Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser (kushoto) akikata utepe kuzindua mfumo wa kidigitali unaowezesha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa njia ya mtandao wa WhatsApp katika Tawi la Absa Mikocheni jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja na Digitali, Samuel Mkuyu na Mkuu wa Wateja Binafsi wa Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi.
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi akizumgumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kidigitali unaowezesha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa njia ya mtandao wa WhatsApp jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Huduma kwa Wateja na Digitali wa Benki ya Absa Tanzania, Samuel Mkuyu akizungumza Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kidigitali unaowezesha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa njia ya mtandao wa WhatsApp.
Meneja Biashara wa Kampuni inayojihusisha na kutengeneza mifumo ya kigitali ya Fasthub Solutions, Hawa Mwakatundu akizumgumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kidigitali wa benki ya Absa Tanzania unaowezesha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa njia ya mtandao wa WhatsApp jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi wa washiriki wakimsikiliza mubashara kupitia video Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa mfumo wa kidigitali wa benki hiyo unaowezesha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa njia ya mtandao wa WhatsApp jijini Dar es Salaam leo.
Meneja wa Tawi la Benki ya Absa Mikocheni, Prisca Daudi (Kushoto) akitoa maelekezo jinsi ya kutumia mfumo wa kidigitali wa benki hiyo unaowezesha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa njia ya mtandao wa WhatsApp uliozinduliwa jijini Dar es Salaam leo. Pamoja naye ni Meneja Huduma kwa Wateja, Joan Mbeyela.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser (kushoto), Mkuu wa Huduma kwa Wateja na Digitali, Samuel Mkuyu na Mkuu wa Wateja Binafsi wa Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi (kulia) wakishangilia wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kidigitali wa benki ya Absa Tanzania unaowezesha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa njia ya mtandao wa WhatsApp jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment