WAZIRI JENISTA MHAGAMA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU KUJADILI NAMNA BORA ZAIDI YA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI


NA KHALFAN SAID, DODOMA
SERIKALI ilianzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata mafao bora na stahiki ya fidia tofauti na sheria ya zamani iliyotoa viwango vya chini vya fidia, lakini pia kuwawezesha waajiri kupata muda zaidi kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendeshaji.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama mjini Dodoma mwishoni Aprili 13, 2018, wakati akifungua mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma) na Chama cha Waajiri Tanzania, (ATE), kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.

Mhe. Waziri alisema viwango vya juu vya malipo ya fidia kwa wafanyakazi walipokuwa wanaumia kazini kabla ya sheria ya kuanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ilikuwa ni shilingi 108,000/=kwa mfanyakazi aliyepata ajali au kuumia kazini, lakini pia sheria inasema kulikuwa na malipo mengine ya shilingi 83,000/= kwa mfanyakzi aliyefariki kwa ajali au ugonjwa kutokana na kazi aliyokuwa akifanya na malipo hayo yalitegemea pia mkataba wa ajira yake unasemaje.

“Serikali ilikuja na sheria mpya baada ya kuona viwango hivi kwa ubinadamu na kwa hali halisi, vilikuwa vimepitwa sana na wakati na wafanyakazi walikuwa wanapata fidia hiyo kwa kadhia kubwa sana na viwango hivyo haviendani na ukuaji wa uchumi na kwa wakati tulionao.” Alifafanua Mhe. Waziri.

Aidha Mhe. Waziri alisema, Mfuko unafaida kubwa sio tu kwa wafanyakazi bali pia kwa waajiri na taifa kwa ujumla ambapo wafanyakazi sasa wanauhakika wa kupata kinga ya kipato kutoakana na majanga ambayo yatasababishwa na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi wanazofanya, lakini waajiri nao watapata muda zaidi wa kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendelevu wa biashara na shughuli zao kwani Serikali kupitia Mfuko itabeba mzigo wote wa gharama pindi mfanyakazi atakapofikwa na janga lolote awapo kazini.

“Pamoja na uchanga wake, Mfuko huu ambao umeanzishwa mwaka 2015 umeonyesha mafanikio makubwa katika kipindi kifupi kwani hadi sasa waajiri ambao wameshajisajili kwenye mfuko wetu ni 13,500 na wafanyakazi wao ambao wamepatwa na majanga wakiwa kazini wameshalipwa fidia na Mfuko fedha zisizopungua shilingi bilioni 2.52 kufikia Februari 2018.” Alibainisha.

Alisema Mfuko umekuja wakati muafaka kwani nchi inakwenda kwenye uchumi wa viwanda bila shaka kutakuwepo na ongezeko la ajali na magonjwa yanayotokana na uendeshaji wa shughuli katika viuwanda vyetu hivyo ni lazima kiwepo chombo kitakachosimamia majukumu haya ya fidia ili kuwapa nafasi pana waajiri kuendelea na shughuli zao za uzalishaji.


“Rais wetu wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kila wakati tunapokutana kwenye baraza la Wafanyabiashara Tanzania amekuwa akituagiza sisi wasaidizi wake, kama kuna jambo lolote linajitokeza na sekta binafsi inafikiri kwamba jambo hili bado halijaeleweka na haliko sawasawa ni wajibu wetu sisi mawaziri kuchukua hatua haraka za kukutana na kujadiliana na wadau na kushauriana na wadau husika ili kufikia muafaka na kuelewana ili kwenda pamoja na ndio maana leo tuko hapa.” Alifafanua Mhe. Waziri Jenista Mhagama.


Wakitoa ushuhuda mbele ya washiriki wa mkutano huo, Wafanyakazi waliopatwa na majanga ya kuumia au kufiwa na wenza wao, wameipongeza Serikali kwa kuanzisha Mfuko huo kwani umekuwa ni mkombozi kwa wafanyakazi.

“Mimi nilikatika mkono wakati nikitekeleza majukumu yangu ya kazi kwenye Kampuni ya Reli Tanzania, (TRL), na WCF imenilipa fidia ya mkupuo na inaendelea kunilipa pensheni ya kila mwezi, shilingi 170,000/= kwa maisha yangu yote nitakapokuwa hai.” Alisema Bw.Fortunatus Kiwale

Naye Mfanyakazi mwingine wa Kampuni ya Frank Pile International Project Limited ya jijini Dar es Salaam, Bw. Patrick Millinga, yeye alisema Mfuko umemlipa fidia ya zaidi ya shilingi milioni 31.9 baada ya kupoteza jicho lake la kushoto kutokana na kugongwa na kipande cha chuma wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi.

Mwingine aliyetoa ushuhuda wa faida ya Mfuko kwa wafanyakazi, ni mama mjane, Bi. Petronila Mligo, ambaye yeye alifiwa na mumewe katika ajali ya gari wakati akirejea kituo chake cha kazi jijini Mwanza akitokea Dodoma.

“Mfuko umenilipa fidia ya mkupuo kutokana na kifo cha mume wangu, lakini pia ninaendelea kulipwa pensheni ya kila mwezi mimi na watoto wangu wawili, ambapo kila mtoto analipwa shilingi 175,000/= na mimi ninalipwa shilingi 375,000/=.” Alisema mama huyo mjane ambaye ni mwalimu.

Akiwasilisha mada mbele ya washiriki, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema Mfuko unaendeshwa kwa msingi wa utatu ambapo katika bodi ya wadhamini ambayo ina uwakishi wa serikali, wafanyakazi na uwakilishi wa waajiri kama ambavyo Shirika la Kazi Duniani linavyotaka katika masuala haya ya fidia kwa wafanyakazi.

Alisema, katika mfumo wa zamani, mfanyakazi anapotoka au kwenda kazini endapo atapatwa na tatizo njiani sheria ya zamani haikumtambua, tofauti na sheria ya sasa ambapo inaeleza mfanyaakzi akiumia au akifikwa na umauti wakati akitoka kazini au akielekea kazini sheria ya sasa inataka afidiwe.

“Alisema Mfuko umeweka utaratibu ili kuhakikisha mfumo wa usajili wa waajiri unakuwa wa haraka na rahisi lakini pia kushughulikia masuala ya ulipaji fidia katika kipindi kifupi.” Alisema.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akihutubia wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Eric Shitindi, akitoa hotuba ya ukaribisho wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhsuu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (Wanne kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Bw. Masha Mashomba, (Wakwanza kushoto), wakisalimiana na wanufaika wa Fidia kwa Wafanyakazi wa (WCF), Bw. Patrick Millinga, (wakwanza kulia) na Bi. Petronila Mligo, (wapili kushoto), wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma, na kufanyika jengo la LAPF mjini Dodoma. Mkuta huo ulilenga kutoa elimu zaidi na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo. Wengine pichani ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Antony Mavunde, (watatu kulia), Mwakilishi wa ATE, Bw. Almasi Maige, (wapili kushoto) na Katibu Mtendaji wa TCCIA-Dodoma, Bw.Iddi Senga.
Mkutano ukiendelea

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(katikati), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Mashan Mshomba, (kulia), wakimsikiliza Niabu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.
Baadhi ya washiriki
Baadhi ya washiriki
Baadhi ya washiriki
Washiriki wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba akiwa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kushoto) na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Anselim Peter, akijibu baadhi ya hoja zilizojitokeza wakati wa mkutano huo wa majadiliano na wadau.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, (kushoto), akiwa na Bw. Mshomba.


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, (WCF), Bi. Laura Kunenge, akizungumza jambo wakati wa mkutano huo.

Mhe. Waziri Jenista Mhagama, akizungumza na waandishi wa habari.

Mhe. Waziri akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wakati akiwasili ukumbini.

Mnufaika wa Fidia, Bi. Petronila Mligo, akitoa ushuhuda wa faida anayopata kutokana na uwepo wa Mfuko, baada ya kufiwa na mumewe akiwa kwenye safarin ya kikazi.

Bw. Patrick Millinga, naye akitoa ushuhuda kutokana na Fidia aliyopata kutoka WCF baada ya kupoteza jicho lake la kushoto wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi.

Mhe. Waziri Mhagama akisalimiana namnufaika mwingine wa Fidia, Bw. Fortunatus Kiwale

Picha ya kwanza ya pamoja.
Picha ya pili ya pamoja.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages