Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Boko, Ambakisye Lusekelo (wa pili kulia) akiongoza matembezi ya Shukrani ya kilometa 5 yaliyoanzia Kanisa la KKKT - Boko na kuishia katika ufukwe wa Ndege Beach Mbweni jijini Dar es Salaam leo Machi 12, 2022. Matembezi hayo yakiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunia ambapo Umoja wa Wanawake wa Usharika huo wametumia fursa hiyo kuhamasishana katika kuwachangia watoto waliolazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambao wakisumbuliwa na ugonjwa wa saratani.
No comments:
Post a Comment