MENEJA MPYA PARK HYATT ZANZIBAR KUSHIRIKI KUINUA VIPAJI VYA VIJANA

Meneja Mpya wa Hoteli ya Park Hyatt ya Zanzibar, Nicolas Cedro, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuzungumzia mipango ya hoteli hiyo katika kuinua vipaji vya vijana walio katika shule zinazofundisha masomo ya hoteli. Kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Park Hyatt Zanzibar, Milvas Burnice.

Hoteli ya Park Hyatt Zanzibar imemtambulisha Nicolas Cedro kama meneja mpya atakayeendesha hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota tano iliyopo katika eneo la hifadhi malum ya UNESCO kisiwani humo katika mji wa Stone Town.

Cedro ambaye analeta uzoefu mkubwa kutoka katika sekta ya hoteli amefanya kazi katika hoteli zenye chapa maarufu duniani kama Hyatt, Melia, La Manga and Marriott na pia ni mwanachama wa shirikisho la kimataifa la wahusika wa masuala ya vyakula linalojulikana kwa kifaransa kama “La Confrerie de la Chaine des Rotisseurs.”  Cedro ambaye ana Shahada mbili za masuala ya vyakula na uendeshaji hoteli kutoka chuo kikuu cha hoteli kilichopo Nice nchini Ufaransa pia ana Shahada ya uzamili ya uendeshaji wa hoteli kutoka katika chuo kikuu cha E Cornel.

Cedro alianza kazi kama mpishi akiwa nchini Hispania na toka wakati huo ameshafanya kazi katika nchi mbali mbali duniani zikiwemo Hispania, Ufaransa, Qatar, Yordani na Tanzania bara na kisiwani Zanzibar. Meneja huyo anasifika kwa uadilifu wake katika uongozi na kuhamasiha ubora katika kazi na pia anazungumza lugha za kifaransa, kiingereza na kihispania.

Katika kipindi cha miaka 25 ambacho amekuwa akifanya kazi amewahi kupata tuzo mbali mbali za ubora za kimataifa ikiwemo ya “Mkahawa Bora” Hoteli ya La Manga nchini Hispania na pia amewahi kupika kwa ajili ya watu maarufu wakiwemo Rais wa zamani wa Ufaranza Jacques Chirac na Mfalme wa Malaysia. Uzoefu wa Cedro, elimu, ujuzi wa lugha pamoja na ubunifu ni vitu muhimu ambavyo meneja huyo atatumia katika kujenga sifa na ubora wa hoteli hiyo na pia kwa wafanyakazi.

“Napenda kufanya kazi katika bara la Afrika na hasa katika kisiwa cha Zanzibar. Ni mahali ambapo kuna mazingira mazuri na watu wenye upendo. Nimeshafanya kazi Tanzania kwa zaidi ya miaka mitatu sasa katika hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro kama mkurugenzi wa chakula na vinywaji, Melia Zanzibar na sasa hapa Park Hyatt Zanzibar. Nikiwa Tanzania nimefanya kazi katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro ya Dar es Salaam kama. Nimesikia furaha kubwa sana kupata nafasi hii ya kuendesha hoteli hii na nategemea kutumia ujuzi na uzoefu wangu ili kuleta ladha ya kipekee katika chakula na pia huduma tutakazowapatia wateja wetu,” alisema Cedro.

Cedro ambaye alizaliwa mjini Nice nchini Ufaransa, alianza kazi ya upishi akiwa kijana wa miaka 17 na hivyo anatambua umuhimu wa kuibua na kulea vipaji vya vijana. Akiwa kisiwani Zanzibar Cedro anategemea kushiriki katika shughuli za kijamii kwa kushirikiana na shule mbali mbali za kisiwani hapo za mapishi ili kusaidia vijana wenye vipaji vya upishi waweze kupata ujuzi wa kimataifa alio nao na hivyo waweze kujiendeleza katika fani hiyo na kuitumia kama njia ya kujiinua kiuchumi.

Hoteli ya Park Hyatt Zanzibar ni Hoteli ya kipekee na yenye historia ndefu hasa kwa kuwa katika eneo maalum lililotengwa kama urithi na shirika la kimataifa la UNESCO. Hoteli hiyo inatumia majengo mawili moajawapo ni  jengo ambalo lililojengwa katika miaka ya 1847 hadi 1850 na aliyekuwa rafiki wa mtawala wa wakati huo Sheikh Seyyid Said. Jengo hilo linalojulikana kama ‘Mambo Msiige’ ni mfano mzuri wa majengo ya kitamaduni ya Zanzibar likiwa na mandhari ya kiarabu na linasadikika kuwa ni imara kutokana na udongo wake uliotumika kujenga uliokuwa umechanganywa na maelfu ya mayai.

Hoteli hiyo iliyosheherekea miaka mitatu toka kuanzishwa kwake tarehe 8 Machi mwaka huu, imejijengea umaarufu mkubwa kwa kipindi kifupi kwa wageni wa kimataifa na nchini. Hoteli ya Park Hyatt Zanzibar inashiriki ipasavyo katika kukuza sekta ya utalii kisiwani humo na kutangaza kisiwa cha Zanzibar kama moja ya maeneo ya kipekee kwa utalii.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages