WAJASIRIA MALI Z'BAR WAPEWA MBINU MPYA

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

WANAWAKE visiwani Zanzibar wameshauriwa kutumia vizuri fursa ya ujasiriamali kwa lengo la kujiongezea kipato na kujiajiri wenyewe.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya New Vision Consortium (NVCT) Pily Khamis Lapda, amesema wanawake wengi hapa nchini wamekuwa wakifanya shughuli za ujasiriamali kwa mazoea jambo linalopelekea kushindwa kufikia malengo yao ya kumiliki mitaji mikubwa ya kibiashara.

Amesema zipo njia mbali mbali za kuwakomboa wanawake kiuchumi zikiwemo kupenda na kuamini shughuli za ujasiriamali kama nyenzo ya kujikomboa kiuchumi.Amewashauri wanawake nchini kujiamini pindi wanapoanzisha biashara zao sambamba na kujiwekea malengo ya kudumu ya kibiashara yatakayowasaidia kumiliki mitaji mikubwa ya kibiashara.

Mkurugenzi huyo Pily, akizungumzia malengo ya taasisi yake inayoendesha na kusimamia mafunzo ya kuyajengea uwezo wa kitaaluma makundi mbali mbali ya kijamii ili kupata uwezo wa kutumia ipasavyo fursa za ujasiriamali wenye maendeleo.“Wanawake tuwe mstari wa mbele kujifunza mbinu mbali mbali za kujikwamua kiuchumi, pia tujitume na kuwa wabunifu katika biashara zetu ili nasi tuwe miongoni mwa wajasiriamali wa kimataifa.”, amesema Mkurugenzi huyo.

Akitoa mada ya Uvumbuzi binafsi, mtaalamu wa Saikolojia na maendeleo ya vijana, Joseph Mrindo amesema wanawake waliopo katika sekta ya ujasiriamali wanatakiwa kuondokana na dhana ya ujasiriamali mdogo mdogo kwani hali hiyo inasababisha kudumaa kiakili na kushindwa kufikia malengo yao ya kumiliki biashara kunwa na makapuni.

Ameeleza kuwa Zanzibar ni sehemu muhimu yenye fursa za kibiashara hivyo wanawake wanatakiwa kutumia nafasi hiyo kujiongeza kibiashara.Mtaalamu huyo, amewasihi wajasiriamali kufuata maelekezo na mbinu mbali mbali za maendeleo ya kibiashara ili wawe na mitaji mikubwa itakayowawezesha kupewa mikopo kwa wakati na benki mbali mbali nchini.

Naye mshiriki wa mafunzo hayo, Munawar Sleiman Mbarouk amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili wajasiria mali ni ukosefu wa mitaji na ujuzi wa kufanya biashara zenye tija kwa mjasiria mali mmoja mmoja na vikundi.Mafunzo hayo ya siku mbili yanatolewa na taasisi ya New vision consortium (NVCT) iliyopo Zanzibar na jumla ya washiriki 200 kutoka taasisi binafsi na za umma wanapewa ujuzi huo wa ujasiriamali.

Wadhamini wa mafunzo hayo ni pamoja na NMB, ZSSF, ZURA na EQUITY BANK

MKURUGENZI wa New vision consortium Pily Khamis Lapda(aliyekaa katikati) akifungua mafunzo ya siku mbili ya ujasiriamali kwa wanawake wa Zanzibar yaliyofanyika katika Skuli ya Haile-Sela-ssie.
BAADHI ya washiriki katika mafunzo hayo kutoka taasisi binafsi na za umma wakifuatilia kwa makini mada mbali mbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo, huko Skuli ya Haile-Sela-ssie.
MSHIRIKI wa mafunzo ambaye pia ni mjasiria mali kutoka U.WT. jimbo la Mwera Salama Mohamed Tahir akichangia mada ya uvumbuzi binafsi.
Share:

Chuo cha Kodi Chapongezwa Kuwajengea Uwezo Wanafunzi Wake


Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani kutka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Michael Muhoja akizungumza alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inayowakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea. Kutoka kulia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Kodi (ITASO), Bi. Happines Gherabaster, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Dkt. Lewis Ishemoi na Naibu Mkuuwa Chuo cha Kodi

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Dkt. Lewis Ishemoi akizungumza wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inayowakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea.
 
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Kodi (ITASO), Bi. Happines Gherabaster akifafanua jambo wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inayowakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouely akielezea namna anavyofurahishwa na jinsi Serikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya kodi wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inatwakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea.
 
Afisa Uhusiano Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Bi. Oliver Njunwa akisisitiza jambo wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inatwakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea.
 
