Marekani yataka Armenia na Azerbaijan kukumbatia Diplomasia


Na Patrick Nduwimana | Washington DC | Waziri wa mambo ya nje wa marekani Mike Pompeo amezisihi Armenia na Azerbaijan kufikia suluhisho la kidiplomasiya kuhusu mzozo kati yao wa kudhibiti jimbo lenye ugomvi la Nagorno Karabakh, ambako ghasia zilizoanza miezi miwili iliopita ziliendelea jana jumanne, licha ya mkataba wa kusitisha mapigano uliofikiwa na pande zote mjini Washington.

Akiwa ziarani nchini India, Pompeo alizungumza kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan pamoja na rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev.

Pompeo amewashinikiza viongozi hao wawili kutekeleza ahadi zao za kusitisha mapambano na kutafuta suluhisho la kidiplomasiya, taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya marekani imesema.

Jumanne, nchi mbili kila mmoja imeishtumu nyingine kushambulia ngome zilizoko nje ya Nagorno Karabakh, baada ya mkataba wa sitisho la mapigano uliopatikana kutokana na juhudi za waziri Pompeo.
Share:

FAIDA YA BENKI YA NMB YAPANDA KWA ASILIMIA 76 KATIKA KIPINDI CHA ROBO YA TATU YA MWAKA 2020

Benki ya NMB imepata ongezeko la asilimia 76 la faida kabla ya kodi kwa kipindi kilichoishia Septemba 30, 2020.

Kwa miaka mitano sasa, Tanzania imeshuhudia ukuaji imara wa uchumi uliowezeshwa na sera thabiti za kiuchumi za Serikali ya awamu ya Tano. Maendeleo haya ya kiuchumi, mazingira rafiki ya kibiashara, pamoja na utekelezaji mzuri wa mikakati ya benki ya NMB ni sababu kuu zilizopelekea ongezeko hili la faida katika robo ya tatu ya mwaka 2020. Katika kipindi hiki faida kabla ya kodi ya Benki ya NMB imepanda kwa 76% kutoka Shilingi bilioni 118 katika robo ya tatu ya mwaka 2019 hadi shilingi bilioni 208 mwaka huu, wakati faida baada ya kodi ikipanda kutoka shilingi bilioni 82 hadi shilingi bilioni 145 ambayo ni sawa na ongezeko la 77%.

Pia katika kipindi hiki, mkakati wa Benki ya NMB wa kukuza vyanzo vya mapato umejidhihirisha kwa ongezeko la mapato yatokanayo na uendeshaji kwa 14% kutoka bilioni 527 katika robo ya tatu mwaka 2019 hadi bilioni 600 katika robo ya tatu ya mwaka huu (2020). Katika kipindi hiki pia programu za Benki za kudhibiti gharama za uendeshaji na matumizi ziliimarishwa na kusababisha uwiano mzuri wa gharama na mapato kwa 52%.

Vile vile, Benki ya NMB kama mwezeshaji mkubwa wa maendeleo na uchumi nchini, imeweza kukuza rasilimali zake kwa 15% kutoka shilingi trilioni 6.1 kipindi kama hiki mwaka jana hadi trilioni 7 katika robo ya tatu ya mwaka 2020; hili limesababishwa na ongezeko la amana za wateja kwa 15% na ongezeko la mikopo kwa wateja la 16%.

Benki yetu pia imepata mafanikio makubwa katika eneo la ukopeshaji kwa kupunguza tengo la mikopo chechefu kwa asilimia 22 ukilinganisha na kipindi husika mwaka 2019.

Kwa matokeo haya ya utekelezaji kwa kipindi hiki, Benki ya NMB imeendelea kuimarisha mtaji wake juu ya kiwango kilichowekwa kisheria na Benki Kuu ya Tanzania cha asilimia 12.5. Hiki ni kiashiria muhimu sana kuthibitisha afya ya Benki ya NMB kuendelea na biashara yake kwa miaka mingi ijayo.

Akitangaza matokeo ya robo ya tatu ya mwaka 2020 ya Benki hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna alisema kuwa matokeo haya yamesababishwa na kukua kwa haraka kwa uchumi wa Tanzania, sera wezeshi na mwendelezo wa ukuaji wa pato la taifa kwa miaka ya hivi karibuni kama ilivyodhihirishwa kwa nchi yetu kuingia kwenye uchumi wa kati mwezi Julai mwaka 2020. Haya yote yamesababisha sekta ya kibenki kufanya vizuri, ikiwemo Benki ya NMB.

Bi. Zaipuna alisema kuwa “utendaji mzuri wa kifedha wa Benki ya NMB mwaka wote wa 2020 ni kielelezo kizuri cha ufanisi wa utekelezaji wa mikakati ya Benki, ubora wa wafanyakazi wetu na imani ya wateja wetu kuendelea kutumia huduma zetu za kibenki. Tunaendelea kuwashukuru wateja wetu, wanahisa wote na wafanyakazi wetu wote kwa matokeo haya chanya”.

