KAMPUNI YA TANGA CEMENT YATAJA FAIDA ZA KILI MARATHON

1646109572360665-2
Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Bi. Mtanga Noor (kulia), kigawa maji kwa mmoja wawashiriki wa mbio za kilimanjaro marathon ambapo kampuni hiyo imetumia zaidi ya shilingi milioni 36 kudhamini vituo vya maji na kupoozea wakimbiaji pamoja na baadhi ya wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo.
1646109556734212-3
Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya saruji Tanga Cement (TCPLC), wakishiriki mbio za km 21 wakati wa mbio za killimarathon ambapo Kampuni Hiyo imetumia zaidi ya shilingi milioni 36 kudhamini vituo vya maji na kupoozea wakimbiaji pamoja na baadhi ya wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo. 

1646109519229112-4
 Mhazini wa Kampuni ya saruji Tanga Cement (TCPLC), Frederick Emmanuel akigawa maji kwa mmoja wawashiriki wa mbio za kilimanjaro marathon ambapo kampuni hiyo imetumia zaidi ya shilingi milioni 36 kudhamini vituo vya maji na kupoozea wakimbiaji pamoja na baadhi ya wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo. 

 Wadau mbalimbali wa michezo nchini kutoka katika sekta binafsi na ya umma wameshauriwa kuendelea kujiunga na mbio za nyika za Kilimarathon kila mwaka – Ambazo kwa sasa ni mbio maarufu kupita zote nchini, kwa kutoa udhamini na vilevile kwa kupeleka washiriki. 

 Wito huo umetolewa na Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Tanga Cement, Bw Peet Brits, wakati wa mahojiano maalum kuhusu Kilimarathon mbio ambayo imekuwa ikivutia washiriki kutoka ndani ya nchi na ng’ambo, ambapo alijadili mbio hizo na manufaa yake kwa mapana.

 “ Ningependa kushauri mashirika na makampuni mengine, ya Serikali na yasiyo ya kiserikali, kujiunga na mbio hizi. Ninaposema kujiunga nina maana ya kushiriki katika mbio hizo, kudhamini na vilevile kwa kuleta washiriki kwa manufaa ya kiafya na vilevile kwa ajili ya kukuza bishara zao,” Alisema Brits. 

 Akiongelea mvuto wa mandhari ya Moshi ambako mbio hizo hufanyika mara moja kila mwaka kuwa ni rafiki na yanashamirisha mbio hizo. Meneja huyo wa biashara wa Tanga cement alisema kuwa wale ambao hawajajiunga na mbio hizo, 'wanakosa mazuri mengi’ na kuwa ‘ wanajikosesha muda mzuri wa burudani tosha’ Brits aliongeza:

 “ Nafikiri inabidi watu waendelee kujiunga na mbio hizi mwakani kwa wale wasiokuja leo waje mwakani kwa wingi wajionee, hali inavyokuwa hasa unapokuwa katika vituo vya kuwapa wakimbiaji maji, vipozeo hisia unayoipata unapokuwa hapa uwanjani wakimbiaji wanapoanza na kumalizia mbio, uwanja wa hapa Moshi ukiwa umefurika watu Kama Hivi leo….kukutana na watu wengi kiasi hicho kutoka maeneo mbalimbali ya dunia, hawatajutia kushiriki, na pengine wakajutia kwa nini miaka yote hiyo wamekuwa wakijikosesha burudani kama hii” Meneja huyo alisifia mbio za Kilimarathon, ambazo mwaka huu zinaadhimisha mwaka wa 20 tangu kuanzaishwa kwake, na kuonyesha matumaini kuwa shamrashamra za mwaka huu wa 20 zitasaidia kunogesha mbio za mwakani , ambazo ni mara ya 19 kwa Tanga Cement Kushirikki. “ Kili Marathon limekuwa ni jukwaa bora ambapo inatuwezesha kuwasiliana ana kwa ana na wateja wetu na wadau wengine. Unapata fursa ya kusikia yale ambayo huwezi kuyasikia katika mikutano ya bodi, tumekutana na wateja kuanzia wadogo hadi wale wakubwa. Kwa hiyo haya maadhimisho ya miaka 20, nina amini, yataboresha zaidi raha ya Kili Marathon,”aliongeza. 

 Kwa upande wa biashara kwa wenyeji wa Moshi, Brits alisema kuwa Kili Marathon imekuwa ni mtambo madhubuti wa kuzalisha kipato kwa mji huo, na kuwa mbio hizo zimekuwa zikitunisha mikoba ya wenyeji kuanzia wenye mahoteli, huduma za malazi, watoaji wa huduma za chakula wadogo na wakubwa, wauzaji vinywaji baridi na vileo na wengineo.”

 Aliongeza Brits: “ Si hao tu, bali pia wapo wale wanaofanya biashara pembezoni mwa barabara wameuza matunda, mbogamboga kwa wasafiri wanaoingia na kutoka mjini Moshi.. Tusisahau vilevile wageni wanaokuja Tanzania kwa ajili ya mbio hizo. 

Hao wote mwisho wa siku wamechangia katika pato kuu la taifa kwa miaka 20 mfululizo. Alisema Tanga Cement ni kati ya wadhamini wakongwe kabisa wa Killimanjaro Marathon, na kuongeza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikishirikikisha wafanyakazi wake, na kuwa mwaka huu imepeleka timu ya wakimbiaji 25, na zaidi ya 30 wamekuwa wakojitolea kugawa maji kwa wakimbiaji. 

Alisema Brits : “ Tunajivunia kuwa sehemu ya tukio maarufu kama hili la kimichezo nchini na tumefurahi kuwa ni sehemu ya historia ya Kilimarathon. Sisi tunajiona kuwa tunakua sambasamba na Kili Marathon. Wakati mbio hizi zinatimiza miaka 20, sisi tunatimiza miaka 42. Jopo letu la wakimbiaji ni sehemu ya wakimbiaji ambao wamekuwa wakishiriki kila wakati wa mashindano.

 Kwa ufupi, tumewaleta wakimbiaji kuja kushindana mbali ya kujiweka vizuri kiafya. Kuhusiana na kilichoivutia kampuni hiyo kubwa ya simenti kujiunga na mbio hizo nakutumia zaidi ya milioni 36 kwaajili ya kudhamini maji vipozeo kwaajili ya wakimbiaji , Brits alisema:” 

Tunapenda michezo, na hasa tunapenda mbio za Kilimarathon, kwa kuwa huu ndiyo mchezo pekee ambao unashirikisha wafanyakazi wetu wengi kwa mpigo, kutoka wakimbiaji hadi wasio wakimbiaji.

 Ninaposema wasio wakimbiaji nina maana ya wale waliojitolea leo hapa katika vituo vya kugawia maji na kazi za uwanjani. Kwa hiyo tunapoongelea Kilimarathon, tunaongelea Timu Simba kutoka Tanga Cement ikishiriki kwa ukamilifu.”
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages