Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa (wa pili kulia), akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa program ya wahitimu wa vyuo vikuu inayovilenga vyuo vikuu visiwani humo itakayowasaidia wahitimu hao kupata ajira moja kwa moja Zantel. Kutoka kushoto ni, Ofisa Rasilimali Watu wa Zantel, Saidi Habibu, Ofisa Kazi wa Idara ya Kazi Zanzibar, Juma Chumu na Juma Vuai Ameir naye pia kutoka Idara ya Kazi.
Ofisa Rasilimali Watu wa Zantel, Saidi Habibu (kushoto), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa program hiyo. Kushoto kwake ni, Ofisa Kazi wa Idara ya Kazi Zanzibar, Juma Chumu, Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa na Juma Vuai Ameir kutoka Idara ya Kazi.
Meneja Masoko wa Zantel Tanzania, Bi. Rukia Mtingwa (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya wawakilishi kutoka vyuo vikuu vya mjini Zanzibar wakihudhuria hafla hiyo.
Ofisa Rasilimali Watu wa Zantel, Saidi Habibu (kulia), akizungumza na baadhi ya wanufaika wa Program ya Wahitimu wa Vyo Vikuu ilipozinduliwa mjini Zanzibar jana. Program hii maalumu kwa wahitimu wa vyuo vikuu visiwani humo itawasaidia kupata ajira moja kwa moja Zantel. Kutoka kushoto ni, Benazir Abdulhakim Omar, Thaurat Ali Abdallah, Ilham Mohamed Haji na Alli Hemed Salum.
Mmoja wa wanufaika wa program hiyo, Ally Hemed Salum (kulia), kutoka Chuo Kikuu Zanzibar, akijitambulisha.