Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi ambae pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) na (wa pili kushoto), akipokea hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Sabasaba Moshingi, kwaajili ya kutunisha mfuko wa Tasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Zanzibar lililoandaliwa na Tanzania Commercial Bank na kufunguliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia kwa Mama) na (kushoto kwa Mama) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCB Bw. Edmund Mndolwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, pamoja na uongozi kutoka Tanzania Commercial Bank akitembelea maonesho ya Wajasiriamali Wanawake wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Zanzibar lililoandaliwa na Tanzania Commercial Bank (TCB), katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar leo (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na (kulia kwa Rais ) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TCB.Bw.Edmund Mndolwa, wakimsikiliza Mjasiriamali Bi. Tatu Suleiman.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB ), Edmund Mndolwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Wajasiriamali Zanzibar lililoandaliwa na Benki hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, (TCB), Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Wajasiriamali Zanzibar lililoandaliwa na Benki hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum ya picha ya kuchora na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) Bw. Edmund Mndolwa, baada ya ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar leo 5-3-2022, na (kulia kwa Rais) Waziri wa Afrya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui . Mkurugenzi Mtendaji wa (TCB) Bw. Sabasaba Moshingi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said.
No comments:
Post a Comment