Ni katika muktadha huo, wiki iliyopita, benki ya NMB ilipata tuzo ya Benki Salama zaidi Tanzania kwa mwaka 2020 itolewayo na jarida la kimataifa la Global Finance la New York, nchini Marekani. Ushindi huu umepatikana miezi kadhaa tangu jarida la Euromoney la London liitangaze Benki ya NMB kuwa Benki Bora Tanzania kwa miaka nane mfululizo.
Share:

TANZANIA’S TELECOMS SECTOR: A POWERFUL FORCE FOR POSITIVE ECONOMIC CHANGE

Ndechao Sangawe | UDBS | The scale of technological change continues to unfold at a dramatic pace. Today, many of the advances in mobile-assisted technology would have not been imaginable at the beginning of the 21st century.

As these advances take place, it is not surprising that the overall data traffic is on the rise and is set to continue to increase in years to come. For example, research released by the United Nations Conference on Trade and Development suggests that global data traffic is set to increase from 46,000 GB per second in 2017 to 150,700 GB per second by 2022.

Given Africa’s young and growing population, it is easy to see how these countries’ citizens will play a significant part in the upward trajectory of global data traffic.

For Tanzania specifically, it is fair to say that digitalization has emerged a key trend for a number of years now. Indeed, the country has seen its digital landscape grow from strength to strength as more and more people seek to take advantage of the benefits that digital tech affords.

For example, this summer, the TCRA announced that the overall use of mobile money in Tanzania continues to rise, with the total number of registered accounts rising from over 27 million in April to 29 million by the end of June.

This growth shows that mobile money has become an essential tool for how people manage their finances.

Meanwhile, it should be noted that this is also the result of the efforts made by the country’s telecoms sector to invest in services and technology that suit the needs of their customers.

One good example is Tigo Tanzania. Tigo’s mobile money service – Tigo Pesa – has provided its customers with a fast and reliable method for depositing and transferring money.

In addition, Tigo Pesa removes the need for customers to make regular trips to the banks, meaning customers can keep track of their finances simply through the click of a button.

Services like Tigo Pesa provide countless customers with a new way of managing their finances.

Tanzania’s telecoms sector has shown that it is a powerful force for positive change.

Going forward, it is now more important than ever that stakeholders come together to provide the necessary support for the sector through sensible regulation and mutual cooperation. This will not only help ensure telecoms operators can better serve future customers, but also ensure that positive impacts of the sector continue to be enjoyed for years to come.

As these advances take place, it is not surprising that the overall data traffic is on the rise and is set to continue to increase in years to come. For example, research released by the United Nations Conference on Trade and Development suggests that global data traffic is set to increase from 46,000 GB per second in 2017 to 150,700 GB per second by 2022.

Given Africa’s young and growing population, it is easy to see how these countries’ citizens will play a significant part in the upward trajectory of global data traffic.

For Tanzania specifically, it is fair to say that digitalization has emerged a key trend for a number of years now. Indeed, the country has seen its digital landscape grow from strength to strength as more and more people seek to take advantage of the benefits that digital tech affords.

For example, this summer, the TCRA announced that the overall use of mobile money in Tanzania continues to rise, with the total number of registered accounts rising from over 27 million in April to 29 million by the end of June.

This growth shows that mobile money has become an essential tool for how people manage their finances.

Meanwhile, it should be noted that this is also the result of the efforts made by the country’s telecoms sector to invest in services and technology that suit the needs of their customers.

One good example is Tigo Tanzania. Tigo’s mobile money service – Tigo Pesa – has provided its customers with a fast and reliable method for depositing and transferring money.

In addition, Tigo Pesa removes the need for customers to make regular trips to the banks, meaning customers can keep track of their finances simply through the click of a button.

Services like Tigo Pesa provide countless customers with a new way of managing their finances.

Tanzania’s telecoms sector has shown that it is a powerful force for positive change.

Going forward, it is now more important than ever that stakeholders come together to provide the necessary support for the sector through sensible regulation and mutual cooperation. This will not only help ensure telecoms operators can better serve future customers, but also ensure that positive impacts of the sector continue to be enjoyed for years to come.
Share:

Donald Trump amuapisha Amy Coney Barrett kuwa Jaji katika Mahakama Kuu Marekani!


Baraza la seneti la marekani limemuidhinisha jaji Amy Coney Barret kwa kura 52 dhidi ya 48 kuwa jaji kwenye mahakama ya juu ya marekani kuchukua nafasi ilioachwa na marehemu jaji Ruth Bader Ginsburg.

Ma seneta karibu wote wa chama cha republican wamepiga kura kumuidhinisha jaji Barret. Seneta mrepublican wa jimbo la Maine Susan Collins ameungana na ma seneta wa democrats wote kwa kutomuudhinisha jaji Barret.

Jaji Barret ni jaji wa 3 kuteuliwa na rais Donald Trump kwenye mahakama ya juu. Mahakama hiyo sasa itakua na majaji 6 wenye msimamo wa kiconservative na wa tatu wenye msimamo wa kiliberali.

