RC MAKONDA AMTAKA MKANDARASI WA KAMPUNI YA MISTECO KUKABIDHI JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITAL YA MWANANYAMALA KABLA YA DISEMBA 30



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 16 ametembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la Gorofa tano la Mama na Mtoto Hospital ya Rufaa ya Mwananyamala na kumtaka Mkandarasi wa jengo hilo Kutoka Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kuongeza kasi na masaa ya kazi ili akabidhi jengo hilo kabla ya Disemba 30 mwaka huu.


RC Makonda amesema ujenzi wa Jengo hilo ulisimama tangu mwaka 2014 lakini kupitia uongozi thabiti wa Rais Dkt. John Magufuli aliona hilo changamoto hiyo na kuamua kutoa zaidi ya Shilingi Billion 2.1 kwaajili ya kukamilisha ujenzi huo ili kupunguza kero kwa wananchi.

Aidha RC Makonda amesema Jengo hilo litaanza kutumika mwezi January mwakani ambapo ndani yake litakuwa na uwezo wa kuchukuwa Vitanda 100 vya Mama na Mtoto na fedha ya kununua Vifaa tiba ipo tayari.


Pamoja na hayo RC Makonda amesema mbali na ujenzi wa Jengo hilo Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospital ya Wilaya Mabwepande na tayari yupo kwenye hatua za kujenga Kituo cha Afya Kawe na Bunju ambapo miradi yote ikikamilika itasaidia kumaliza Changamoto za Afya Wilaya ya Kinondoni.
Share:

Benki ya NBC yatoaelimu ya bima ikiadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja

Ofisa wa Bima wa Benki ya NBC, Catherine Ngowi (kulia) akitoa elimu ya masuala ya bima n aina mbalimbali ya huduma za  bima zitolewazo na NBC kwa ammoja wa wateja wa benki hiyo,  Miryam Mjema ikiwa ni moja ya matukio katika kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo mjini Dar es Salaam hivi karibuni. Wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Bima wa benki hiyo, Benjamin Nkaka na ofisa mwingine wa NBC,  Batuli Kassim.
Ofisa wa Bima wa benki ya NBC, Emarynziana Mtega (kulia), akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kujiwekea bima na aina mbalimbali ya huduma za bima zitolewazo na NBC kwa mmoja wa wateja  wa benki hiyo kutoka Kampuni ya Mogas Tanzania Ltd, Grayson Kazeni kiwa ni moja ya matukio katika kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo mjini Dar es Salaam hivi karibuni.
Maofisa wa benki ya NBC, wakizungumza na wateja wakati wakitoa elimu kuhusu masuala ya bima kwa wateja ikiwa ni moja ya matukio ya maadhimisho ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakipozi kwa picha ya kumbukumbu katika hafla hiyo. Wafanyakazi hao walitoa elimu ya bima ikiwa ni pamoja na bidhaa mbalimbali za bima zitolewazo na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC.

NA Mwandishi wetu;

BENKI ya NBC imeendelea kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja kwa kufanya matukio sehemu mbalimbali nchini na hapo jijini Dar es Salaam ikitoa elimu kuhusu umuhimu wa bima na pia ikiwaleleza wateja aina mbalimbali ya huduma za bima zitolewazo na benki hiyo.

Akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Kitengo cha Bima wa NBC, Benjamin Nkaka alisema watanzania wanapaswa kuwa utamaduni wa kujiwekea bima wao pamoja na watoto wao dhidi ya matukio na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza wakati wowote.

Akitoa mfano wa bima hizo ni bima ya elimu ya Educare itolewayo na inayomuwezesha mzazi kuweka akiba kidogokidogo kwa ajili ya elimu ya mtoto wake pindi yatokeapo majanga yanayoweza kusababisha ulemavu wa kudumu ama kifo.

“Tumekwishakuwa na huduma hii, tunachotaka sasa ni kwa wateja kuweza kuielewa vivuri, na ndio maana tumendaa hafla kama hii ili kuwafahamisha wateja wetu na wananchi kwa ujumla huduma ya bima ya elimu ya NBC inavyoweza kumkomboa mteja,” alisema.

Alisema kwa kupitia huduma hii mteja humwekea akiba mtoto wake kidogokidogo kwa kiasi atakachopanga kwa mkataba wa muda kuanzia miaka saba hadi 18 ili kugharamia elimu ya mtoto wake.


“Bima hii ya elimu ni mpango ambao mzazi huweka akiba kila mwezi hivyo kuleta faraja moyoni kwamba endapo chochote kitatokea iwe ulemavu wa kudumu ama kifo kabla ya muda huo basi bima itagharamia elimu ya mtoto wako.

“Kiwango cha chini ni miaka saba hadi 18 na kiwango cha chini cha kuwekeza katika mpango huu kwa mwezi  ni shs 7,500/- hakuna kiwango cha mwisho cha juu. Uwekezeji katika elimu ya mtoto ni jambo pekee katika kuhakikisha malengo ya kielimu ya mtoto yanatimia ,” aliongeza Bwana Nkaka.
Share:

RC MAKONDA AELEKEZA MADUKA YOTE DAR KUFUNGULIWA KESHO SAA TANO ASUBUHI ILI KUTOA NAFASI KWA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA


Ikiwa Imesalia siku moja kabla ya kufungwa kwa zoezi la kuandikisha wananchi kwenye Daftari la kudumu la Wapiga kura kwajili ya Kuchagua viongozi wa ngazi ya Mtaa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kwa kutambua umuhimu wa zoezi hilo amewaelekeza wenye maduka kufungua maduka yao Kesho October 14 kuanzia saa tano ili kutoa nafasi kwa wananchi kwenda kujiandikisha.

RC Makonda amesema kwakuwa kesho ni Siku ya Kumbukumbu ya Miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ameona ni vyema Wananchi wote wakamuenzi Baba wa Taifa kwa kuhakikisha wanapata Nafasi ya Kutosha ya Kujiandikisha ili waweze kuchagua Viongozi wa mitaa wanaoweza kutatua matatizo yao.

Aidha RC Makonda amewasihi Wamachinga, Bodaboda, Makondakta, madereva, Viongozi wa Taasisi, wafanyakazi wa Bar, Saloon, wamiliki na wafanyakazi wa Sehemu za Starehe kuhakikisha wanajiandikisha kwenye Ofisi za Serikali ya Mtaa, Shule za Msingi,  sekondari na sehemu zilizowekwa mahema maalumu ya kujiandikisha.

EWE MWANANCHI TUMIA HAKI YAKO YA MSINGI YA KUJIANDIKISHA KWAAJILI YA KUCHAGUA VIONGOZI WENYE SIFA.
Share:

NBC yatoa wito kwa wazazi kuwafungulia watoto wao Chanua Akaunti ya NBC

Meneja Huduma Bora wa NBC, Jane Dogani akiwawekea chakula baadhi ya watoto wa wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki ya NBC, Benjamin Nkaka akizungumza na watoto wa wateja wa benki hiyo pamoja na wafanyakazi kuhusu umuhimu wa wazazi kuwafungulioa watoto wao akaunti ya Chanua na pia bima ya elimu ya educare ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao wakati wawapo hai ama wasipokuwepo katika hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa Malipo ya Ndani wa NBC, Suzyo Gwebe Nyirenda akikabidhi zawadi kwa baadhi ya watoto wa wateja wa benki hiyo katika hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Huduma Bora wa NBC, Jane Dogani akikabidhi zawadi kwa baadhi ya watoto wa wateja wa benki hiyo katika hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya watoto waliohudhuria katika hafla hiyo wakichorwa picha ikiwa ni sehemu ya shamra shamra zilizokuwepo katika kuadhimisha moja ya matukio ya mwezi wa huduma kwa wateja ambapo NBC iliandaa sherehe hiyo kwa watoto wa wateja wao.
Baadhi ya watoto walihudhuria hafla hiyo wakifurahia burudani mbalimbali zilizokuwepo katika siku hiyo ikiwa ni moja ya matukio ya NBC kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja.

Na Mwandishi wetu,


BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), imetoa wito kwa wazazi kote nchini kufungua akaunti maalumu ya watoto ya Chanua pamoja na bima ya elimu ya Educare za benki hiyo ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao pindi wawapo hai ama wasipokuwepo.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam hivi karibuni na Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki hiyo,  Benjamin Nkaka katika hafla waliyoiandaa kwa ajili ya watoto wa wateja wao ikiwa ni sehemu ya matukio ya kuadhimisha Mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC.

Mkurugenzi huyo alisema akaunti ya watoto ya Chanua ya NBC pamoja na bima ya elimu ya educare vitamuwezesha mzazi kuanza kuwekeza kidogodogo kwa ajili ya mtoto wake hivyo kuondoa hofu ya watoto kupata elimu  bora pindi  mzazi  anapoondoka duniani.

“Akaunti ya Chanua na bima ya Educare za NBC ni suluhisho la uhakika kwa elimu ya watoto, wakati mzazi awapo duniani,asipokuwepo au atakapotapa ulemavu wa kudumu, nawashauri wazazi kuwafungulia watoto wenu akaunti hii na kuanza kuwekeza pamoja na bima ya educare zote kutoka NBC,” alisema.

Kuhusu hafla hiyo Bwana Nkaka alisema NBC imekuwa na desturi ya kukutana na wateja wao mara kwa mara ikiwa ni moja ya azma yao ya kusogeza huduma zao karibu na wateja wao hivyo licha ya kuwaeleza watoto  walioambata na wazazi wao bidhaa mbalimbali zinazotolewa na benki hususan zinazowalenga watoto, lakini pia watoto walishiriki burudani za aina mbalimbali jambo ambalo ni muhimu katika malezi ya watoto.

“NBC imekuwa ikibadilika siku hadi siku tukitumia njia mbalimbali katika kuwafikia wateja wetu, licha ya kuwa na mtandao mpana wa matawi lakini pia tumeanzisha NBC Kiganjani inayomuwezesha mteja kupata huduma mbalimbali za kibenki kwa kupitia simu yake ya mkononi.

“Lakini hii haitoshi NBC inao mtandao mkubwa wa mawakala wake wakitoa huduma mbalimbali za kibenki nchini kote, lakini hivi karibuni tumeingia ushirika na Shirika la Posta ambapo wateja wetu wanaweza kupata huduma zetu za kibenki katika ofisi zote za shirika hilo mahali kote nchini,” aliongeza mkurugenzi hiuyo.

Share:

Barclays Bank Tanzania donates TZS 10m to sponsor 6 girls for vocational training at VETA

Barclays Bank Tanzania Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga (right) addresses a media conference in Dar es Salaam during the weekend to announce the bank's sponsorship of six unprivileged background girls  to receive vocational training at  the Vocational Education and Training Authority (VETA). Looking on from left are; Pact Tanzania Country Director, Marianna Balampama, VETA Project and short Course Coordinator, Mashaka Kassara and Barclays Corporate Banking Director, Brian Kalero. 

Barclays Bank Tanzania Limited under its education skills Citizenship pillar has today donated TZS 10million to sponsor 6 girls for vocational training at VETA.

The sponsorship will enable the girls from underprivileged background to receive vocational training at VETA Centers which will contribute towards improving their opportunities for developing Livelihoods and employment skills. The funding covers tuition fees, accommodation at VETA centers, and prescribed books and other learning materials.

Speaking during the event, the bank’s Head of Marketing and Corporate Relations, Mr. Aron Luhanga said, “Barclays is committed to volunteer, engage and play part in giving back to the community with aim of upskilling and empowering youth. As a pan-African bank, we manage all our Citizenship initiatives in alignment with our purpose of bringing possibilities to life.

Citizenship for us is a strategic centre of excellence that develops the business socio-economic strategy with a commitment to play a shaping role in society by becoming an “active force for good”.

Cementing more on the sponsorship, the bank’s Corporate Director, Mr. Brian Kalero said that the partnership with VETA has been generated from a business relationship the bank has with Pact Tanzania.

Commending the bank for its support, Pact’s Country Director, Ms. Mariana Balampama, said “It’s only through integrated efforts and partnerships such as these that we are going to bring sustainable impact that will benefit Tanzania for generations to come. Our work in Tanzania focuses on improving the lives of orphans and vulnerable children and this support from Barclays Bank goes a long way in helping us achieve what we have set out. We envision a Tanzania where communities are heard, capable and vibrant.”

In concluding, Mr. Luhanga gave assurance that as a bank, Barclays will continue to cement their commitment to making a positive impact in the society in which they serve by advocating change. “We’re all about bringing possibilities to life as we support initiatives that help upskill, empower people and play part to change lives, and solve communities’ challenges”, he said.
Share:

RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KUWEZESHA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO DHIDI YA WATENDAJI WASIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda October 09 amezindua Mfumo wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo kuwasilisha kero na changamoto walizonazo kwa kutumia simu ya mkononi au Computer na ujumbe wao kuwafikia watendaji kwa haraka na kupatiwa majibu ndani ya muda mfupi jambo litakalosaidia kuokoa Muda na gharama za usafiri.

RC Makonda amesema ameamua kuanzisha mfumo huo baada ya kubaini kuwa wananchi wengi wamekuwa wakifika kwenye ofisi za umma na kupewa majibu ya "Njoo Kesho" pasipokujua kuwa wamepoteza muda na nauli zao kufuata huduma.

Aidha RC Makonda amebainisha kuwa mfumo huo utakuwa ukipokea taarifa za malalamiko ya Watendaji wasiowajibika kuanzia ngazi ya Mtaa, Kata, Wilaya hadi Mkoa na taarifa zitawafikia Viongozi wote kuanzia RC Makonda mwenyewe, Mkuu wa Wilaya husika, Mkurugenzi, Katibu tawala na Mkuu wa idara.

Hata RC Makonda amewahimiza wananchi kutumia mfumo huo kueleza kero zote zinazowakabili ikiwemo Afya, Barabara, Elimu, Maji, Umeme, Miradi inayokwama pamoja na kutoa taarifa pindi wanapobaini uhalifu kwenye mtaa.

Jinsi kuwasilisha ujumbe andika neno DSM kisha eleza changamoto zako kisha tuma kwenye namba 11000 au ingia kwenye Website www.malalamiko.dsm.go.tz na ujumbe wako utapokelewa mara moja na kupewa mrejesho.

HUDUMA HII NI BURE.
Share:

KATIBU UVCCM BAGAMOYO AWATAKA VIJANA KUTOKUWA CHANZO CHA MPASUKO


Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Bagamoyo ndugu Omary Ally, (aliyesimama), akizunguimza wakati wa hafla fupi yakuwapongeza vijana wa kata ya Mapinga waliohitimu Mafunzo yaujasiriamali katika kambi maalum  kwa vijana wa wilayani humo hafla hiyo imefanyika Bagamoyo  hivi karibuni

Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Bagamoyo ndugu Omary Ally amewasihi Vijana kuwa wavumilivu hasa Katika kipindi hiki cha Uchaguzi ili kuepusha Migongano ndani ya Chama yenye kuleta Mipasuko ambayo Miaka yote ndio imewanufaisha Vyama vya upinzani kwenye Chaguzi .

Katibu huyo ameyasema hayo wakati alipoalikwa kuwa Mgeni wa Rasmi kwenye  hafla ya kuwapongeza Vijana wa kata ya Mapinga waliohitim Mafunzo ya Ujasiriamali Katika Kambi maalum ya Vijana wilayani humo  iliyofanyika kwa siku 10

Pamoja na hayo Ndugu Omary Aliwataka Vijana hao kutembea Kifua mbele kwakua Serikali ya awamu ya Tano imefanya Mengi Makubwa katika kuketa maendeleo nchini na yote yanaonekana hivyo kila wanapokaa basi wayaseme mafanikio hayo.


"Ndugu zangu Nchi yetu kwa Sasa inaongoza miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara Katika kupambana na Umasikini na jitihada hizi zinachochewa sana na Kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli hivyo tuendelee kumuombea Rais wetu Kwani Sasa Taifa letu limepiga hatua kubwa kupitia yeye " alisema Kaimu Katibu huyo
.
Katika Hafla hiyo Diwani wa Kata ya Mapinga ndugu Mbonde naye alipata Nafasi ya kueleza Utekelezaji wa ilani ya ccm Katika kipindi cha miaka minne  ambapo ameishukuru serikali kwa kufanikisha Ujenzi wa Zahanati pamoja na Shule mbili za Msingi pamoja na Shule ya Sekondari Kata ya Mapinga.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (353) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (132) MICHEZO (41) SIASA (3)

Pages