MIXX BY YAS YAONGEZA NGUVU JUHUDI ZA SERIKALI KUIMARISHA KILIMO NA VYAMA VYA USHIRIKA TANGA

Mrajis wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga, Bi. Enikia Wilfred (watatu kushoto), akikabidhi pikipiki kwa viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Maziwa Tanga (TDCU). Pikipiki hiyo imetolewa na Mixx by Yas kupitia kampeni yake ya Vuna na Mixx, kwa lengo la kusaidia TDCU katika shughuli za ukusanyaji wa maziwa kutoka kwa wakulima na kuongeza ufanisi katika mnyororo wa thamani wa sekta ya maziwa. Wengine pichani ni Meneja Biashara wa Mixx by Yas Kanda ya Pwani Kaskazini, Anwar Kisesa, pamoja na maafisa wengine kutoka Mixx by Yas na TDCU.

TANGA: Mixx by Yas imeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuimarisha sekta ya kilimo na vyama vya ushirika kwa kutoa vitendea kazi kwa vyama vya ushirika mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuongeza matumizi ya huduma za kifedha za kidijitali na kuchochea maendeleo ya wakulima.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Meneja wa Uhusiano wa Biashara na Serikali na Taasisi zake wa Mixx by Yas, Suleiman Asilia Khamis, alisema kampuni hiyo inalenga kujenga ushirikiano unaokwenda zaidi ya kuwezesha malipo kwa wakulima.

“Mixx by Yas tunaunga mkono juhudi za Serikali katika kuimarisha sekta ya kilimo, vyama vya ushirika na matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kufanya malipo kwa wakulima. Dhamira yetu ni kuhakikisha teknolojia na huduma za kifedha zinakuwa sehemu ya kuongeza ufanisi katika mnyororo mzima wa thamani wa kilimo,” alisema Khamis.

Katika hafla hiyo, Mixx by Yas ilikabidhi pikipiki na freezer kwa Tanga Dairy Cooperative Union (TDCU), vitakavyosaidia katika ukusanyaji wa maziwa kutoka kwa wakulima pamoja na shughuli za uuzaji wa maziwa.
Kwa upande wa Tanga Rural Cooperative Union (TARECU), inayoshirikiana na wakulima wa mazao mbalimbali yakiwemo kakao, ufuta, mbaazi na korosho, Mixx by Yas imetoa guta litakalosaidia kusafirisha mazao kutoka mashambani kwenda katika vituo vya ukusanyaji.

Khamis alisema hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya Mixx by Yas ya kuunganisha huduma za kifedha za kidijitali na mahitaji halisi ya wakulima, ili kuongeza ufanisi, kurahisisha malipo na kuimarisha shughuli za vyama vya ushirika.

“Hatuangalii malipo pekee. Tunataka mkulima aione Mixx by Yas kama mshirika anayekuwa naye kuanzia shambani, katika ukusanyaji wa mazao hadi anapopokea malipo yake. Huu ni mchango wetu katika kujenga kilimo chenye tija, vyama vya ushirika imara na uchumi wa kidijitali unaomfikia mkulima moja kwa moja,” alisema.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa TDCU, TARECU na Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Wakulima (AMCOS), huku makabidhiano yakiongozwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga, Bi. Enikia Wilfred.

Kwa upande wake, Bi. Wilfred aliipongeza Mixx by Yas kwa kuendelea kushirikiana na vyama vya ushirika na kuunga mkono juhudi za Serikali za kuimarisha sekta hiyo.

“Tunapongeza Mixx by Yas kwa ushirikiano huu. Vitendea kazi vilivyotolewa kupitia kampeni ya Vuna na Mixx vitasaidia vyama vyetu kuongeza ufanisi katika ukusanyaji na usafirishaji wa mazao na maziwa, na hatimaye kuongeza tija na kipato kwa wakulima,” alisema Bi. Wilfred.

Hatua hiyo inaendelea kuonyesha nafasi ya teknolojia na huduma za kifedha za kidijitali katika kusaidia shughuli za kilimo, kuimarisha vyama vya ushirika na kuongeza ufanisi katika mnyororo wa thamani wa mazao nchini.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (343) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (131) MICHEZO (41) SIASA (3)

Pages