Jaji Barret ameapishwa katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya nchi hiyo White House.
Share:

RC KUNENGE AWATAKA BODABODA KUWAFICHUA WAHALIFU, ASEMA SERIKALI ITAENDELEA KUWAWEKEA MAZINGIRA BORA YA KAZI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewataka waendesha Bodaboda na Bajaji kuwa mabalozi wazuri wa kulinda amani na utulivu wa Mkoa huo na kuwaomba kutoa taarifa pindi wanapobaini watu au kundi la watu wahalifu.

RC Kunenge ametoa kauli hiyo leo wakati wa mkutano na waendesha bodaboda na Bajaji uliofanyika viwanja vya Mnazi mmoja jijini humo ambapo amesema kazi yao imewafanya wakutane na watu wa aina mbalimbali ikiwemo wahalifu hivyo ni vizuri wakashirikiana na jeshi la polisi pindi wanapoona viashiria vya uvunjifu wa amani.


Aidha RC Kunenge amewahakikishia ushirikiano na Serikali kwenye masuala mbalimbali huku akiwahimiza kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa na Serikali kupitia Halmashauri.

Pamoja na hayo RC Kunenge amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli imefanya kazi kubwa Katika kuwatatulia changamoto na kero zilizokuwa zikiwakabili na itaendelea kuwawekea mazingira Bora na salama ya kufanya kazi ili kuhakikisha ajira yao inaheshimika na kuwanufaisha kiuchumi.


Hata hivyo amewahimiza kujitokeza kushiriki kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika October 28 kwa kuwachagua Viongozi wanaofaa.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam, RPC Ilala, makamanda wa Polisi, na Bajaji pamoja na waendesha Bodaboda na Bajaji.
Share:

TWIGA A TRIUMPH OF PARTNERSHIP

Barrick President and Chief Executive, Mark Bristow addresses a media conference in Dar es Salaam, Tanzania on 23rd October this year about the success story of Twiga Mineral Corporation. Twiga is a joint venture between Barrick and the Government of Tanzania.
Members of international and Tanzania local media at work during the Barrick President and Chief Executive, Mark Bristow press conference in Dar es Salaam on 23rd October this year. Twiga is a joint venture between Barrick and the Government of Tanzania.

Dar es Salaam | Tanzania | Barely a year after it was established, Twiga Minerals Corporation has demonstrated the value-creating capacity of a true partnership between a mining company and its host nation, Barrick president and chief executive Mark Bristow said here today at a press briefing following his quarterly mine visits.

Twiga is a joint venture between Barrick and the Government of Tanzania, and oversees the management of Barrick’s assets in the country as well as the implementation of the economic benefit-sharing agreement. It was formed when Barrick took over the operations of the former Acacia Mining in September last year and subsequently entered into a framework agreement with the government. In terms of the agreement, Barrick will pay the government $300 million to settle past disputes with Acacia.

In addition to the first $100 million tranche of the settlement, Barrick’s assets in Tanzania have since paid more than $200 million to the government in taxes and royalties, and last week Twiga declared a maiden interim dividend of $250 million.

The fact that so much value has been delivered in such a short time is a tribute to the power of what I believe is the first partnership of its kind in Africa. With the framework agreement now fully implemented, we have settled most of the landowner disputes and are well on our way to ensure that we are fully compliant with our environmental permits as well as with the government’s local content legislation,” Bristow said.

A rehabilitated and re-energized North Mara is ahead of plan in the year to date and Bulyanhulu has resumed underground mining operations and is scheduled to restart processing of underground ore by the end of 2020 as a long-life underground mine. We are gearing up to potentially make North Mara and Bulyanhulu into a combined Tier One complex, capable of producing at least 500,000 ounces of gold annually for more than 10 years in the lower half of the industry’s cost profile1. We shall also be looking to expand the life of operations as well as other new Tanzanian opportunities within the Twiga framework.

Barrick has been awarded 10 new exploration licenses in Tanzania and plans to spend $8 million on exploration there this year.

The company’s commitment to stakeholder partnership encompasses its host communities and a community development committee has already been established at North Mara. On the environmental front, a comprehensive water management plan is being implemented. Since Barrick assumed operational control in 2019 some 50% of the water in the North Mara tailings dam has been removed to date.
Share:

Tanzia: Mtangazaji wa TBC, Elisha Elia Afariki Dunia!


Mtangazaji wa Shirika la Habari Tanzania (TBC), ELISHA ELIA MWAKAGALI amefariki Dunia hii Jumamosi ya leo, Oktoba 24, 2020 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokua amelazwa kwa matibabu. 
Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba amethibitisha kutokea kwa msiba huo.


Bwana Ametoa! Bwana Ametwaa! Jina la Bwana Lihimidiwe! Amen!

Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (339) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (131) MICHEZO (41) SIASA (3)

Pages