KUWAIT KUING'ARISHA DODOMA KWA BARABARA

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem, akizungumzia uhusiano mzuri ambao umeendelea kuwepo kati ya Tanzania na Kuwait alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)(hayupo pichani), ofisini kwake Mjini Dodoma.
Maafisa Waandamizi wa  Wizara ya Fedha na Mipango na Ubalozi wa Kuwait wakifuatilia kwa umakini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (hawapo pichani) kuhusu ujenzi wa barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma,  katika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma.
 Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga (Kulia) na Afisa mwandamizi kutoka Ubalozi wa Kuwait wakifuatilia mazungumzo ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) kuhusu ufadhili wa ujenzi wa barabara za Mkato za kuingia Makao Makuu ya Nchi Mjini Dodoma.
Msaidizi wa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Bw. Edwin Makamba na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Hangi Laban, wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri huyo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (hawapo pichani), Mjini Dodoma.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) akimkabidhi zawadi Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) alipomtembelea kwa mazungumzo Mjini Dodoma.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) akiagana na mwenyeji wake  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) alipomtembelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akizungumza jambo na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga (katikati) baada ya kuagana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (hayupo pichani) alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 207.3, sawa na shilingi bilioni 466.4, kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko wa kuingia katikati ya mji wa Dodoma pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma, yenye urefu wa kilometa 257.
Ahadi hiyo imetolewa mjini Dodoma na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Jassem Ibrahim Al-Najem, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Balozi Al-Najem amesema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko za kuingia na kutoka mjini Dodoma zitasaidia kuondoa msongamano wa magari yanayopita katikati ya mji huo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na vyombo vya moto baada ya Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma.
Aliahidi kuwa nchi yake kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait na taasisi washirika (Mifuko ya Waarabu) wa mfuko huo, wataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa ufadhili wa ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya miundombinu na kilimo ili iweze kukuza uchumi na maisha ya watu wake.
Katika kipindi cha miaka 40, Serikali ya Kuwait, kupitia Kuwait Fund, imeipatia Tanzania mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 608 kwa ajili ya kutekeleza miradi 14 ya kiuchumi katika sekta za barabara, kilimo, umeme, Maji na Afya.
Baadhi ya miradi hiyo ambayo imekamilika ni pamoja na barabara ya Dar es Salaam hadi Somanga inayohusisha pia ujenzi wa Daraja la Mkapa, Kiwanda cha Karatasi Mufindi, Mradi wa kuzalisha Umeme unaotokana na nguvu ya maji-Mtera, na gharama za upembuzi yakinifu wa upanuzi wa Bandari ya Zanzibar.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake wa Maendeleo wa Kuwait kwa kuisaidia nchi kutimiza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia mikopo yenye gharama nafuu inayotolewa na taasisi hiyo.
Dkt. Mpango alisema kuwa mwaka jana, Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait uliipatia Tanzania mkopo nafuu wa shiingi bilioni 115 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Chaya hadi Nyahua (km 85) kwa kiwango cha lami pamoja na mradi wa maji safi na salama wa miji ya Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro na sehemu ya eneo la wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wenye thamani ya shilingi bilioni 77.

Mradi mwingine ni ufadhili wa ukarabati wa hospitali ya Mnazi Mmoja-Zanzibar utakaogharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 13.6 sawa na shilingi bilioni 31.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages