaka 2024 kupitia Tuzo mbalimbali 11 ilizopata. Pamoja naye ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga.

• Kutambuliwa kwake kunadhihirisha, Ufanisi katika Ubunifu wa Kifedha, Uongozi na kujali Wateja.

Benki ya Absa Tanzania inajivunia kutangaza mafanikio yake makubwa ya kushinda tuzo 11 za heshima mwaka 2024. Tuzo hizi zinatambua mchango mkubwa wa benki katika uwezeshaji wa kifedha, uvumbuzi, utawala bora, na huduma kwa wateja.

Tuzo muhimu ambazo benki imeshinda mwaka huu ni pamoja na:

• Chapa ya Benki Inayokua Haraka Zaidi 2024, iliyotolewa na World Brand Magazine.

• Benki ya Wateja rejareja na Wateja Wadogo na wa Kati inayokua haraka zaidi Tanzania 2024 zilizotolewa na World Economic Magazine Awards.

• Benki inayofanya vizuri zaidi katika kuwawezesha wanawake kupata huduma za kifedha Tanzania, iliyotolewa na Tanzania Women Industrial Awards.

• MD/CEO Bora wa Mwaka, iliyotolewa na Top 100 Executive List Awards.

• Hatifungani Bora ya Mwaka, iliyotolewa na Soko la Hisa la Dar es Salaam.

• Muwasilishaji Bora wa Ripoti ya Taarifa za Fedha 2023, iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)

• Mwajiri Bora anayeinukia na Mwajiri Bora katika Usimamizi na Maendeleo ya Vipaji, zilizotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

• Benki inayotoa Huduma Rafiki na Utulivu za Mikopo Tanzania, iliyotolewa na Consumer Choice Awards Afrika 2024.

• Benki inayopendwa zaidi na kufikika zaidi Kusini mwa Afrika, iliyotolewa na Consumer Choice Awards Afrika 2024.

Utendaji bora wa Benki ya Absa Tanzania mwaka 2024 umeoneshwa kupitia matokeo yake mazuri ya kifedha kwa nusu ya kwanza ya mwaka. Mapato ya jumla yaliongezeka kwa 25% kufikia TZS bilioni 105, huku faida kabla ya kodi ikipanda kwa 65% kufikia TZS bilioni 54. Amana za wateja ziliongezeka kwa 21%, zikionesha uimara wa benki hiyo na uwezo wake wa kutoa ukuaji endelevu.

Tuzo ya Chapa ya Benki Inayokua haraka zaidi inaadhimisha maendeleo makubwa ya Benki ya Absa Tanzania tangu ilipoanzishwa mwaka 2020. Ndani ya miaka minne tu, Absa imepata kiwango sawa cha imani na kutambuliwa kama benki za ndani na kimataifa zenye karibu karne moja ya historia nchini Tanzania. Tuzo hii inaonyesha ahadi ya chapa ya Absa: 'Stori yako ina Thamani', inadhihirisha kujitolea kwa benki hiyo katika kuthamini Stori za kipekee za wateja wake, kuunda suluhisho za kibunifu, na kuiwezesha jamii.

Tuzo ya Benki inayofanya vizuri zaidi katika kuwawezesha wanawake kupata huduma za kifedha inaonyesha dhamira ya Absa katika kukuza ujumuishi wa kifedha. Kupitia bidhaa kama Akaunti ya Absa She Business, benki hiyo imewawezesha wanawake wajasiriamali kupata huduma za kibenki bila gharama, msaada wa ushauri, na programu za kujenga uwezo.

Katika sekta ya SME, suluhisho maalum za Absa na ushirikiano wa kimkakati zimesaidia benki kushinda tuzo ya Benki inayotoa huduma Kwa wateja wadogo na wa Kati (SME) inayokua haraka zaidi Tanzania 2024.

Tuzo ya Benki ya Wateja Rejareja inayokua haraka zaidi Tanzania 2024 inaonyesha msisitizo wa benki hiyo katika mabadiliko ya kidijitali na urahisi wa wateja, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa huduma za uwakala na suluhisho za kibunifu kama jukwaa la malipo la Mobi Tap.

Kutambuliwa kwa Mkurugenzi Mtendaji kama MD/CEO wa Mwaka na tuzo ya Ripoti Bora za Kifedha 2023 kunathibitisha kujitolea kwa Absa kwa utawala bora, uwazi, na uongozi wa mfano wa kuigwa.

Tuzo kutoka Consumer Choice Awards, kama Benki Inayotoa Huduma Rafiki na Utulivu wa Mikopo Tanzania, zinaonyesha dhamira ya Absa ya kuwapa wateja nafasi ya kwanza katika shughuli zake.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Obedi Laiser, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, alisema: "Tuzo hizi ni ushahidi wa nguvu ya ushirikiano wetu na wateja na wadau wetu. Tunaheshimika kutambuliwa katika nyanja nyingi, na tutaendelea kujitolea kuimarisha Afrika ya Kesho kupitia suluhisho za kibenki zenye ubunifu, ujumuishi, na athari chanya.

Benki ya Absa Tanzania inapoendelea na safari yake ya ukuaji na mabadiliko, inabaki imara katika dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwawezesha jamii. Tuzo hizi ni kielelezo cha kujitolea kwa benki hiyo kwa uvumbuzi, uwazi, na kuridhisha wateja wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kushoto), akionesha Moja ya tuzo waliyoshinda wakati akizungumza na waandishi wa habari kutangaza mafanikio ya benki kwa Mwaka 2024 kupitia tuzo mbalimbali 11 walizipata. Pamoja naye ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa tatu kushoto), pamoja na baadhi ya maofisa wa ngazi za juu wa benki hiyo, wakionesha kwa waandishi wa habari, tuzo mbalimbali 11 ambazo benki hiyo imeshinda kwa mwaka 2024, alipokutana nao, jijini Dar es Salaam jana.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages