HALMASHAURI MANISPAA KIGAMBONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ILANI YA CCM

Mwenyekiti wa CCM Mkoa Bi. Kate Kamba ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa utekelezaji wa Ilani wa chama cha Mapinduzi na kusema kuwa ameiona thamani ya fedha katika miradi yote aliyoitembelea hivyo mshikamano uliopo uendelezwe. 
Amayezungumza hayo jana mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi aliyoifanya Manispaaa ya Kigamboni yenye lengo la kuona ni naman gani Ilani ya Chama inatekelezwa. 
Akizungumza na watumishi na wananchi wanao shiriki kusimamia miradi Bi.Kamba amesema kuwa, Miradi yote inatekelezwa katika ubora na ndani ya wakati na thamani ya fedha ( Value for money) inaonekana. 
"Miradi yenu mizuri na inatekelezwa kwa ubora na wakati, mnaspidi nzuri sana hii inaonesha ni naman gani mnaushirikiano, Kigamboni ni Wilaya changa lakini mambo mnayofanya mnawazidi hata Wilaya kongwe, tumependa" Alisema Kamba 
Aliongeza kuwa ameona ushirikishwaji katika utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba jamii imeshiriki kikamilifu hali inayopelekea kuona wanao wajibu wa kutunza na kusimamia miradi yao ndio maana wameweza hata kufikia makubaliano ya kuomba punguzo la bei ya ununuzi wa vifaa vinayohitajika kwenye ujenzi miradi. 
Aidha Bi. Kamba alisema kuwa sheria ya manunuzi inagharimu sana utekelezaji wa miradi , urasimu mwingi tofauti na utaratibu wa local fundi unaosaidia kutumia fedha kidogo na miradi kujengwa kwa wakati huku thamani ya fedha ikionekana. Kamba aliwataka watumishi kuona anao wajibu na sehemu yake ya kufanya kazi na kuhudumia wnanchi ikiwa ni utekelezaji wa ilanai na kuhakikisha lengo lililowekwa linafikiwa kwa kiwango cha juu. 
Kwa upande wake a Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa alisema kwamba yeye pamoja na Madiwani , Mkurugenzi na watendaji wake wanaimba wimbo mmoja , thamani ya fedha inayoonekana katika kila mradi ni matokeo ya usimamizi uliopo ambao wamepewa na mamalaka kusimamaia. 
Ameongeza kuwa kigamboni inaweza kuwa ya kwanza kwa Halmashauri zinazotekeleza ujenzi wa makao makuu tangu kuanzishwa kwani ndani ya kipindi kifupi cha miaka 2 tangu kuanzishwa kwake na watumishi watakuwa tayari kwenye jengo lao la Utawala lenye ghorofa 3, hii imewezekana kutokana na mfumo mzuri wa matumizi ya fedha. 
Aidha alisema kuwa mfumo unaotumika wa mafundi wenyeji unaokoa kiwango kikubwa cha fedha ambazo zilikuwa zinapotea bila sababu katika mfumo wa manunuzi. 
"Nadhani tuendelee kuangali hizi sheria za manunuzi, zinazumiza sana Serikali na tuanze kufuata taratibu za kawaida, mfano mfuko wa misumari kwa mfumo wa manunuzi unaweza nunua hadi elfu 6000, wakati kawaida unanunua elfu3000 hadi elfu 3500"Alisema Mkuu wa Wilaya. 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw. Stephene Katemba alisema kuwa anashukuru kutembelewa na viongozi wake na kuona namna gani Ilani  ya Chama inatekelezwa, 
Amesema hadi sasa ameshapokea Bilion 2 kwaajili ya ujenzi wa jengo la utawala na taratibu zote zimezingatiwa za kupata mkandarasi , mradi unayobond ya kulinda( secured bond) na performance bond ( fedha zitekelezwe kwa kadri inavyotakiwa). 
Mwisho alishukuru ujio wa viongozi wa Chama na kwamba kwake ni hamasa kubwa hivyo yeye kama kiongozi atajitahidi kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa kadri ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyotaka. 
Ziara ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa iliyoambatana na viongozi mbalimbali wa Chama walipata fursa ya kutembelea mradi wa ukarabati wa Zahanati ya Buyuni, Ujenzi wa kituo cha Afya Kimbiji, Ujenzi wa miundombinu ya Shule kwaajili ya kuanzisha kidato cha tano kwenye Shule ya Sekondari Nguva, ujenzi wa jengo la utawala na ujenzi wa uanzishwaji Sekondari eneo la Shule ya Msingi Kigamboni. 


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Bi. Kate Kamba akizungumza na kutoa pongezi zake kwa Manispaa ya Kigamboni.

Baadhi ya Wakuu wa idara na vitengo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM Mkoa alipokuwa akizungumza nao
 

Jengo la wamama wajawazito likiwa kwenye hatua ya renta ​
Jengo la maabara na upasuaji likiwa katika hatua ya upauaji kama inayoonekana katika picha ​
muonekano wa jengo la kuhifadhia maiti
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kigamboni akiwa ameongozana na viongozi nyingine kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Kimbiji. ​
​ Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigamboni Dk.Charles Mkombachepa akitoa maelekezo ndani ya jengo la maabara na upasuaji.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages