Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amekagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa miundombinu ya kituo cha afya Songwa pamoja zahanati ya Maganzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Katika ziara hiyo Telack alikagua ujenzi wa chumba cha upasuaji na maabara katika kituo hicho cha afya ambayo unaotekelezwa kwa fedha zilizotolewa na Benki ya Dunia (WB) sh. milioni 400.
Akiwa Songwa aliwapongeza wananchi kwa akujitolea katika shughuli za maendeleo umoja na kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha wanapata maendeleo katika maeneo yao ikiwa ni kuboresha huduma.
“Niwapongeza wananchi kwa kujitolea kushiriki shughuli za ujenzi na tumekuja hapa tumeona mmejitokeza kwa wingi kujenga kituo chenu siku. Siku zote umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu kazi itakwenda haraka na kwa muda mfupi kwa sababu ninyi mmeamua kusema kile kitu ni cha kwenu,” alisema.
Mhe. Telack aliwataka wananchi kuwapa ushirikiano watumishi wa afya ambao wanawahudumia na kutoa taarifa kwa viongozi wao endapo wanaona wanakwenda kinyume cha taratibu za kazi.
Pia aliwataka watumishi wasivunjike moyo kutokana na baadhi ya changamoto zinazojitokeza pindi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao huku akiwaahidi kuwa Serikali iko nao bega kwa bega.
Awali akiwasilisha taarifa ya Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba alisema huduma ya upasuaji katika kituo hicho cha afya itaanza baada kukamilika kwa majengo ya upasuaji.
Alisema Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi, Serikali Kuu na wadau mbalimbali wa maendeleo wanaendelea kujenga vituo vya afya na zahanati kwa kutenga fedha kwa ajili ya ukamilishaji.
Mhe. Taraba aliongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri imetenga jumla ya sh. 100,000,000 kwa ajili ya kukamilisha jengo la afya ya baba, mama na mtoto katika hospitali ya wilaya.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na watumishi pamoja na wananchi katika viwanja vya kituo cha afya cha Songwa alipofanya ziara kukagua mradi wa afya. Wengine pichani kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba na diwani wa kata ya Songwa, Abdul Ngoromole.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na wananchi wanaojitolea nguvu kazi akiwa katika mradi wa upanuzi wa kituo cha afya Songwa wilayani Kishapu.
Sehemu ya watumishi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao viwanja vya kituo cha afya Songwa.
Mganga mfawidhi wa zahanati ya Maganzo, Sam Phillip akitoa maelezo kuhusu kituo hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack alipokitembelea.
Wananchi wa kata ya Songwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack viwanja vya kituo cha afya Songwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na watumishi pamoja na wananchi katika viwanja vya kituo cha afya cha Songwa alipofanya ziara kukagua mradi wa afya.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akitoa taarifa ya wilaya kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na ujumbe kutoka mkoani alipowasili ofisini kwake tayari kwa kuanza ziara.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya, Peter Mwita akitoa maelezo kuhusu shughuli za afya katika zahanati ya Maganzo.
No comments:
Post a Comment