Mkuu
wa Mkoa wa Katavi, Komredi Juma Zuberi Homera (katikati), akikata keki
wakati wa uzinduzi Ofisi ya wakala mkuu wa huduma ya NBC Wakala Plus
katika Manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi hivi karibuni. kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Theobald Sabi, Meneja wa Huduma za
NBC Wakala Robert Madaki, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya
hiyo Elibariki Masuke, na kulia ni na Wakala wa ofisi hiyo Emmanuel
Atimili, Hafla hiyo imefanyika hivi jana.
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi, Komredi Juma Zuberi Homera (katikati), akikata keki
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya wakala mkuu wa huduma ya NBC
Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi hivi karibuni
kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Theobald Sabi, pamoja na
maofisa wengine kutoka Benki hiyo na Wakala wa Ofisi hiyo Emmanuel
Atimili.
Taarifa
kwa Umma Mei 5 mwaka huu 2021 Wakazi wa Mkoa wa Katavi wameipongeza
Benki ya NBC kwa kuzindua NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda
kwani kwa kuwepo kwa wakala mkuu huyo kutafungua fursa za kiuchumi,
kuziendeleza pamoja na kuinua uchumi wa wafanyabiashara katika Mkoa huo.
Akizungumza
na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara waliohudhuria katika hafla
hiyo ya uzinduzi wa tawi hilo la NBC Wakala Plus, Mgeni rasmi Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Komredi Juma Zuberi Homera ameupongeza uongozi wa Benki
ya NBC kwa kuja kuwekeza katika Mkoa huu ambapo watu zaidi ya elfu moja
wamefungua akaunti katika tawi hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi, Komredi Homera aliupongeza uongozi wa Benki ya NBC
kwa kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wa Katavi. Mafunzo hayo yalifanyika
kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda. Komredi
Homera pia aliusihi uongozi wa Benki ya NBC kutoa mikopo kwa
wajasiriamli wa Katavi ili matunda ya mafunzo hayo yaonekane kwa haraka.
Aidha
Homera ameishukuru Benki ya NBC kwa kutoa msaada mifuko 300 ya saruji,
Bati 60 sambasamba na ndoo 5 za rangi katika Cho Cha Afya huku benki
hiyo ikiahidi kusimamia ujenzi wa madarasa mawili katika chuo hicho.
Homera
pia amewapongeza Benki ya NBC kwa kufika Mkoani Katavi japo alisema
kuwa wamefika kwa kuchelewa kwani fursa zipo nyingi katika Mkoa huu wa
Katavi kwani uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara upo juu pamoja
na mazao ya kimkakati.
Pia
Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliuhakikishia uongozi wa Benki ya NBC kwamba
huduma ya NBC Wakala Plus waliyoifungua katika Mkoa wa Katavi inakuwa na
kuwa tawi kamili Ili huduma kubwa za kibenki zaidi ziweze kutolewa.
“Kuzunduliwa
kwa NBC Wakala Plus hapa Katavi maana yake ni kwamba wapo wafanyakazi,
Wakuu wa Taasisi pamoja wananchi ambao akaunti zao zilikua zimelala sasa
kupitia NBC Wakala Plus wakazifufue na kuanza kutumika na kuungana na
benki nyingine zilizopo katika Mkoa wetu Ili uwekezaji huu wa Benki ya
NBC uweze kuleta maendeleo katika Mkoa wetu," alisisitiza Homera.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi alisema
kuwa wameamua kufungia NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda kwani
manispaa hiyo inakuwa kwa haraka kiuchumi na miradi mingi ya kimakakati
iliyoanzishwa na awamu ya tano inaendelea katika awamu ya sita na ni
Mkoa wenye fursa nyingi za kiuchumi wa nchi yetu na ukanda huu.
"Na
sisi NBC tumeona ni muhimu kuwa hapa tushirikiane na wananchi wa Katavi
pamoja na wafanyabiashara katika kuhakikisha kwamba fursa hizi za
kiuchumi tunaziendeleza ukizingatia nchi yetu ipo katika mkakati wa
kukuza viwanda na kuongeza thamani katika mazao hivyo hiyo ni fursa
kubwa ambayo tumeiona kwa hiyo uwepo wetu hapa utatuwezesha kutoa mikopo
kwa wafanyabiashara na wakulima Ili waweze kuongeza thamani katika
mazao yao na kununua pembejeo kama matreka na nk na kuongeza uzalishaji.”
Naye
Meneja wa huduma na bidhaa kutoka Benki ya NBC, Nd Jonathan Bitababaje
amewahakikishia wakazi wa Mkoa wa Katavi kwa Benki ya NBC ina akaunti
mbalimbali zinazomfikia kila mmoja kwa upande wake Kama Shambani
Akaunti, Kuwa Nasi Akaunti, Johari akaunti kwa ajili ya wanawake,
Akaunti za watoto, wanafunzi na Bima za kulinda Mali zao.
No comments:
Post a Comment