Mwakilishi kutoka Taasisi ya Global Education Link (GEL), Bi. Happiness Agathon akimkabidhi kwa niaba ya wenzake, mwanafunzi wa mwaka wa TATU WA Chuo cha Kodi (ITA), Bi. Nteghenjwa Kidika zawadi ya ushindi wa pili katika uwasilishaji wa mada wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inatwakutanisha  wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea. Wanafunzi hao waliwasilisha mada kuhusu hesabu za kodi na forodha. Kulia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Kodi (ITASO), Bi. Happines Gherabaster.
 
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Kodi wakifuatilia hutuba ya mgeni rasmi Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani kutka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Michael Muhoja (hayupo pichani) ambaye alimwakilisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere katika maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inatwakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea.

Mwakilishi kutoka Benki ya CRDB, Bw. Wilberforce Benda( mwnye Kaunda suti) akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha wanafunzi walioibuka washindi wa kwanza katika uwasilishaji wa mada wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inatwakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea.Wanafunzi hao waliwasilisha mada kuhusu namna ya kuandaa mipango ya kodi.
Share:

OFFICIALY INFINIX INTRODUCED IN TANZANIA PARTNERED WITH VODACOM TANZANIA.

                                                                                 
OFFICIALY INFINIX INTRODUCED IN TANZANIA PARTNERED WITH VODACOM TANZANIA.

Dar es Salaam 28thApril 2018: Infinix the premier leading Mobile company which has been doing well all over Africa has finally engage in Tanzania market by officially announcing the Brand opening at Mlimani City and the launch of one of its newest retail store today. The company is now doing well with one of its latest smartphone Infinix HOT S3, which has 20MP selfie camera with a full display of 5.7 inch. 

 Infinix Mobility is a Hong Kong-based smartphone manufacturer that was founded in 2013. The company’s headquarter are in Paris and Shanghai. Infinix mobile phones are manufactured in China and managed to penetrate all over 30 countries in the world in which is more popular in the Middle East and African countries (especially Egypt, Morocco, Nigeria, Zambia and Kenya). Currently the company promotes four product lines in a global marketplace reaching countries in Europe, Africa, Latin America, Middle East and Asia which are: ZERO, NOTE, HOT S, and HOT and for Tanzanian market Infinix Mobile will be equipped with 2GB free bundle from VODACOM Tanzania.

Both companies came together to make sure Tanzanians enjoy the speed of 4G network from VODACOM and the best smartphones from Infinix Mobile. Infinix smartphones are global developed most of them are covers 4G network.

Speaking during the press launch, Infinix Mobility Public Relation Mr, Eric Mkomoye said, “The Company is committed to build cutting-edge technology and fashionably designed dynamic mobile devices to create globally-focused intelligent life experiences through a merging of fashion + technology” .and with the brand spirit of challenging the norms, Infinix smart devices are designed specifically for the people who want to stand out, reach out and in sync with the world.

Mr. Mkomoye continued “And to make it much easier for our customers to reach us we brought to you Infinix retail shop near you. The shop is wider enough to carry more than 30 people at a time who will be assisted with professional sellers, Infinix guarantees the after sales service and provides knowledge on how to use and keep your device safe all these services are available from Mondays to Sundays, we are here to save you”. 

Vodacom’s Head of Terminal and Retail Operations Brigita Stephen said that “Vodacom  is very happy to cooperate with Infinix mobile in brand opening and the launch of Infinix mobility first retail store and for any Infinix smartphone will be equipped with Vodacom 2 GB internet bundle, Infinix buyers will only need to send word ZAWADI to special number 15300 where 12000 minutes , 10000 sms and 2 Gb free from Vodacom will be activated on  Infinix device”

She concluded “though it’s a newly brand in Tanzania but we choose to partnered with them for a reason that Infinix has the best smartphones. with unique features and another good factor is its price range which is reasonable to our customer,  you can take an example with Infinix HOT S3, is a 4G device equipped with 20MP and FACE ID technology”. 

Apart  retails stores also Infinix smartphones  will be available on Jumia online selling platform at good price for those who can’t reach  retail shops across Tanzania. 
Share:

DKT. MWAKYEMBE AKUTANA NA WADAU WA SEKTA ZA WIZARA YA HABARI BUNGENI JANA

Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Habari mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge jana Jijini Dodoma.
Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Utamaduni mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge jana Jijini Dodoma.
Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Sanaa na Mitindo mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge jana Jijini Dodoma.
Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Muziki mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge jana Jijini Dodoma.
Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge jana Jijini Dodoma.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages